Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah unaodaiwa kukutwa mtoni ukiwa umefungwa kwenye mfuko.



Mwili wa Mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa katika mto Ndabaka eneo la Bunda /Lamadi

Taarifa kutoka vyanzo vya habari zinasema kwamba mwili wa Samson Josiah umeokotwa na wavuvi wa samaki leo jioni Jumatano Machi 14,2018.

Watu wa karibu na marehemu wanasema mwili uliookotwa ni wa Samson Josiah.

Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa. Soma => TANZIA: Mmiliki wa mabasi ya Super Sami akutwa amekufa na gari lake kuchomwa moto Serengeti

Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa hajapatikana.

Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.

Chanzo: Muafrika Halisi blog
Hakuwa kweli anawinda wale wanyama wanalindwa na Ak47
 
Inahitaji upelelzi gani hapo mkuu?
Style yao ya mauaji ni ileile , namini huko kanda ya ziwa kutakuwa n amauaji mengi sana yakiendelea kimyakimya.
Kama mtindo wa uhalifu huu unafanana na matukio mengine mbona hatujaokota magari yaliyochomwa moto sawa na idadi ya viroba vya maiti vilivyookotwa?

Huoni hapo kuna jambo tofauti kabisa na mengine?
 
Toka kupotea kwake mpka kukutwa gari lake limechomwa moto wasiojulikana hawajawahi kusema lolote,hii awamu ndio wahusika na kiongozi wao hajawahi kusema lolote toka haya mauaji yameanza.
Mlimchagua wenyewe n kumsifia n kiongozi mwema kuwahi kutokea.kumbe ni kiongozi mwenye mikono iliyojaa rangi nyekundu,roho mbaya,visasi,kujifanya yeye ndio anaakili kuliko mtz yeyote
Sioni sababu ya kuigizwa magufuri na mauaji haya mbona kumtesa mtu ni kitu kidogo sana ona wakina rugemalila na karasinga refer wakina babu saya na yule billione mdogo wa kule arusha alopigwa lisasi kipindi cha jk aliuwawa na jpm unajua unamjua vzr marehem anaingiaje kwenye siasa wew upo kimbiji huko umejuaje mambo ya hukoo nyie ndo mnatupandikiza imani mbaya tena wew naomba ukamatwe uhojiwe wote tuna hali ngumu lakin hasira zako usiziamishie kwenye msiba ya watu kila mmoja anacycle yake ya maisha unajua siri za matajir wew
 
Eee Mwenyezimungu tunusuru na hili balaa. Poleni sana familia ya mfiwa
 
Ata waalifu na wenyewe wamejificha kwenye kivuli cha siasa majambazi na wenyewe watafanya hayo na kujificha kwenye kivuli cha siasa
 
Fanya busara kidogo kwa kuigiza kama nawewe ni mtu timamu.

Unaharibu upepelezi kwa kuingiza siasa. Au wewe ndio muhusika hapa unafanya hivi kuwapotosha wapelelezi?
....Acha porojo wewee, eti unaharibu upelelezi haya mambo yameanza leo?
 
RIP Sam, familia poleni sana, Mola awape wepesi ktk msiba huu mzito. Mungu ndie anajua kila kitu ILA hakuna aliyemwaga damu ya binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe halafu akawa salama.
 
Hilo boga juu ya shingo linachosha miguu yako kwan watu wametupiwa mtoni leo nani kakwambia magufuli ni msemaji wa serikali pumbuv wew umekaa hapo na kwapa zako nyeusi kushadadia ujinga akwelina anaingiaje hapa
Mbona ukali? hebu jibu mambo kwa hekima hata za kukopa kama hukujaaliwa hikma.
 
Mkuu umeeleza vyema,wameshindwa kufanya siasa wamebakia kutafuta huruma kutoka kwa wananchi.Hawatafika mbali kwa sababu siasa zimewashinda
acha uchochezi we hujui kwamba kufanya siasa kumezuiliwa hadi 2020? sasa wanafanyaje hizo siasa wakati hata mikutano ya jimboni inawekewa figisu,, Pole pole peke yake ndio karuhusiwa maaana hata Kinana kapigwa stop
 
MWIII GULU alisema hajawahi kusikia watanzania wakilia na kuweka misiba kwa maiti zinazookotwa ufukweni kila kukicha. Kilio chake bila shaka kimepata majibu.
Yule muandishi wa Mwananchi waliyemua ndio angewaumbua kwani alikuwa na orodha ya watu zaidi ya 100 waliopotea Kibiti..Ndugu wanatoa taarifa polisi nao wanatishiwa maisha..
 
Back
Top Bottom