Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
- Thread starter
- #161
Mkuu,unawezaje kupata watu "wa fulani" bila kuwa na huyo fulani?Na watu wa mkuu atakayekuja hiyo sentensi inazungumzia hao watu na wala haizungumzii huyo mkuu, ila inawakilisha kwamba hao ni watu wa mkuu
Watauangamiza mji na patakatifu hapo inaongelewa wingi wa watu watakaouangamiza huo mji na sio mkuu mwenyewe
Mkuu mwenyewe ni nani sasa!? fungu la 27 linaelezea
Daniel 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
kwa hiyo mambo yote yanaanzia hapo sasa kwenye hilo fungu la Daniel 9:27, hilo ndio mpinga kristo anaelezewa, ndio maana hata Yesu aliposema mkiona Chukizo la Uharibifu lililonenwa na nabii Daniel alikuwa akirejea hilo fungu la Daniel
Ni kweli pia roho ya mpinga kristo inafanya kazi, lakini mnyama Masihi wa uongo ambae Wayahudi watamkubali kwasababu walimkataa Yesu ni huyo mmoja na wala sio wengi kwa hiyo huyo ndio tunayemzungumzia, hiyo Daniel 9:27 bado sioni kama imetimia...
hiyo kuharibu hapo mahali patakatifu na mji imo ndani ya majuma 69, kwa hiyo juma la 70 hapo bado halijatimia...
Mfano huwezi kusema watu wa Kikwete bila ya kuwa na Kikwete ...!