Bunge la 12 linamaliza muda wake miezi 3 ijayo watanzania tutalikumbuka kwa lipi?

Bunge la 12 linamaliza muda wake miezi 3 ijayo watanzania tutalikumbuka kwa lipi?

BUNGE la 12 linavunjwa rasmi Tarehe 27 Juni 2025 baada ya kumaliza kazi yake kwa miaka 5 kama watanzania tutalikumbuka Bunge hili kwa lipi chini ya Spika Tulia Ackson?
"Siku moja nchi itapigwa Manda" Sipika alietumbuliwa Kazi(2022)
 
Hakuna bunge la hovyo kama hli aliloacha mwendazake tokea Tanzania ipate uhuru kwa kweli mwendazake aliiemaz demokrasia na kuifubaza ccm
 
Mm binafsi ata sitalikumbuka mana some mps siwalewagi kabisa what de be doing ..Huku kitaa njaa kali
 
1. Spika wa BUNGE NDUGAI kujiuzulu nafasi ya Spika kwa kuandika barua kwa Katibu wa CCM badala ya kujiuzulu mbele ya waajiri wake ambao ni National Assembly jambo lililostaajabisha ulimwengu mzima

2. Spika Tulia alivyozuia mijadala muhimu ndani ya Bunge yenye manufaa kwaTaifa kama utekaji, ugumu wa maisha, mgao wa umeme, nk

3. Bunge kuridhia kuuza bandari licha ya watanzania wote kupinga masharti ya Mkataba

4.Wabunge kujifanya hawaoni matatizo ya wananchi na kutumia miaka 5 ya Bunge kuwasifia Mawaziri

5.Kufukuzwa bungeni kwa Mheshimiwa Mpina akipinga utoaji wa vibali vya sukari kwa watu wasioruhusiwa na Sheria wauza vocha na watu wa steshenari na kelele za Mpina zikawezesha mwaka huu kukawa hakuna mgogoro wa sukari na bei ikatulia hakuna kelele kutokana na uhaba wa sukari wa kutengeneza uliotengezwa na kina Bashe na washirika wake.

6. Wezi na mafisadi wa Ripoti ya CAG kupigiwa makofi bungeni na kutetewa na wabunge wote kwamba hakuna wizi wowote uliotokea serikalini na kusababisha kushindwa kumwajibisha mtendaji yoyote wa serikali ndani ya miaka 5.


hayo ni machache ninayokumbuka kwa Bunge hili
Bunge hili kumbe linataswira mbaya kiasi hiki
 
BUNGE la 12 linavunjwa rasmi Tarehe 27 Juni 2025 baada ya kumaliza kazi yake kwa miaka 5 kama watanzania tutalikumbuka Bunge hili kwa lipi chini ya Spika Tulia Ackson?
Kuididimiza TANZANIA.
 
Back
Top Bottom