Tetesi: Bunge Kuwaka Moto hadi Zanzibar ijadiliwe kwa Dharula

Tetesi: Bunge Kuwaka Moto hadi Zanzibar ijadiliwe kwa Dharula

Lazima ijadiliwe na Serikkali ya Magufuli isiruhusiwe kutoa fedha za kurudia uchaguzi.
Maana balozi safari za ikulu haziishi....fedha za kodi za bara zisitumike kabisa kwenda kuleta mifarakano...kama wanazo zao ccm unguja sawa wao hawana bunge kuna sultam shein
 
mgogoro wa zanzibar umesababishwa na ccm kutokubali kushindwa uchaguzi kule zanzibar. wabunge pia wajadili suala la bomoabomoa dar kama jambo la dharura.
 
Sisi watanganyika tuna shida ya barabara, maji, umeme, huduma bora za afya na elimu, masoko ya uhakika, mbinu bora za kilimo na kuongeza tija, ajira kwa vijana na mambo meengi, wabunge tumewaagiza mkatutekelezee haya.....

Miaka mitano sio mingi.....shauri yenu
Ka s.enge, tayari umeshasahau kwamba kazi ya mbunge si kuleta maendeleo bali ni kuwasemea wananchi ambao ni pamoja na wazanzibar.
 
Wadau habari nilizopata kutoka Dodoma hivi punde ni kuwa siku ya Jumanne Bungeni Dodoma moto utawaka kwani kuna hoja itatolewa ya kujadili suala la Zanzibar kama suala la dharura na kuwa shughuli zingine zisiendelee mpaka hilo lipatiwe ufumbuzi kwanza.

Hoja hiyo pamoja na kutoka upinzani lakini habari ni kuwa wapo wabunge wengi wa ccm wanaiunga mkono bila kujali mikakati waliyopewa kikao cha Kinana majuzi.

Wabunge hawataki uvunjifu wa amani utokee ndio eti hatua zichukuliwe, kwani kimya cha watu visiwani sio kuwa hali ni shwari.

Nimeileta kama nilivyoisikia kutoka reliable source

Usikonde kama ilivyokuwa katika kuchagua Meya Kndoni kura zitapigwa na kalamu za kamera zitatumika. Ila wakumbuke wazanzibar wako shwari wala ngendembwe hakuna sasa wakigeuza kichaka waambie watanzania wanataka kazi tu! Ya Wanzazibar watayaamua wazanzibar wenyewe.
 
Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano.Bunge la muungano kulijadili hilo Swala ni kuvunja katiba ya nchi

Mkuu yehoyada Kama usemavyo ni kweli kwa nini wale wabunge watano watokanao na baraza la wawakilishi hawapo? Maana bao ni sehemu ya wabunge WA Bunge la JMT. Usiongee mbele ya watu hivyo utachekwa Mkuu!
 
Ile mizinga 21 Aliyopigiwa na wanajeshi wa Zanzibar SHEIN wakati wa Sherehe za mapinduzi unafikiri alipigiwa kama nani?
Askari wa muungano walioko Zanziibar wako chini ya Magufuli.Lakini kuna vikosi vya Zanzibar kama nchi vilivyo chini ya Amiri jeshi Shein.Shein ana uwezo wa kumwagiza mkuu wa polisi zanzibar akamate wote wanaokula hadharani mwezi wa Ramadhani .hUKUMWONA mkuu wa majeshi wa Zanzibar Siku ya sherehe ya mapinduzi?

Yehoyada, Mkuu WA majeshi ya Zanzibar anaitwa nani?
 
Kama hoja hiyo ina ukweli nimejilidhisha tuna wabunge malofa, tunataka maindeleo jimboni kwetu hiyo ZEC ni sehemu ya muungano? Kwa katiba ipi watajadli? jMT ikiona kuna dalili za kutokuwepo amani INAPELEKA JESHI na Vifaru hilo ni la muungano
Hao wabunge wajiandae kupigika ukumbini vijana wa kazi wapo
 
Sisi watanganyika tuna shida ya barabara, maji, umeme, huduma bora za afya na elimu, masoko ya uhakika, mbinu bora za kilimo na kuongeza tija, ajira kwa vijana na mambo meengi, wabunge tumewaagiza mkatutekelezee haya.....

