Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Baada ya Mheshimiwa raisi kuvunja Bunge na wagombea mbali mbali kujitokeza kuchukua fomu za kugombea uraisi!hadi sasa kachero mbobezi Benard Membe hajajitokeza hadi sasa!kwani uko wapi?ulituahidi utanuka mbona harufu sisikii???Tupe matumaini kama upo mbioni au ndio basi tena!!kwa maana mwenyekiti ameshachukua fomu sisi wakulima wa korosho wa huku mtwara tunakusubiri kwa hali na mali tukuunge mkono!!!
kama kuna mwakilishi wake au yeye mwenyewe humu jukwaani aje atuambie kulikoni!ukimya wako unatutisha sisi ambao tunasubiria kunuka kwako tena kwa hamu ili tunuse!!!!!!Jitokeze!tuambie ili tuondoe duku duku letu!!

Bashiru alimuita akakataa kwenda sasa hiyo fomu atachukuwa wapi?
 
Huyu Bulembo ndo msemaji wa CCM? Au Polepore Kakoroneka?
 
downloadfile-360.jpg




“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo

Kwa hiyo akishinda au ashinde, kwa sheria za chama ni lazima rais awe katika vipindi viwili. Ahsante mheshimiwa kwa kuliweka hilo wazi.
 
Sasa kwa nini Magufuli achukue tena fomu, si angesubiri kuchukua fomu ya kugombea urais kutoka kwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi?
Logic hawana,mgombeaji ni Mwenyekiti ambae ni Raisi ndie mtetezi huyo huyo wa kiti cha uraisi , angepitishwa bila drama kwa kuwa CCM hairuhusu kumshindanisha sitting president na mtia nia yeyote.

Kwa hiyo hakuna sababu za msingi kupitia mchakato wa kugombea uraisi kwa tiketi ya CCM kwa sababu HAKUNA WAGOMBEA.

Kwa hiyo uteuzi wa Raisi Magufuli hauitaji kupitia CC,NEC na mkutano mkuu kwa kuwa hakuna jambo la kujadiri wala kupigia kura. Wangewahurumia wananchi kutumia pesa za kutia nia iende mfuko wa afya.

Lakini kama bado wanadai utaratibu wa CC,NEC,NC.kuwa una muhimu kwa Raisi Magufuli ,utakuwa ni batili kwa kuwa endapo mkutano mkuu ungetilia shaka uwezo wa Raisi Magufuli itabidi watia nia wapya wachukue form na kusaka wadhamini nchi nzima katika week mbili,harafu ipitie CC,NEC na mkutano mkuu NC.

Utaratibu wa one man show wa CCM ni kizingiti endapo yule mtetezi akikumbwa na matatizo hawana second runner.
 
Hata kama kazi imemshinda analia lia kila siku kazi ngumu, kazi ina MATESO makubwa, halali na amechoka ATASUKUMIZWA hivyo hivyo ili aendelee KUIVURUGA Nchi.



downloadfile-360.jpg


Aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli.

“Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana CCM, Rais anatakiwa awe katika vipi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?,” amesema Bulembo


Bulembo amesema hataki kugombea licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe wabunge.

“Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa wabunge haileti picha nzuri,” amesema Bulembo.
 
Mkuu, hebu muwe mnatumia akili hata kidogo na kuacha propaganda na utapeli wa wazi. Hivi Membe anachukuaje fomu huko CCM ikiwa alifukuzwa uanachama na sasa si mwanachama wa CCM?

Petro na ww umeanza kuwa mzee nini. Ana zaidi ya wiki 2 sasa akisema alifukuzwa lakini hakupewa barua ya kufukuzwa. Unakwama wapi dogo?
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] wakikujibu ni tag!
He! tena kwa hiyo mnaogopa nini wakati Mkuu anapendwa na wanaccm, ruhusuni watu wachukue form ili awaonyeshe kwamba ana pendwa kwa kuwagalagaza kabla hajakutana na upepo wa nje, hii pia inasaidia kumuongezea hamasa kuelekea uchaguzi mnao shauri hii mnampoteza sana Mgombea wenu
 
Back
Top Bottom