Bunge la Ulaya(EU) lajadili hali ya kisiasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe

Bunge la Ulaya(EU) lajadili hali ya kisiasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe

Kwani chama si mnasema kimetoka mikononi mwa washamba?
Kuna mshamba aliyebisha? Chama kimetoka kwa mazwazwa kimerudi nyumbani. Kama imekuuma chomoa afu urudi zako usukumani ukalime
 
Waliomdanganya mh Rais Mama Samia kwamba washirika wa Mbowe wamefungwa jela kwa kesi ya ugaid wanapaswa kushughulikiwa maana wamemuaibisha sana rais mpaka kutamka maneno hayo mbele ya vyombo vya habar kimataifa ili hali watu hao walishaachiwa kitambo kutokana na DPP kutoonyesha nia ya kuendelea na kesi pamoja na kuwasotesha, kuwatesa sana watuhumiwa.
 
Umoja wa Ulaya(EU) wamwambia Rais wa Tanzania mama Samia Suluhu amwachie huru kutoka jela kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA mheshimiwa Freeman Mbowe.

View attachment 2030182

Mwenyekiti wa kamati wa mambo ya nje kwenye Bunge la Ulaya, David James McAllister amesema anawasiliana na watu wengi nchini Tanzania ambapo amesema wapo kwenye hali ambayo viongozi, wanachama na wafuasi wa upinzani wanakumbana na udhalilishaji, kushikiliwa kinyume cha sheria na vitisho.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mambo ya Afrika kutoka umoja wa Ulaya, Laranjinha Rita amesema kuna sababu za matumaini Tanzania ambapo miezi ya karibuni kumekuwa na mwanzo mzuri kwa Rais Samia nyumbani na kimataifa ambapo ametambulisha baadhi ya mabadiliko.

Laranjinha amemueleza Rais Samia kwenye uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari na mabadiliko hayo yamepokelewa vizuri na jamii ya kimataifa. Pia ameongelea ruhusa ya kurudi shuleni kwa wanafunzi waliopata ujauzito.

Laranjinha amesema pamoja na hatua zilizofikiwa kuna mapungufu machache ikiwemo demokrasia ya vyama vingi ambapo hakuna uwakilishi wa upinzani kwenye bunge, mwenyekiti wa chama cha upinzani kushikiliwa na umoja wa ulaya itaendelea kufatilia kwa karibu.

Kutumia externals kama sehemu ya majumuisho ya kupambana na dola binafsi sikubaliani nalo. Mara mabalozi kuwa mahakamani inakua topic ya chama mara kujadiliwa EU. Oppositions na wanaharakati lazima wajikite kama nationals binafsi nitaelewa harakati ila si hizi sarakasi
Lazima tuamke bila NGOs nk tunaweza kusonga
 
Labda mimi ndo sio mfatiliaji,

Mambo kama haya ya upinzani kuwekwa rupango yakitokea huko Rwanda mboma huwa ni kimya sana kana kwamba hakuna kinachotokea?

Wapinzani nchini urusi pia wanapitia wakati mgumu kama vile kukamatwa na kufunguliwa kesi. Mbona sisikii kelele za kuomba waachiwe.

Sasa kama kuna watu hawawezi kuwakemea basi ni bora wakae kimya tu.

Niko Tayari kuelimishwa
 
Bunge la mashoga. Kwani hawajui kwamba tanzania ni nchi huru? Wajadili haki za binadamu ulaya ndio eneo lao. Wana mengi ya kujadili sio kujiingiza mambo ya nchi zingine.
Nchi huru wakati kutwa kuombaomba kwa hawa mabwana zenu.
 
Bunge la mashoga. Kwani hawajui kwamba tanzania ni nchi huru? Wajadili haki za binadamu ulaya ndio eneo lao. Wana mengi ya kujadili sio kujiingiza mambo ya nchi zingine.
Kwahiyo hujui kwenye hilo bunge kuna kamati inashughulikia mambo ya nje ya Ulaya au kichwa maji?
 
Kwani Tanzania ni koloni la mataifa ya ulaya inaingiliwaje mambo yake ya ndani au sio nchi huru?
Nchi huru wakati mpaka matundu ya vyoo mnaomba msaada kwa hao mabwana zenu. Uhuru ni pamoja na kujitegemea sio kutwa kuomba omba. Ukitaka usipangiwe mambo basi acha umatonya.
 
Wasiofahamu Siasa za kimataifa wanaona jambo kubwa sana na wengine wanahisi Tayari wanachukua Nchi

Magharibi wameishambulia sana Saudia kwny kadhia ya Mwandishi Khashoghi alieuwawa Ubalozi wa Saudia kule Uturuki

Lakin biashara na mambo mengine yanaendelea kama kawaida na hao Wazungu

Wazungu wanakuwa serious na Wewe ukiwakazia kwny mambo yao hizi zingine ni kitchen Talks tu

Sie tunaminya Demokrasia kuliko Rwanda na Uganda?
Kwahiyo bado tu watumwa wa hawa mabwana wakubwa?
 
Namuona Sansiro akistaafu kwa aibu kubwa. Huku Mama akinawa na akiwazodoa " Si niliwaambia wacheni Mambo yenu ya dhambi na dhuluma, mkasema ushahidi upo ! Yako wapi"
 
Kuna mshamba aliyebisha? Chama kimetoka kwa mazwazwa kimerudi nyumbani. Kama imekuuma chomoa afu urudi zako usukumani ukalime
Tatizo lako unafikiri kila mtu anachomekwa kama wewe!


Sasa kama kimerudi kwa wenyewe inakuwaje hilo bunge la ulaya lianze chokochoko..
 
Sikubaliani na uonevu wowote kwa wapinzani, ila ni upumbavu mkubwa kwa Taifa moja kuingilia uhuru wa Taifa lingine
 
Back
Top Bottom