Miaka mitano sio mingi.....shauri yenu
kwahiyo kwa ushauri wako ni bora tubaki na tanganyika tusishughulike na maswala ya zenji
 
Kama hoja hiyo ina ukweli nimejilidhisha tuna wabunge malofa, tunataka maindeleo jimboni kwetu hiyo ZEC ni sehemu ya muungano? Kwa katiba ipi watajadli? jMT ikiona kuna dalili za kutokuwepo amani INAPELEKA JESHI na Vifaru hilo ni la muungano
Hao wabunge wajiandae kupigika ukumbini vijana wa kazi wapo
Umeambiwa Balozi Idd Seif kiguu na njia Ikulu kila siku anataka ile Pesa ya kwenda kujengea hospitality kwenu iende ikagharamie Uchaguzi uliofutwa na Jecha, kwa hiyo unataka Mbunge wako aseme NDIOOOO?
 
Nasema hivi,kwa hapa tulipo haturudi nyuma zanzibar yenye mamlaka kamili ni jambo la lazima.
 
ndipo hapo tunapoenda kupima uwezo wa wabunge wetu na wabunge wa magufuli.. dokta ataweza kusimamia show hii kweli au ndo itabaki business as usual
 
Sisi watanganyika tuna shida ya barabara, maji, umeme, huduma bora za afya na elimu, masoko ya uhakika, mbinu bora za kilimo na kuongeza tija, ajira kwa vijana na mambo meengi, wabunge tumewaagiza mkatutekelezee haya.....

Miaka mitano sio mingi.....shauri yenu

Ni kweli tumewatuma wabunge wetu waende bungeni wakatutetee kuhusu shida zetu za maji, barabara, zahanati etc lakini ikumbukwe kuwa Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya muungano na kama kule visiwani hakuna amani itakuwa vigumu sisi huku bara kupata hivyo tulivyowatuma wabunge kutuletea !!! Nadhani utanielewa!!!!
 
bunge hili ndugai litamshinda tu. yeye ni mwanaccm na chama chake ndo chanzo cha yote yaliyotokea zanzibar. tutegemee mabishano na mipasho zaidi bungeni....
 
Aliyevuruga Uchaguzi ni Seif Hamad ALIYEJITANGAZA kuwa mshindi wa uraisi bila kutangazwa na tume na kabla ya matokeo kukamilika hivyo kuleta taharuki ya usalama hivyo kusababisha ulinzi uongezwe kila mahali ikwemo kwa mkurugenzi wa ZEC Kwa ajili ya usalama wake.Kujitangaza kule ilikuwa ni uhaini hivyo wanajeshi kuingia barabarani kulinda raia na mali zao baada ya mhaini Seif KUJITANGAZA ILIKUWA NI SAHIHI.

Na utakubaliana nami kuwa baada ya mhaini kujitangaza wanajeshi walikuwa maeneo yote ya Zanzibar si Bwawani tu.
"Uhaini"?
Umekuwa jaji au hakimu?
Seif amefunguliwa mashitaka mahakama ipi ambayo imemtia hatiani kwa kosa la uhaini?
Ndugu acha kuropoka, jiongezee maarifa kwa kusikiliza wenye hoja zilizoshiba.

"Uhaini"?
Umekuwa jaji au hakimu?
Seif amefunguliwa mashitaka mahakama ipi ambayo imemtia hatiani kwa kosa la uhaini?
Ndugu acha kuropoka, jiongezee maarifa kwa kusikiliza wenye hoja zilizoshiba.

Umemjibu vena sana na kwa ustaarabu mkubwa
 
Zanzibar ni nchi itajitatulia matatizo yake yenyewe walisha jikamilishia wana bendera yao na mamlaka yao
Kama ndivyo akina shein na Maalim Seif walikuwa wanafuata nini ikulu yetu,si wangebaki huko kwao wakamaliza wenyewe,we should be critical thinkers!!!
 
A
Amani ikivurugika Zanzibar hayo yote uliyoyaainisha hapo juu yatakua si lolote kwani bila Amani na Utulivu huko Visiwani hakuna kitakachofanyika huku Bara.

Aidha bila viongozi wenye ridhaa ya wananchi na bila utawala wa kikatiba na kisheria, hakuna maendeleo ya maana.
 
Back
Top Bottom