Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda kwa vile anaona KMKM na MAFUNZO wanachezza gwaride basi kwake hayo ni majeshi!YEHODAYA mbona huna akili kiasi hiki
Amiri mkuu wa Tanzania ni MMOJA TU ambaye ni Rais wa Jamhuri
Rais wa Zanzibar hana jeshi lolote isipokuwa KKKM...Ambalo sio jeshi bali kikosi cha kuzuia magendo
Ficha Upumbavu wako
Wadau habari nilizopata kutoka Dodoma hivi punde ni kuwa siku ya Jumanne Bungeni Dodoma moto utawaka kwani kuna hoja itatolewa ya kujadili suala la Zanzibar kama suala la dharura na kuwa shughuli zingine zisiendelee mpaka hilo lipatiwe ufumbuzi kwanza. Hoja hiyo pamoja na kutoka upinzani lakini habari ni kuwa wapo wabunge wengi wa ccm wanaiunga mkono bila kujali mikakati waliyopewa kikao cha Kinana majuzi.
Wabunge hawataki uvunjifu wa amani utokee ndio eti hatua zichukuliwe, kwani kimya cha watu visiwani sio kuwa hali ni shwari.
Nimeileta kama nilivyoisikia kutoka reliable source
Nikuulize swaliMambo ya muungano tuliyokubaliana ni ulinzi na usalama.Kuna majeshi ya muungano Zanzibar na yale yasiyo ya muungano.Mfano kuna JKU,KMKM na vikosi vya usalama vya Zanzibar nk.Zazibar pia wana mkuu wa majeshi na polisi, wa nchi ya Zanzibar.Kikiinuka Zanzibar nmkuu wa Jeshi wa Zanzibar na majeshi yaliyo chini yake aweza kiinukisha baada ya kupewa amri na amiri jeshi wa Zanzibar kamanda Shein.Kama akiona ANAHITAJI MSAADA basi amiri jeshi mkuu wa zanzibar aweza kubaliana na mkuu wa Majeshi wa Zanzibar kuwa vikosi vya muungano viingile kumsaidia
Lakini kwenye Swala la uchaguzi wa Zanzibar hauhusu muungano wala bunge la muungano sababu ule ni wa nchi huru ya Zanzibar yenye raisi wake,katiba yake,baraza lake la wawakilishi,jaji mkuu wake na sheria zao ambazo ni tofauti na Tanzania bara mfano mwezi wa Ramadhani mwiko kula barabarani na hotel kuwa wazi na serikali husimamia hilo.
Bunge la muungano kujitosa kujadili mambo ya ndani ya nchi huru ya zanzibar ni uingiliaji na uvunjaji katiba
Kuna haja gani ya sisi kujiita watanzania?Zanzibar wana majeshi yao na mkuu wa majeshi kama ambavyo wana jaji mkuu wa Zanzibar.Amiri jeshi wa Zanzibar ni Raisi wa Zanzibar.
Anayejua hali ya amani na Usalama ya zanzibar ni raisi wa Zanzibar na mkuu wa majeshi wa Zanzibar sio BUNGE la muungano au UKAWA
Kwani kujadili ndiyo kuchukua kazi ya Tume .............!!? Tume yenyewe imeshindwa mpaka leo kutueleza kinachoendelea ....... inaelekea Jecha bado yuko mafichoni!!Kwa hiyo bunge linaichukua hiyo kazi?
Sisi watanganyika tuna shida ya barabara, maji, umeme, huduma bora za afya na elimu, masoko ya uhakika, mbinu bora za kilimo na kuongeza tija, ajira kwa vijana na mambo meengi, wabunge tumewaagiza mkatutekelezee haya.....
Miaka mitano sio mingi.....shauri yenu
Bunge linataka kufanya kazi za ZEC?
