Unique Flower
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 12,838
- 25,282
Hapana kama wolper ready to fight huyo ni mchaggaAmekaa kaa kama kajala
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana kama wolper ready to fight huyo ni mchaggaAmekaa kaa kama kajala
My wangu....mambo?ila watu wa kanda ya ziwa kwa matukio mwee
Ooh Nifah is sad and am sad too 😭😭Ofisa kilimo katika kata ya Neruma wilayani Bunda Mkoani mara anadaiwa kufariki dunia baada ya kuchomwa kisu na mke wake katika ugomvi uliohusishwa na wivu wa mapenzi.
Ofisa Kilimo wa Kata ya Neruma wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Julius Rubambi (38) amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa na kisu na mke wake baada ya kutokea ugomvi baina yao.
Akizungumza kwanjia ya Simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne Aprili 2,2024 katika eneo la Kibara wilayani Bunda majira ya saa 4 asubuhi.
Kamanda Morcase amemtaja mtuhukiwa wa mauaji hayo kuwa ni Elizabeth Steven ( 30) ambaye tayari anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.
"Ni kweli tukio lipo,mke wa marehemu naye amejeruhiwa na tunavyoongea amelazwa katika hospitali ya Kibara huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwaajili ya taratibu zingine," amesema
Amesea taarifa za awali zinadai wanandoa hao walikuwa na ugomvi ambapo mume alimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano nje ya ndoa hali iliyoplekea kuwepo na majibizano kisha kuibuka kwa ugomvi.
Amefafanua kuwa kufuatia ugomvi huo mke huyo alimchoma kisu mume wake kifuani ndipo mume naye alipompiga na kupelekea mke kupoteza fahamu kabla ya wote kukimbizwa hospitalini kwaajili ya matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema,marehemu mbali na kuchomwa na kisu lakini pia amekutwa na majeraha ya kung'atwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Kibara.
"Amejeruhiwa sehemu mbakimbali hadi sehemu za siri na taarifa zinasema ugomvi wao ulianza tangu usiku wa kuamkia leo ila hadi sasa bado sijajua chanzo cha ugomvi ni nini," amesema Dk Naano
Amesema baada ya kufikishwa hospitalini hapo hali ya ofisa kilimo huyo ilionekana kuwa mbaya hivyo uongozi wa hospitali ukiwa unafanya maandalizi ya rufaa kwaajili ya kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando kwaajili ya matibabu zaidi ofisa kilimo huyo alifariki dunia.
Mimi sijui Kama Kuna MWANAMKE wa kunipigaa najarib kuwazaMwanamke mwenyewe anaoneka ni mbavu kama Body Guard wa Diamond