Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Mshahara haujaongezwa. Ila kuna national pay day(kuckulia dirishani mshahara). Itakuwa suprise, ucpokuwepo ck hyo imekula kwako unahesabika mtumishi hewa.
Hii sasa waitolee ufafanuzi, kama mtu ni mgonjwa na siku hiyo hakufika atahesabika ni mfanyakazi hewa? Vipi waliopo masomoni?
 
Hapo CCM inawauma sana wanaona wameshindwa.Serikali haijatafuta vyanzo mbadala wa mapato badala yake wanaongeza mianya ya rushwa kwa Trafic Police kwa kuongeza notification mpaka 50,000/= mpaka wabunge wakaguna na kuacha kumsilikiliza Mkullo.
 
Hata wakisema CCM hawawezi kutekeleza

Ni kweli, kwa sababu:
1. Kikwete alipewa fedha za kampeni ya urais kutoka Oman.
2. Tukaletewa kampuni ya Richmond eti ina uwezo wa kuzalisha umeme.
3. Raia wa Oman akanunua mitambo ya Richmond akijiita Dowans.
4. Tanesco / serikali wakakatisha mkataba na Dowans, na Dowans wakashtaki na watalipwa / wamelipwa hela nyingi.
5. Symbion wakainunua Dowans na hawa jamaa wameisha ingiza umeme kwenye grid ya Taifa.
 
Hata hajamaliza bajet yake wameishakata umeme loo...!
 
Licha ya mapato ambayo wafanya Biashara wanalipa TRA leseni za zamani zimerudishwa Wilayani Elfu 50 maduka yote na vijijini ni Elfu kumi ndo anamalizia mie sijaambulia chochote afu wabunge wanapiga makofi yaani sijui inamgusa nani.
 
Sijaelewa kitu chochote kile cha muhimu katika bajeti hii..
 
Chadema ni kama mwanamke mjamzito akifanyiwa zuri kwake karaha akifanyiwa baya ndio tabu! Sasa mnataka Serikali ipuuze kila linalosemwa na Upinzani!

Tatizo nikwamba magamba mna-copy halafu mna-edit bila kutumia professionals kwahiyo inakuwa balaa zaidi, nakwakuwa hata copy inawasumbua yawezekana ni kama mjamzito ambaye anasumbuliwa na tatizo la kuchagua (edit) chakula na hataki kupangiwa
 
Nilipo hapa naangalia uchambuzi wa budget kupitia ITV. Inaelekea huyu mtaalam anayehojiwa hajui Kiswahili vizuri. Je kama si Mtanzania, tumekosa wataalam wa Kitanzania wanaoweza kujieleza kwa ufanisi?
 
Punguzo la kodi kwa mfanyakazi wa umma na sekta binafsi haijulikani ni kiasi gani. Wamesema wanaondoa kodi posho kwa wafanyakazi wa umma (hapa tegemeeni posho kukua maradufu serikalini na katika taasisi za umma). Wameongeza kodi ya sigara na pombe (mh sijui tuanze kunywa mataputapu na kuvuta bangi!!!). Mkulo amesema wilaya husika zitakuwa zinatoza ushuru (sijui sasa ukuaji wa sekta binafsi itakuaje?). Sekta ya madini haifahamiki kutarekebishwa kitu gani (mrahaba wa asilimia 3 wataubadilisha au wataongeza kodi ya mapato ????). Vyanzo vya mapato ya nchi havifahamiki vitatoka wapi.

Mwisho kabisa serikali yetu inapunguza utegemezi wa wahisani kwa kukopa zaidi (deni la nchi linakua nje na ndani). Mungu ibariki nchi hii.
 
Acheni pumba au ndo the more u study the more u become craiz ukikosa kabisa jadili hata kati ya wachumba ulionao nani mkali kuliko wenzie
 
Nilipo hapa naangalia uchambuzi wa budget kupitia ITV. Inaelekea huyu mtaalam anayehojiwa hajui Kiswahili vizuri. Je kama si Mtanzania, tumekosa wataalam wa Kitanzania wanaoweza kujieleza kwa ufanisi?

Siyo hajui Kiswahili, mambo ya kugugumizi hayo!
 
wana JF mnaionaje bajeti ya mwaka huu. maoni yenu yakoje maana naona kuna bia zimepanda, vinywaji baridi na mambo kaza wa kaza. vp inamsaidia raia wa kawaida maana naona kodi ya mafuta imepunguzwa na kilimo pembejeo nazo unafuu unaendelea, kuna mambo mengi ya kuangalia hapa kabla hujatoa maoni yako.
 
Nilichovutiwa na hotuba ya Mkulo ni kupunguzwa kwa posho, safari na semina zisizonamaana serikalini. Pia punguzo la kodi katika kilimo, pembejeo itasaidia kushuka kwa bei za vyakula (wakichanganya na kushuka kwa bei ya mafuta kama watapunguza kodi ya mafuta).
 
Back
Top Bottom