Bunge kuihoji Bodi ya Mikopo sakata la upendeleo utoaji wa Mikopo

Bunge kuihoji Bodi ya Mikopo sakata la upendeleo utoaji wa Mikopo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Spika Dkt. Tulia Ackson ameitaka Bodi ya Mikopo (HESLB) kufika Bungeni kujibu tuhuma za kugomea Uchunguzi wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda.

Prof. Mkenda ameituhumu HESLB kukataa kutoa ushirikiano na taarifa kwa Kamati yake kuhusu uwepo wa upendeleo wa utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itaihoji Bodi ya Mikopo Ijumaa Novemba 4, 2022 Bungeni jijini Dodoma.
 
Ifutwe tu

Yaani Bodi inagoma kuchunguzwa?!!

Enzi za Shujaa ingeshafutiliwa mbali
hii bodi inanyanyasa sana watoto wetu (watoto wa maskini).wanawagawia mikopo watoto wa wenye uwezo tu.pia ina tabia ya kuwabambikiza madeni watoto wa maskini ilhali ikijua fika deni halisi la wanalodaiwa.ni bodi ya kinyonyaji na kibeberu.
 
Ifutwe tu

Yaani Bodi inagoma kuchunguzwa?!!

Enzi za Shujaa ingeshafutiliwa mbali
Hiyo bodi ina nguvu kiasi gani, si inafutwa tu kirahisi na kuteua nyingine na ku review malalamiko ya wanufaika wa mikopo. Mambo mengine tusipofanya maamzi magumu hatutapifa hatua linapokuja swala la manufaa ya umma. Sote ni sehemu ya umma
 
Yaani wabunge nyie mtutumie "vimemo" vya kuwapa upendeleo ndugu zenu na woto wa nyumba ndogo zenu alafu nyie hao hao mtuhoji? Pumbavu!
 
Bodi ya mkopo wana mambo ya ajabu sana, unaweza kuta mtoto kapewa boom tu halafu mwingine mwenye uwezo kapewa ada, Boom, book and stationary, special facat, field na research sasa unashindwa kuelewa wanatumia kigezo gani
 
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameitaka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), kufika katika Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Ijumaa Novemba 4, 2022, ili kujieleza kwanini hawataki kusikiliza maelekezo ya Serikali.

Dodoma. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameitaka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), kufika katika Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Ijumaa Novemba 4, 2022, ili kujieleza kwanini hawataki kusikiliza maelekezo ya Serikali.

Agizo hilo limefuatia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda na baadhi ya wabunge kulalamikia kuwa kamati aliyoiunda na (Profesa Mkenda), kuchunguza utoaji wa mikopo ya elimu ya juu imeshindwa kupata ushirikiano.

Dk Tulia ametoa uamuzi huo baada ya Bunge kujadili hoja ya uwepo wa wanafunzi wenye vigezo kukosa mikopo ya elimu ya juu, hoja iliyotolewa na Mbunge wa Biharamulo (CCM), Ezra Chiwelesa

“Naamini kwamba Waziri hawakusikilizi kwenye mambo mengine lakini kwenye hili watakusikiliza wao wataitwa katika Kamati yetu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii…Siku ya Ijumaa saa 7.00 wajikute kwenye hiyo kamati,”amesema.

Tutatoa fursa tujue kama ni kiburi ama kitu kingine tofauti kwa ngazi hii. Kwa maana ya kuichunguza kama inatoa mikopo sawa sawa sio hoja wanazoitiwa ndani ya kamati, sasa hivi tunataka kuelewa kama Bunge kwa nini hiyo bodi haisikilizi hayo maelekezo,”amesema.

Amesema kuhusu hoja kama HESLB inatoa mikopo sawa sawa itajadiliwa Februari mwakani wakati kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itakapokuwa inatoa taarifa yake bungeni na hivyo kuona kama kuna haja ya Bunge kuunda tume ya kuchunguza bodi hiyo ama la.

Amesema wabunge watapewa
 
Wanachofanya baada ya waziri kucharuka Sasa ni hivi,vyuo vyenye majina wanawapa mkopo asilimia 100% wale continuous na wakati mwaka Jana waliwap Maskini 49%😅 ,Sasa vyuo vilivyobak hawajapewa hata kidogo wanarefusha kalenda et tar 4
 
Prof ameyakoroga baada ya kutaka kumpachika CEO mchaga kwa nguvu, watendaji wenzake ndani ya wizara wamgeuka, huko Bodi ya mikipo ya elimu ya juu hapakaliki, yeye mwenyewe akili hali kuwa mbaya.

Na uhenda akapanguliwa muda si mrefu.View attachment 2404163
Screenshot_20221101-170750_1.jpg
 
Spika Dkt. Tulia Ackson ameitaka Bodi ya Mikopo (HESLB) kufika Bungeni kujibu tuhuma za kugomea Uchunguzi wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Elimu Prof. Profesa Adolf Mkenda.

Pro. Mkenda ameituhumu HESLB kukataa kutoa ushirikiano na taarifa kwa Kamati yake kuhusu uwepo wa upendeleo wa utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itaihoji Bodi ya Mikopo Ijumaa Novemba 4, 2022 Bungeni jijini Dodoma.
Yaani Bodi inagomea Kamati ya Waziri? Is it seriously?
 
Wanufaika wa mkopo wamepunguzwa kutoka 70k mwaka 2021/2022 na kufika 42k 2022

Kuna baadhi ya cluster 2 na three wananyimwa mkopo huku wanaosoma Art wanaopewa priority ni degree ya Kiswahili
Tu

So ao continuous wanapata nyongeza huku first year wengi wakitoka 0-0

Kiufupi hii hatari
 
Hili "bunge" ambalo kimsingi ni kamati ya ccm linatafuta attention baada ya kuona watanzania wamewapuuza sana.
 
Back
Top Bottom