Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Mkuu, hebu muwe mnatumia akili hata kidogo na kuacha propaganda na utapeli wa wazi. Hivi Membe anachukuaje fomu huko CCM ikiwa alifukuzwa uanachama na sasa si mwanachama wa CCM?
Mdau..kwani kuna mahali kamtaja Membe..? Au mie sijaelewa hapa...
 
Baada ya Mheshimiwa raisi kuvunja Bunge na wagombea mbali mbali kujitokeza kuchukua fomu za kugombea uraisi!hadi sasa kachero mbobezi Benard Membe hajajitokeza hadi sasa!kwani uko wapi? ulituahidi utanuka mbona harufu sisikii???

Tupe matumaini kama upo mbioni au ndio basi tena!!kwa maana mwenyekiti ameshachukua fomu sisi wakulima wa korosho wa huku mtwara tunakusubiri kwa hali na mali tukuunge mkono!!!

Kama kuna mwakilishi wake au yeye mwenyewe humu jukwaani aje atuambie kulikoni!ukimya wako unatutisha sisi ambao tunasubiria kunuka kwako tena kwa hamu ili tunuse!!!!!!Jitokeze!tuambie ili tuondoe duku duku letu!!
 
downloadfile-360.jpg

Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo

Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
Kusoma na kuandika tu ndiyo shida ya bunge letu kuwa na watu wa aina ya Bulembo
 
Mbona wakati wa kina Mkapa na kina Kikwete na Mwinyi wanachama wengi walijitokeza kuchukua form?
downloadfile-360.jpg

Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo

Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
 
Atachukua form tu ingawa nasikia katibu anakimbia ofisi kama wale ma DED wanavyo kimbiaga wagombea wa cdm wakati wa kurudisha form kwenye chaguzi za marudio
Huyu mgombea ni miongoni mwa wanachama wa ccm ambao ni mbishi na aliapa kugombea urais wa JMT akimpinga rais anaemaliza kipindi chake cha miaka mitano ya awali.
CCM ina tamaduni yake, mgombea wake kutoshindanishwa kwa muda wa miaka kumi,akimaliza ndipo wengine hugombea hiyo nafasi.
Lakini Membe alipinga na akaahidi kuuvunja utamaduni huo ,kulikoni yupo kimya?,na muda unayoyoma wa kutafuta wadhamini nchini?,au kakubali yaishe baada ya kichwa kuelekezwa kibla ?,

Je?anao uwezo wa kupambana na ccm nje ya ccm?,anaejua habari za huyu gwiji na kachero mbobezi atujuze tafadhali
 
Wanajisikia aibu kubwa sana mbele ya umma wa watanzania na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Ila sema hawana jinsi ya kulisemea maana midomo yao imepigwa kufuli
Kwamba CCM anyetakiwa kuchukua fomu ya kugombea urais kisheria ni mmoja tuuuuu???????
Bahati mbaya sana sheria za nchi, katiba na kanuni za CCM hazisemi hivyo!!!!. Sasa kafundisha somo gani zuri?????
Laiti angesema kuwa kwa mazoea yetu CCM mgombea urais ni mmoja na fomu imechapishwa moja tuuuuuu.
 
Alifukuzwa kwenye kikao kipi? Unamfukuzaje mtu kwa maneno tu bila ya kumkabidhi barua?

Membe hakuwa mwana chama kama ulivyo wewe huko kwenu mbwinde, Membe alikuwa ni kiongozi wa ngazi za juu ndani ya ccm. Hawezi kufukuzwa kama utakavyo fukuzwa wewe.
Mkuu, hebu muwe mnatumia akili hata kidogo na kuacha propaganda na utapeli wa wazi. Hivi Membe anachukuaje fomu huko CCM ikiwa alifukuzwa uanachama na sasa si mwanachama wa CCM?
 
Ndiyo kisheria bado ni mwana ccm maana hakuna barua mliyo mpatia ya kumfukuza
Mkuu kadri siku zinavyozidi kwenda wana CDM mnachanganyikiwa na kupoteza kumbu kumbu,

Agombee uraisi kwani Membe ni mwanachama wa CCM ?
 
Back
Top Bottom