Nikuulize swali
Inakuwaje siku ya matokeo ya uchaguzi jeshi la jamuhuri ya muungano kuvamia eneo la bwawani na kumchukua mwenyekiti wa uchaguzi akafute uchaguzi? Jee huioni ya kwamba mumeingilia na kuuvuruga uchaguzi ulio huru?
Nani alie ivuruga amani? Hutoweza kunipa majibu nikakuelewa
Wanataka tu kupoteza muda na fedha na kujipatia ujiko wa kisiasa,ukawa hawana tena ajenda ya ufisadi,wamehamia zanzibar.
Bunge la muungano halina mamlaka ya kumtangaza rais wa zanzibar wala kuamuru uchaguzi urudiwe.Ni ZEC tu mwenye mamlaka,tutazunguka wee mwisho tutarudi kwa jecha.
Hicho kikao kitakua kama cha harusi tu,maamuzi hayatakua na impact yoyote.
Maalim awaandae wafuasi tu kumpigia kura tena anaogopa nini kama hakuiba?
huna lolote .Aliyevuruga Uchaguzi ni Seif Hamad ALIYEJITANGAZA kuwa mshindi wa uraisi bila kutangazwa na tume na kabla ya matokeo kukamilika hivyo kuleta taharuki ya usalama hivyo kusababisha ulinzi uongezwe kila mahali ikwemo kwa mkurugenzi wa ZEC Kwa ajili ya usalama wake.Kujitangaza kule ilikuwa ni uhaini hivyo wanajeshi kuingia barabarani kulinda raia na mali zao baada ya mhaini Seif KUJITANGAZA ILIKUWA NI SAHIHI.
Na utakubaliana nami kuwa baada ya mhaini kujitangaza wanajeshi walikuwa maeneo yote ya Zanzibar si Bwawani tu.
Wabunge kutoka Zanzibar wanahudhuria bunge na walishaapishwa. Kilichobaki ni kile kinachohusu Zanzibar kama nchi. Maadam Tanzania ina serikali na mambo yanaenda hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na issue ya serikali ya Zanzibar. Unless useme kuna maslahi ya kisiasa kama ilivokuwa ule msiba wa mawazo. Kikatiba mnaweza kujadili na kila mbunge wa ukawa anapewa nafasi ya kuongea lakini kiuhalisia mtakuwa mnavunja katiba na kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar. Na chochote mtakachoamua hakina uhalali wa kutumika Zanzibar. Ingekuwa unaongelea issue ya Zanzibar kama Mkoa sawa na mtwara hapo ungeeleweka. Lakini ukiongelea Zanzibar kama nchi huna haki ya kujadili mambo yasiyo ya muungano kwenye bunge la muungano. Mind you this. Halafu hakuna alieapishwa kule wala hakuna aliepewa ushindi na wala hakuna alietangazwa mshindi na zaidi sana hakuna vurugu wala vita. Watu wanaongelea kuhusu kurudia uchaguzi au la. Sasa kufanya vurugu kwenye bunge la muungano ni kuhamasisha vurugu. Ni uchochezi. Ni ujinga na ni siasa za kipumbavu. Mbona wao wa zanzibar hawaongelei issue ya kafulila kudai kaibiwa ubunge wake. Mi naona siasa ni mchezo mbaya ambao lengo lake ni kunufaisha wachache. Ukawa wakifanya vurugu watatolewa bungeni na bunge litaendelea na miswada kibao itapitishwa. Yaan ikifika apo utaona kuwa hakukuwa na haja ya kuwapigia kura wabunge wa ukawa kama tulikuwa na uhakika kuwa lowasa hawezi kushinda Urais. Kuna tofauti kati ya mawazo ya watu na sheria inavosema. Ni hivi. Nchi huwa haziongozwi na mawazo tu ya watu. Watu wamelala na mahawala zao uko then tuamke asubuhi tusikie sheria imebadilika. Tunaongozwa na sheria na ili kubadilisha kuna taratibu zake. Wabunge wa ukawa wanatakiwa wawe makin katika hayo na mengine makubwa sio kufanya vurugu kwa sabb za kipuuzi ambazo hata kisheria hazikubaliki. Tutabaki nyuma mpaka lini. Inamaana hata matendo yetu tutatenda kwa kuwanufaisha akina lowasa. Hatuwawazii kabisa maskini wanaopata shida ya maji na Chakula wanakula mlo mmoja kwa sikuUpo sahihi kabisa. Lakini hali ya usalama ikiwa mbaya ndani ya sehemu ya muungano itakuwa vigumu kuyafanya yote hayo. Hebu ona ya kule Mtwara tuu kuhusu gas yalivyotusumbua! Na Zanzibar kuiacha bila kuijadili na kupata ufumbuzi ni sawa na kuwa na chui ndani ya nyumba ambaye yuko usingizini na kutegemea atalala daima.
