Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Najua hivi huwezi fanyaMtihani Sana.
Kamwe siwezi.Najua hivi huwezi fanya
Mwinyi dead wives aliveMungu asimame na hizo ndoa zenu,
Maana hali ni tete kwa upande huo mumshinde sheitwain ibilis
Dah so sad lo.
zote ni sahihi,
Umeongea kwa hisia sana.Tunatofautiana akili kwa kweli hivi kitu cha kuingia ukakojoa ukaendelea na mishe zako zinatoa mtu roho! Hivi kuna watu wapo serious na mpz kiasi hiki?
Jitu hujazaliwa nalo mumekutana ukubwani umelioa au kukuoa hujalikuta bikira unalikuta lilishatumika hadi basi kulifanyia wivu hadi kukutoa roho inatoka wapi?
YAKOBO 4:1,2, INASEMA; 1 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? 2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! 3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.Ofisa Kilimo katika kata ya Neruma wilaya ya Bunda mkoani Mara anayefahamika kwa jina la Julius Rubambi ameuawa kwa kuchomwa kisu na kung'atwa ulimi na mkewe kutokana na wivu wa kimapenzi huku mkewe Elizabeth Stephen akijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Kibara.
Inasadikika kuwa chanzo cha ugomvi huo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa ameanzisha mahusiano mengine nje ya ndoa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mara ACP Salim Morcas na amesema tayari mwanamke huyo anashikiliwa na Jeshi hilo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
na kwa wasio wanasheria, nikiwadokeza tu, hii kesi hawezi kunyongwa, ni manslaughter kwasababu kifo kimetokea wakati wa ugomvi, malice aforethought inaweza kuwa ya kutafuta. soon dada atakuwa mtaani, na ataolewa tena. ila mwenzake ndo kafa, na siajabu kafa katika dhambi. ndo maana tunasema okokeni, shetani yupo ili kuangamiza maisha ya wanadamu kabla hawajarudi kwa Mungu. shetani hua anagombanisha wanadoa,wanapigana, wanachinjana yeye kakaa pembeni, ikiwezekana wote wauane ili wote waende motoni. kuweni makini, kuishi nje ya Mungu hakuna mwisho mwema.Ofisa kilimo katika kata ya Neruma wilayani Bunda Mkoani mara anadaiwa kufariki dunia baada ya kuchomwa kisu na mke wake katika ugomvi uliohusishwa na wivu wa mapenzi.
Ofisa Kilimo wa Kata ya Neruma wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Julius Rubambi (38) amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa na kisu na mke wake baada ya kutokea ugomvi baina yao.
Akizungumza kwanjia ya Simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne Aprili 2,2024 katika eneo la Kibara wilayani Bunda majira ya saa 4 asubuhi.
Kamanda Morcase amemtaja mtuhukiwa wa mauaji hayo kuwa ni Elizabeth Steven ( 30) ambaye tayari anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.
"Ni kweli tukio lipo,mke wa marehemu naye amejeruhiwa na tunavyoongea amelazwa katika hospitali ya Kibara huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwaajili ya taratibu zingine," amesema
Amesea taarifa za awali zinadai wanandoa hao walikuwa na ugomvi ambapo mume alimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano nje ya ndoa hali iliyoplekea kuwepo na majibizano kisha kuibuka kwa ugomvi.
Amefafanua kuwa kufuatia ugomvi huo mke huyo alimchoma kisu mume wake kifuani ndipo mume naye alipompiga na kupelekea mke kupoteza fahamu kabla ya wote kukimbizwa hospitalini kwaajili ya matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema,marehemu mbali na kuchomwa na kisu lakini pia amekutwa na majeraha ya kung'atwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Kibara.
"Amejeruhiwa sehemu mbakimbali hadi sehemu za siri na taarifa zinasema ugomvi wao ulianza tangu usiku wa kuamkia leo ila hadi sasa bado sijajua chanzo cha ugomvi ni nini," amesema Dk Naano
Amesema baada ya kufikishwa hospitalini hapo hali ya ofisa kilimo huyo ilionekana kuwa mbaya hivyo uongozi wa hospitali ukiwa unafanya maandalizi ya rufaa kwaajili ya kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando kwaajili ya matibabu zaidi ofisa kilimo huyo alifariki dunia.