Tetesi: Bunge Kuwaka Moto hadi Zanzibar ijadiliwe kwa Dharula

Tetesi: Bunge Kuwaka Moto hadi Zanzibar ijadiliwe kwa Dharula

Bunge linataka kufanya kazi za ZEC?
Kwani jambo linapojadiliwa kwa dharula, kunakuwa hakuna chombo maalumu kinachopaswa kushughurika na jambo hilo..?? JARIBU KUKUMBUKA YOTE YALIYOWAHI KUJADILIWA KWA DHARULA
 
Sisi watanganyika tuna shida ya barabara, maji, umeme, huduma bora za afya na elimu, masoko ya uhakika, mbinu bora za kilimo na kuongeza tija, ajira kwa vijana na mambo meengi, wabunge tumewaagiza mkatutekelezee haya.....

Miaka mitano sio mingi.....shauri yenu
Unless uniambie wewe si mtanzania, mtanzania( wa bara na visiwani) hawezi kuongea amani kama sehemu yoyote kati ya bara au visiwani hakuna amani.
Suala la Zanzibar ni letu sote na ndio maana wanamhusisha raisi wa JMT, hata wabunge kama kweli watalijadiri,Mungu awasaidie wapate ufahamu wa nini wakijadiri,wakiongozwa na mihemko ya kiitikadi na ushabiki hakutakuwa na umhimu wa kuliweka bungeni.
Busara zaidi zinatakiwa katika suala hili zaidi ya ushabiki.
 
Wadau habari nilizopata kutoka Dodoma hivi punde ni kuwa siku ya Jumanne Bungeni Dodoma moto utawaka kwani kuna hoja itatolewa ya kujadili suala la Zanzibar kama suala la dharura na kuwa shughuli zingine zisiendelee mpaka hilo lipatiwe ufumbuzi kwanza. Hoja hiyo pamoja na kutoka upinzani lakini habari ni kuwa wapo wabunge wengi wa ccm wanaiunga mkono bila kujali mikakati waliyopewa kikao cha Kinana majuzi.
Wabunge hawataki uvunjifu wa amani utokee ndio eti hatua zichukuliwe, kwani kimya cha watu visiwani sio kuwa hali ni shwari.
Nimeileta kama nilivyoisikia kutoka reliable source

Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano.Bunge la muungano kulijadili hilo Swala ni kuvunja katiba ya nchi
 
Bilashaka Utakua ni Uzinduzi bora wa Bunge ndani ya mwaka 2016..

1.Mategemeo kama hiyo hoja itaruhusiwa kujadiliwa ni
1.1/Lugha kali za kuudhi
1.2/Matusi na Kejeli..
1.3/Miongozo bila kikomo
1.4/...........

Alafu mwisho wa yoooooooooote muafaka upatikane bila kupepesa macho.
 
kwani
Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano.Bunge la muungano kulijadili hilo Swala ni kuvunja katiba ya nchi

Kwani wawakilisi wao hua wanakuja kufanya nini kama halihusiki????? Vita ikitokea Zenji watasubiri majeshi ya muungano ndo yaende au ni hayahaya tuliyonayo ndo yatahusika????????????? na bunge lako la muungano linakaa lini?? au mpaka Wazenji waseme sasa basi????????????????????????????? Hebu fikiri kwa upana zaidi mkuu
 
Huu ni mkwamo...Ulioletwa na Kungang'ania madaraka kwa CCM.....Bunge ni sehemu ya kuihoji serikali ....Hivyo Bunge lina wajibu wa kupata majibu wanapoyahitaji na kuielekeza serikali nini cha kufanya

Pale bungeni kuna uwakilishi wa wananchi wote

Kweli mkuu huu ni wajibu wa bunge letu na si kama wanavyofikiria wasioelewa sana majukumu ya bungela jamhuri. Mi nawatakia kila la heri na mambo yaende sawa ili mwisho wa yote Zaznibar wapate muafaka bila kumwaga damu, nahisi kuna watu wanategemea sana damu kumwagika zenji!!! hasa unaposoma coments zao hadi roho inauma.
 
CCM wajanja sana. Watamwambia jecha atoe tangazo la tarehe ya uchaguzi kabla ya hiyo jumanne.
 
Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano.Bunge la muungano kulijadili hilo Swala ni kuvunja katiba ya nchi
Kinachojadiliwa sio kura ngapi kapata nani au nani ni mshindi. Bali amani ya eneo hilo na jee haki za kikatiba zilizingatiwa katika kufuta Uchaguzi?
Na jee Bunge hili ni sahihi kuitambua serikali ya Zanzibar ya sasa ambayo haina baraza la wawakilishi?
Hii sasa hivi ndio hasa SERIKALI YA MAPINDUZI maana yupo rais na mawaziri ambao hawakuchaguliwa na wananchi
 
Mnapopeleka majeshi nchi za watu, mna muungano nao..??
Mambo ya muungano tuliyokubaliana ni ulinzi na usalama.Kuna majeshi ya muungano Zanzibar na yale yasiyo ya muungano.Mfano kuna JKU,KMKM na vikosi vya usalama vya Zanzibar nk.Zazibar pia wana mkuu wa majeshi na polisi, wa nchi ya Zanzibar.Kikiinuka Zanzibar nmkuu wa Jeshi wa Zanzibar na majeshi yaliyo chini yake aweza kiinukisha baada ya kupewa amri na amiri jeshi wa Zanzibar kamanda Shein.Kama akiona ANAHITAJI MSAADA basi amiri jeshi mkuu wa zanzibar aweza kubaliana na mkuu wa Majeshi wa Zanzibar kuwa vikosi vya muungano viingile kumsaidia

Lakini kwenye Swala la uchaguzi wa Zanzibar hauhusu muungano wala bunge la muungano sababu ule ni wa nchi huru ya Zanzibar yenye raisi wake,katiba yake,baraza lake la wawakilishi,jaji mkuu wake na sheria zao ambazo ni tofauti na Tanzania bara mfano mwezi wa Ramadhani mwiko kula barabarani na hotel kuwa wazi na serikali husimamia hilo.

Bunge la muungano kujitosa kujadili mambo ya ndani ya nchi huru ya zanzibar ni uingiliaji na uvunjaji katiba
 
Back
Top Bottom