Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.
“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo
Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.
“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.