Bunda: Auawa na mkewe kwa kuchomwa kisu, kung'atwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo sehemu za siri pamoja na ulimi

Bunda: Auawa na mkewe kwa kuchomwa kisu, kung'atwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo sehemu za siri pamoja na ulimi

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Ofisa Kilimo katika kata ya Neruma wilaya ya Bunda mkoani Mara anayefahamika kwa jina la Julius Rubambi ameuawa kwa kuchomwa kisu na kung'atwa ulimi na mkewe kutokana na wivu wa kimapenzi huku mkewe Elizabeth Stephen akijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Kibara.

Inasadikika kuwa chanzo cha ugomvi huo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa ameanzisha mahusiano mengine nje ya ndoa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mara ACP Salim Morcas na amesema tayari mwanamke huyo anashikiliwa na Jeshi hilo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Mapenzi.png
 
Ofisa Kilimo katika kata ya Neruma wilaya ya Bunda mkoani Mara anayefahamika kwa jina la Julius Rubambi (38) ameuawa kwa kuchomwa kisu na kung'atwa ulimi na mkewe kutokana na wivu wa kimapenzi huku mkewe Elizabeth Stephen (36) akijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Kibara
Mhh! Okay, kuna viwango vya hasira. Lakini kweli hivii? Nawazaga sipati majibu 🙌
 
Biblia inasema, "uovu wa mwanamke unaonekana kwenye sura yake"

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Ukweli ukiitizama sura ya mwanamke inajieleza lakini huyo bwana mdogo alikuwa so innocent hata kwa kuonekana tu.

Mungu amrehemu lakini tuliobaki tunasonga mbele ndoa bado zitakuwepo tu hiyo ni ajali kama zilivyo ajali nyingine au kama leo tulipotoka makwetu asubuhi kwenda kutafuta ridhiki hadi muda huu giza linaingia kuna ambao hatukupata kitu na kuna ambao wamepata so yote ni matokeo mwenye mke ameuawa na mkewe na yupo mwengine anatengewa maji na mkewe akaoge muda huu.
 
Ukweli ukiitizama sura ya mwanamke inajieleza lakini huyo bwana mdogo alikuwa so innocent hata kwa kuonekana tu.

Mungu amrehemu.
Kweli kabisa kaka hapo alikuwa nice man. Sasa wanawake huwa wanajuaga kimbilio la wakosefu. RIP kaka, bora ungeishi na simba kuliko mwanamke mwovu.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Tunatofautiana akili kwa kweli hivi kitu cha kuingia ukakojoa ukaendelea na mishe zako zinatoa mtu roho! Hivi kuna watu wapo serious na mpz kiasi hiki?

Jitu hujazaliwa nalo mumekutana ukubwani umelioa au kukuoa hujalikuta bikira unalikuta lilishatumika hadi basi kulifanyia wivu hadi kukutoa roho inatoka wapi?
 
Ofisa Kilimo katika kata ya Neruma wilaya ya Bunda mkoani Mara anayefahamika kwa jina la Julius Rubambi (38) ameuawa kwa kuchomwa kisu na kung'atwa ulimi na mkewe kutokana na wivu wa kimapenzi huku mkewe Elizabeth Stephen (36) akijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Kibara.

Inasadikika kuwa chanzo cha ugomvi huo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa ameanzisha mahusiano mengine nje ya ndoa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mara ACP Salim Morcas na amesema tayari mwanamke huyo anashikiliwa na Jeshi hilo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

View attachment 2951950
kikulacho kinguoni mwako
 
Ofisa kilimo katika kata ya Neruma wilayani Bunda Mkoani mara anadaiwa kufariki dunia baada ya kuchomwa kisu na mke wake katika ugomvi uliohusishwa na wivu wa mapenzi.

Ofisa Kilimo wa Kata ya Neruma wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Julius Rubambi (38) amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa na kisu na mke wake baada ya kutokea ugomvi baina yao.

Akizungumza kwanjia ya Simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne Aprili 2,2024 katika eneo la Kibara wilayani Bunda majira ya saa 4 asubuhi.

Kamanda Morcase amemtaja mtuhukiwa wa mauaji hayo kuwa ni Elizabeth Steven ( 30) ambaye tayari anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.

"Ni kweli tukio lipo,mke wa marehemu naye amejeruhiwa na tunavyoongea amelazwa katika hospitali ya Kibara huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwaajili ya taratibu zingine," amesema

Amesema taarifa za awali zinadai wanandoa hao walikuwa na ugomvi ambapo mume alimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano nje ya ndoa hali iliyoplekea kuwepo na majibizano kisha kuibuka kwa ugomvi.

Amefafanua kuwa kufuatia ugomvi huo mke huyo alimchoma kisu mume wake kifuani ndipo mume naye alipompiga na kupelekea mke kupoteza fahamu kabla ya wote kukimbizwa hospitalini kwaajili ya matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema,marehemu mbali na kuchomwa na kisu lakini pia amekutwa na majeraha ya kung'atwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Kibara.

"Amejeruhiwa sehemu mbakimbali hadi sehemu za siri na taarifa zinasema ugomvi wao ulianza tangu usiku wa kuamkia leo ila hadi sasa bado sijajua chanzo cha ugomvi ni nini," amesema Dk Naano

Amesema baada ya kufikishwa hospitalini hapo hali ya ofisa kilimo huyo ilionekana kuwa mbaya hivyo uongozi wa hospitali ukiwa unafanya maandalizi ya rufaa kwaajili ya kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando kwaajili ya matibabu zaidi ofisa kilimo huyo alifariki dunia.
 
Back
Top Bottom