Labda mimi ndo sio mfatiliaji,
Mambo kama haya ya upinzani kuwekwa rupango yakitokea huko Rwanda mboma huwa ni kimya sana kana kwamba hakuna kinachotokea?
Wapinzani nchini urusi pia wanapitia wakati mgumu kama vile kukamatwa na kufunguliwa kesi. Mbona sisikii kelele za kuomba waachiwe.
Sasa kama kuna watu hawawezi kuwakemea basi ni bora wakae kimya tu.
Niko Tayari kuelimishwa
Kesi za hawa, sio za kubambikizwa,wanakamatwa na ushahidi ukiwepo.Wewe utamtetea mwalifu ali hali ametenda uhalifu unaoonekana na wenye ushahidi wa wazi kama huu wa Sabaya wa CCT Cameras ,si utaonekana na wewe ulishiriki?
Kesi kama hizi tunazozifuatilia (ahsante sana mawakili na wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,kama msingechachamaa walipotaka kuwapiga ban kusikiliza mwenendo wa kesi ya Mkiti wenu mkakomaa wakalegea leo hii tusingepata mwanga huu tulioupata mpaka tukajua kwamba wengi wanaojiita wanalinda mali za raia na kuwakamata wahalifu,hawajui PGO mwongozo wa utekelezaji wa kazi zao za kila siku.Sasa hata sis tumefahamu) mtu anaambiwa mahakamani alikuwa anakwenda kukata magogo kuziba barabara,hujamkamata hata na chain saw au basi hata msumeno wa mkono.Haya anakwenda kulipua vituo vya mafuta,hivyo vilipuzi mlivyomkuta navyo viko wapi nk.lazima kelele za kutafuta haki zitakuwepo tu.Kubali usikubali ni hivyo.
Hapa ni ubambikiwaji wa makosa ambayo ni wazi aliyepewa hausiki ila amebambikiziwa ili kumkomoa.Au we hukusikia kuwa aliambiwa, tutakufungulia mashtaka ya uhujumu uchumi yale ambayo hayana mdhamana.Yule mwingine kule hai alimwakikishia mgombea kuwa watahakikisha hashindi ubunge.
Na kweli wakafanya walilofanya ikawa hivyo.Kundi hili linaloonewa hivi ndilo linalopigiwa kelele na mabaraza ambayo Tanzania imeahidi kulinda na kutenda haki kwa watu wake na kutia saini na kukubaliwa kuwa mwanachama,
Unapokwenda kinyume sasa na kujifanya ni nchi huru ndio sasa wanakufuatilia na kukushauri ubadilike.Usipofanya hivyo ban inakuhusu.
Haya yanayoonekana kuwa hayajatendeka kwa haki,ni lazima kelele ziwe nyingi sana,na zitaendelea mpaka haki itendeke kwa kupenda ama kwa kulazimishwa kwa njia ya makelele.