juve2012
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 3,343
- 2,040
Papa Francis,anasema kwamba mkristo bila Bikira Maria na Kanisa ni yatima.Haya ni maneno aliyozungumza hivi karibuni pale Rome.(Lourdes Grotto of the Vatican gardens).Anasema wakati fulani miaka 40 iliyopita akiwa kwenye mkutano fulani,aliwauliza rafiki zake fulani imani yao kwa Maria,wakamjibu kuwa HAWAMHITAJI MARIA KWA KUWA WAMESHAMJUA YESU ANAWATOSHA.PAPA AKAHUZUNIKA MOYONI NA KUWAONA NI YATIMA.MKRISTO BILA MARIA NA KANISA NI YATIMA.Akaendelea kwa kusema kuwa Mkristo anahitaji mama wawili ili awe na ustawi mzuri kiimani,Maria na Kanisa,na ili aweze kufanya uchaguzi sahihi katika mambo mbalimbali kimaisha,ili aweze kufuata wito sahihi kwake katika maisha,anapaswa kujiuliza kwanza kama ana mahusiano mazuri na Maria na kanisa.
Kuonyesha msisitizo baadae Papa alitweet hivi,"A CHRISTIAN WHO DOES NOT FEEL THAT THE VIRGIN MARY IS HIS OR HER MOTHER IS AN ORPHAN".
Maelezo haya ya Papa Francis yamezua mjadala huko ulaya hivi sasa.Yoyote anayetaka kufuatilia agoogle tu hiyo tweet ya Papa,zitakuja sources kibao,fuatilia hiyo mijadala.
Biblia takatifu,katika Wakolosai 1;12-14,inasema,
"mkimshukuru BABA aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.Naye alituokoa katika nguvu za giza,akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake,ambaye katika yeye tuna ukombozi,yaani,msamaha wa dhambi."
Pia nikichunguza muktadha wa mafundisho ya biblia kuhusu uhusiano huu wa "kuwa wana",sioni mahali inaposisitiza uhusiano wa mama(Maria) na mwana(binadamu),bali uhusiano wa BABA(Mungu) na mwana(binadamu) kupitia mwana wa Mungu(Yesu) kama jambo muhimu kwa ustawi wa mkristo kiimani.
Mafungu yanayoeleza hii doctrine ni meeengi mno,nitoe moja kama hili hapo chini;
"Kwa kuwa alitangulia kutuchagua,ILI TUFANYWE WANAWE KWA NJIA YA YESU KRISTO,sawa sawa na uradhi wa mapenzi yake.Na usifiwe utukufu wa neema yake,ambayo AMETUNEEMESHA KATIKA HUYO MPENDWA."
Katika waefeso 1;12 inasema
"Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake,sisi tuliotangulia KUMWEKEA KRISTO TUMAINI LETU".
Kuna yale ambayo Yesu mwenyewe anasema yeye ndiye njia na uzima,mtu haendi kwa BABA ila kwa njia yake,kuna lile la kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe...so,so,so many bible verses zinaeleza hii doctrine,kwamba ni BABA na si mama,tena intercession inafanywa na YESU,sio Maria.Ukatoliki ni ukristo,na ukristo unatokana na biblia.Papa anapata wapi authority ya kufundisha hii doctrine ya "tunamhitaji mama yetu Maria" kwa ustawi wetu kiimani?!Tena amefikia mahali anatuita sisi wakristo tusiomuomba Maria kuwa tu YATIMA?Mtu amemwambia kuwa hamhitaji Maria kwa kuwa amemjua Yesu,yeye anamuona Yatima?Maria na Yesu nani zaidi?!Nini maana ya kujiita "Christian" ikiwa "Christ" mwenyewe humtambui kama njia kuu na pekee kwako kumfikia Mungu?!Naomba mkasome wenyewe,mie nimepitia Catholic news agency na radio Vatican.