Bunge la Ufaransa lafanya kikao jioni hii na baadae kupiga kura kumuondoa waziri mkuu Michelle Barnier

Bunge la Ufaransa lafanya kikao jioni hii na baadae kupiga kura kumuondoa waziri mkuu Michelle Barnier

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Waziri Mkuu wa Ufaransa Michel Barnier ambae yupo njiani kurejea Ufaransa kutoka katika ziara nchini Saudi Arabia, anatarajiwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na Bunge la nchi hiyo na hivyo kuipundua serikali yake.

Vyama vya upinzani nchini Ufaransa vikiongozwa na Maria Le Pen muda huu wapo wakifanya kikao na kujadili masuala mbalimbali kabla ya kupiga kura hiyo jioni hii.

Hatua hiyo yatokana na mvutano katika kukubaliana masuala mbalimbali yahusuyou bajeti na uchumi wa nchi hiyo ambapo vyama vya upinzani vimeona suluhisho ni kumuondoa bwana Barnier.

Tuendeee kufuatilia taarifa hii jioni hii kutoka Paris na hali ya serikali ya raisi Emmanuel Macron ikiwa na wasiwasi wa kupoteza serikali na hivyo kutishia uwezo wa raisi Macron kuongoza kwa utulivu nchi hiyo ya pili kwa nguvu ya uchumi na kijeshi barani Ulaya.

PIA SOMA
- Ufaransa: Waziri Mkuu Barnier kupigiwa kura ya kutokuwa na imani baada ya kulazimisha kupitishwa kwa bajeti
 
Marie le Pen aongea mida hii.

Ni kiongozi wa muungano wa vyama vyenye msimamo mkali National Rally Group wenye wabunge wengi.
 
Raisi Emmanuel Macron kumteua waziri mkuu mpya mara moja endapo Barnier ataondolewa.

Hiyo ni kwa mujibu wa chanzo cha Associated Press (AP)

Endapo Barnier ataondolewa Ufaransa huenda ikaingia mwaka mpya wa 2025 bila serikali wala bajeti.
 
Michel barnier aongea saa hii.

Aongelea mafanikio yake ya miezi mitatu katika kutengeneza bajeti ya kumaliza mwaka huu wa 2024.
 
Barnier asema Ufaransa ina deni la euro bilioni 60 ambazo ni wananchi wa nchi hiyio ndo itawabidi kulipa.

Bilioni 60 ni zaidi ya bajeti ya elimu au ulinzi.
 
hii SMO ya Urusi kule Ukraine inawasumbua sana serikali z ulaya, uingereza nao niliona majuzi raia zinataka uchaguzi mpya[emoji3][emoji3][emoji3]
 
1733381583411.png

Michel Barnier akiwa amezungukwa na wabunge ndani ya jengo la bunge mjini Paris. Picha na Reuters

Waziri mkuu wa Ufaransa Michel Barnier ameondolewa katika nafasi yake hiyo baadaya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na bunge la nchi hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa tukio hilo kutokea nchini Ufaransa baada ya tukio kama hilo kutokea mwaka 1962.

Ufaransa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa barani Ulaya ipo katika hali ya sintofahamu lakini kiongozi wa umoja wa upinzani Marie Le Pen amesema hana nia ya kumuondoa raisi Emmanuel Macron.

Raisi Macron anatarajiwa kutoa hotuba kwa taifa jioni ya leo kuwahutubia wananchi .

Kura 331 za kutokuwa na imani zilipitishwa na bunge huku kura 228 tu zikihitajika na ni muungano wa upinzani ndo ulochochea kura hiyo.

Le Pen amesema kumuondoa bwana Barnier ndo njia pekee ya kuhakikisha Ufaransa haingii kwenye matatizo ya kiuchumi kwa kuwa na bajeti ya hatari, isozingatia mahitaji ya kila mwananchi na yenye kuadhibu.
 
Back
Top Bottom