Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
- Thread starter
- #141
Sasa mkuu kama huyo mkuu atakaekuja ni Mpinga Kristo,mbona waliolivunja hekalu ni watu wa Titus?Mara ya kwanza hukuyaelewa maelezo yangu ila kwa sasa natumai umeyapata fresh, huyo mkuu Automatically ni Mpinga kristo kwasababu katika Daniel 9:27 ndio anaonekana atafanya agano na Wayahudi na fungu la 27 ndio lile juma la 70 la Daniel yaani ile miaka 7 ya mwisho kwa hiyo siyo mfalme wa Rumi, halafu kuna resume kati ya juma la 69 na 70 kwa hiyo juma la 70 bado halijatimia, majuma 69 yote yamekwisha timia...
kwa hiyo sio mfalme wa Rumi wa kipindi hicho...
Kama ni Rumi inayoongelewa hapo hebu niambie unabii ulioko kwenye Danieli 7:24-26 imetimizwaje? Maana maandiko yanasema hayo yatatokea mara tu baada ya ule ufalme wa nneSasa hapo swali linabaki kwanini hakutajwa kwa jina, Ila kwa mtiririko anaingia yeye, kwasababu mkuu unatakiwa ujiulize tena kwa nini huyo mnyama wa nne hakutajwa kwa jina!?
Lakini pia hizo falme zilikuwa zinaenda kwa series
Daniel 2:40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.
Danieli 7:24-26
24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
26 Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.
Kama unakumbuka tuliwahi kujadili hilo na tukakubaliana kuwa hiyo pembe ndogo ni Mpinga Kristo,kama hapo inasema huyu atainuka baada ya kuondoka Rumi kisha kuinuka pembe ndogo na kisha kuinuka huyu Mpinga Kristo,tunatarajia haya yawe tayari yametokea kwasababu Rumi ilishaanguka ila hayo mengine sijui ni yapi hayo
Hebu nifafanulie hapo mkuu!!