Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Alienda kudai deni,alienda kumdai nani ?
aliondoka na ndugu zake,ndugu kivipi na wenye mahusiano gani ?
atarudi na mgeni,mgeni gani ?
alikuwa anadai nini ?
R.I.P
 
Hili li nchi sijui likoje yani ningekuwa na uwezo wa kuweza hata kupiga sniper ningewatafuta hao watu wasiojulika kwa namna yoyote ile ili nife na koromeo la mtu ***** zake tunakufa kama mbu kwa sasa na hakuna hata mtu mmoja aliedandiwa hii inamanisha nini. Au ni sawa na ule msemo unaosema kesi ya mwizi kumpelekea Jambazi kinuke tu kama vipi jamani
 
Dah sema hatuwezi jua... Matajiri wa kanda ya ziwa wanamambo yao bana
Tuseme tu RIP
 
Tuanzie kudadisi mawasiliano yake ya simu na huyo mdaiwa na pia katika biashara kuna michezo mibovu. Yaani inabidi simu zake line zichunguzwe kwa kina na zile za ndugu zake wa karibu pia. Nina imani mitandao ya simu ikikaa vyema inaweza kabisa kupata namba za simu zilizotumika eneo gari lilikutwa na msafara za kwenda kutupa maiti hiyo. Ila kwa kweli Tanzania sijajua ile amani tuliyoikuta tunazaliwa imekwenda wapi. Ukweli ndiyo maana tunapata alama za mkia kwa matendo ya furaha Tanzania kwa kuwa kila siku mambo na matukio ya kuhuzunisha yamejaa tu. Sisi tuliolelewa kwa imani za dini na kuzishika huwa inatupa shida sana. Ila tunaamini tukisimama katika maombi tunaweza kurejesha tena nchi hii katika amani. Haya yanayotokea leo tulikuwa tunayasikia huko Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya ila si Tanzania kwa hakika.
 
we nae haueleweki sasa..inamaana maombi yako hauyaamini au mungu uliemuomba hapo hawezi kukujibu mpaka umeanza na kushtaki kwa JPM aingiie kati? hahaha kuwa na msimamo basi.
[emoji23] [emoji23] [emoji125]
 
Rais na taasisi yake baada wakemee mauaji kama aya wako busy kumjibu Mange kimambi kwenye Instagram shame wako busy kujibu sijui maandamano
 
Ccta mie naogopa sana lifestyle iliyopo sasa Tanzania. Hebu angalia ujasiri walionao hao wauaji!! Najiuliza je inamaana tangu wazaliwe hawajawahia kufundishwa uwepo wa mungu!? Nimechoka kabisa heri kufa kwa Ukimwi lkn si kwa style hii. Nchi imelaaniwa
Yaani acha tu,watu wamekosa utu.Walimpigia simu akawaamini kwa vile ni Binadamu wenzake.Kumbe wanakwenda kumchinja.Usimwamini mtu yeyote.
 
RIP Samson. Naambiwa marehemu ni kati ya watu waliochangia vizuri matibabu ya TL. Aliyemchangia yu hai, yeye ametangulia. Mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake yalipie pale ambapo hakutimilika, na Mungu mwenye huruma aiweke mahali pema peponi.
 
PICHA YA KUTISHA.jpg


MAGE.jpg


Mwili wa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Super Sami(Josiah) umekutwa katika mto serengeti ukiwa unaelea juu ya maji pia kafungwa na mawe makubwa ....wananchi wakiwa katika pilikapilika zao za uvuvi walibahatika kuona mwili huo ukielea juu ya maji
Rest in peace josiah!
chanzo.

Tunangojea Majibu toka Kwa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya ndani Mr Mwigulu nchemba.
Tanzania yangu amani imekuwa ni ya mdomo mtupu sio vitendo. Tunako kwenda ni karibu kuliko tunako toka Mungu iokoe Tanzania yangu amin.
 
Back
Top Bottom