Tusikubali nchi yetu sehemu moja ikageuka kama Somalia, ikifikia hapo hatuta weza kuidhibiti bila damu zetu kumwagika
Mhaini na bado yuko mtaani? Wadanganye watoto. Seif hakujitangaza mshindi kataja kura zake kulingana na fomu za mawakala zilizo sainiwa na anazo mkononi. Sasa Jecha hilo lingeweza kumzuia asitangaze zake?Aliyevuruga Uchaguzi ni Seif Hamad ALIYEJITANGAZA kuwa mshindi wa uraisi bila kutangazwa na tume na kabla ya matokeo kukamilika hivyo kuleta taharuki ya usalama hivyo kusababisha ulinzi uongezwe kila mahali ikwemo kwa mkurugenzi wa ZEC Kwa ajili ya usalama wake.Kujitangaza kule ilikuwa ni uhaini hivyo wanajeshi kuingia barabarani kulinda raia na mali zao baada ya mhaini Seif KUJITANGAZA ILIKUWA NI SAHIHI.
Na utakubaliana nami kuwa baada ya mhaini kujitangaza wanajeshi walikuwa maeneo yote ya Zanzibar si Bwawani tu.
Siwezi kukubaliana na wewe, ikiwa maalim kajitangaza mshindi kutokana na hati miliki zilizo tolewa kila kituo cha kupiga kura na kusainiwa na mawakala wa tume ya uchaguzi na kubandikwa katika vituo.Aliyevuruga Uchaguzi ni Seif Hamad ALIYEJITANGAZA kuwa mshindi wa uraisi bila kutangazwa na tume na kabla ya matokeo kukamilika hivyo kuleta taharuki ya usalama hivyo kusababisha ulinzi uongezwe kila mahali ikwemo kwa mkurugenzi wa ZEC Kwa ajili ya usalama wake.Kujitangaza kule ilikuwa ni uhaini hivyo wanajeshi kuingia barabarani kulinda raia na mali zao baada ya mhaini Seif KUJITANGAZA ILIKUWA NI SAHIHI.
Na utakubaliana nami kuwa baada ya mhaini kujitangaza wanajeshi walikuwa maeneo yote ya Zanzibar si Bwawani tu.
Kuna kitu hujijui kuhusu sheria ya uchaguzi.Kazi ya tume ni pamoja na kujumlisha matokeo.Huwezi kulala na hawara yako kitandani ukachukua matokeo toka vituoni na kuanza kujijumlishia na hawara yako halafu uende kutangaza kuwa kwa mujibu wangu na hawara yangu matokeo tuliyojumlisha ni haya! Tume itoe ya kwao ilinganishe na yale tulliyojumlisha kitandani na hawara yangu!!!!!! Tume ndie mjumlishaji pekee anayetambulika kisheria sio MHaini SEIF au mtu mwingine yeyote.Seif hakujitangaza mshindi kataja kura zake kulingana na fomu za mawakala zilizo sainiwa na anazo mkononi. Sasa Jecha hilo lingeweza kumzuia asitangaze zake?