Bunge kuihoji Bodi ya Mikopo sakata la upendeleo utoaji wa Mikopo

Bunge kuihoji Bodi ya Mikopo sakata la upendeleo utoaji wa Mikopo

Bodi ya mkopo wana mambo ya ajabu sana, unaweza kuta mtoto kapewa boom tu halafu mwingine mwenye uwezo kapewa ada, Boom, book and stationary, special facat, field na research sasa unashindwa kuelewa wanatumia kigezo gani
Labda ungeainisha ni vigezo vipi vitumike katika kutoa mikopo,ili malalamiko kama hayo yasiwepo.
 
Hapa suala siyo vigezo bali kuna ubaguzi na upendeleo katika kutoa mikopo!
Sina hakika na hizo tuhuma zako, nachokiona mimi, ufanisi wa bodi hauwezi kuwa wa kuridhisha kwa fungu wanalopewa kwa ajili ya kukopesha.
 
Awamu ya watu unanijua Mimi nani imerudi.wamepata nguvu ya kukataa kuhojiwa sababu ni awamu legelege
acha kuweweseka wewe
awamu iliyopita ndiyo iliyolazimisha bodi ya mikopo kuongeza makato ya mikopo kutoka 8%-15% unajua madhara watu waliyo yapata kutokana na hilo?
watumishi walikaa 6 years bila nyongeza ya mishahara wala madaraja kinyume na sheria unakumbuka?
 
Sina hakika na hizo tuhuma zako, nachokiona mimi, ufanisi wa bodi hauwezi kuwa wa kuridhisha kwa fungu wanalopewa kwa ajili ya kukopesha.
Sasa kumbe una majibu yako! Yaweke hadharani yajadiliwe.
 
Sasa kumbe una majibu yako! Yaweke hadharani yajadiliwe.
Sina majibu yangu, nazungumzia ufanisi na uhalisia. Nyingine ni porojo tu.

Azimio lipite, wanafunzi wote wapate mikopo, bodi wapate fungu kukidhi watu waombaji wote.

Katika Act inayoongoza shughuli za board hakuna msamiati "needy student", msamiati uliopo ni "eligible students"

Hii hali kwa mfano, ya kutoa fungu la kukopesha wanafunzi 30,000 huku waonbaji wakiwa 50,000 lazima ilete malalamiko.
 
Nadhani definitions za needy na eligible ndizo zinazotumika na Bodi ya mikopo kufanya ubaguzi na upendeleo vinginevyo kusingekuwa na matatizo yaliyopo.
 
Spika wa bunge na viongozi wengine fahamuni kuwa kidonda ukikilea kinakuwa donda ndugu ........kwann mrivunja mkataba wa 8% na kutupeleka 15% ? Bila kutushirikisha ? Kama ingekuwa hivi basi hata benki mzishinikize kupunguza riba kwa vile wamepunguza kwa wakopaji wapya ilii iwe Sawa na aliyekopa kipindi iko 20%+ .
 
Mzizi wa tatizo hapo ni ufinyu wa bajeti.
Sasa tujiulize swali la msingi ni nani anaepitisha bajeti hiyo..?
Then ukisha mfahamu ndio utakapojua kwamba hawa wapuuzi wanatuoni sisi mabayo
 
Spika Dkt. Tulia Ackson ameitaka Bodi ya Mikopo (HESLB) kufika Bungeni kujibu tuhuma za kugomea Uchunguzi wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda.

Prof. Mkenda ameituhumu HESLB kukataa kutoa ushirikiano na taarifa kwa Kamati yake kuhusu uwepo wa upendeleo wa utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itaihoji Bodi ya Mikopo Ijumaa Novemba 4, 2022 Bungeni jijini Dodoma.
Tetesi: - Afisa Elimu Sekondari Moshi Manispaa amuweka lokapu Mwalimu wa idara ya Elimu Msingi kisa Mwalimu kuuliza barua ya kazi maalum haina siku maalum
 
Back
Top Bottom