Bunge la Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) lapitisha maazimio kumtoa Museveni madarakani muda wowote

Bunge la Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) lapitisha maazimio kumtoa Museveni madarakani muda wowote

Nyie uFipa mnawategemea wazungu wawape madaraka, mtasubiri sana, Mseveni hawezi kuondoka kizembe namna hiyo.

kwa mnaotaka Tanzania pia rais aondolewe, ni kweli mna akili sawasawa? au mnadhani ni jambo jepesi kiivo?

Sanduku la kura limewashinda hamna hoja tena.
 
Nchi huru kwa uhuru wa bendera sawa, vipi uhuru wa kiuchumi??
Swala la Kiuchumi ni Lingine kabisa my friend,na karibia nchi zote za kiafrika zina struggle kuimprove uchumi wao,na si Afrika pekee hata ulaya pia,na ndio maana kama unafatilia Kujiondoa kwa Uingereza Umoja wa Ulaya lazima kutaathiri Uchumi wa nchi za Ulaya maana Uingereza ndie alikua mchangiaji mkubwa wa fedha kusukuma gurudumu la Uchumi wa ulaya.....
 
na wewe endelea kusubiri ndugu.....utafika 2020 hiyooo hapo Magu anarudi tena madarakani Museveni anazidi kudunda Uganda..Acheni kurubunika na vitu vya nje/vya wengine wekeni focus kutatua ya ndani kwenu kwa style yenu...

Hivi Bob Wine kupigwa vile hapa Tanzania hakuna aliyewahi kupigwa kama vile!??Mauaji kibao mf.Akwelina n.k yametokea tena zaidi ya Uganda hamfikirii kwanini huko nje hawayazungumzii!??
Nan kakudanganya kama hakuna alopgwa vile? Unamjuwa mdude Nyagali? Huna habar kama kapewa ulemavu kwa kipigo?
 
Utasubiri sana wewe mtumwa wa wazungu!!
Waafrika walianza kuwa watumwa wa wazungu baada ya mkutano wa Berlin wa kuligawa bara letu kwenye makoloni yao. Tutaacha kuwa watumwa wa wazungu pale tutakapopata uhuru wa KIUCHUMI.
 
Hawa wazungu kuna jambo wanalitafuta Africa ya Mashariki. " Destabilization of East Africa". Ndugu zangu tuwe makini sana tena sana.
Umakini wawe nao hao madikteta ya Afrika mashariki. Umoja wa kitaifa unahitajika sana kipndi hiki kuliko kihubiri ubaguzi kisa vyama vya siasa.
 
Ni watu wachache sana ikiwemo wewe ndio amuoni juhudi anazofanya Mheshimiwa Raisi....

Ila kwa ufupi tu, jua nyuma yake kuna watu wengi sana wanaunga juhudi zake...
Wazungu wanatoa misaada kila kukicha kwa kuonyesha kukubali afanyachk rais. Uzuri nao wanajua siasa za afrika mpinzani huwa hakubali ipande wa pili.
 
my friend sakata la Lissu mlisema wazungu wakate misaada,misaada kila siku inakuja, uchaguzi wa Zanzibar mkasema jumuiya za kimataifa zitatutenga jumuiya za kimataifa kila siku tupo nazo na support ya kutosha wanatupa, ni nyie mlisema mnaenda ICJ na kwamba Lowassa atapewa urais wake mpaka leo kimya.... Mnategemea wazungu sanaaa kama mnataka something to change should start with you,sio kuwategemea wazungu wawafanyie.

Na swala unalosema eti wakiamua watakalo,hakuna hiko kitu cha kuamua kuingilia taifa jingine tena taifa lilipiga kura na kumchagua rais aliyepo hapo madarakani, mbaya zaidi hakuna maandamano au viashiria vyovyote inavyoonyesha dalili za serikali kuwa out of control hakuna. Kila ktu kina taratibu zake,kila kitu kina mipaka yake Uganda ni Nchi Huru tena ya Kidemokrasia, hata huyoo Bob Wine amepata nafasi Kidemokrasia ndomana yupo hapo alipo, kwa vigezo kama hivi hao EU hawana mamlaka hata punje ya haradali kumuondoa Museveni madarakani na hawawezi.
To some extent nakubaliana na wewe. Watanzania wangeandamana ingeleta alarm katika jumuiya ya kimataifa.

Ila nakupinga unaposema wazungu hawawezi kufanya watakalo. Wanajua kwamba kila nchi ina sovereignty yake, hivyo hawawezi kuja kwa jinsi ya kawaida.

Wakati kichaa jiwe ana jeshi la "watu wasiojulikana" wazungu hutumia "mercenaries" wanaosababisha chaos chini ya mwamvuli wa "waasi"

Rejea situation ya russia, ukraine na crimea. Rejea waasi wa libya. Rejea waasi wa syria ambao kama sio urusi marekani angeshamtoa assad.
 
Museveni ni rafiki mkubwa sana wa EU na USA. Majadiliano hayakuwa kwamba wamtoe madarakani yalikuwa ni kwamba wanalaani kilichotokea kuna tofuati kubwa sana hapo.
 
ya Gadafi yalikua ni tofauti kabisa,na lile lilikua vuguvugu la nchi karibia zotee za kaskazini kufanya mapinduzi...

Naomba na vuguvugu la Afrika Mashatiki lianze tumuondoe Mkoloni CCM.
 
Swala la Kiuchumi ni Lingine kabisa my friend,na karibia nchi zote za kiafrika zina struggle kuimprove uchumi wao,na si Afrika pekee hata ulaya pia,na ndio maana kama unafatilia Kujiondoa kwa Uingereza Umoja wa Ulaya lazima kutaathiri Uchumi wa nchi za Ulaya maana Uingereza ndie alikua mchangiaji mkubwa wa fedha kusukuma gurudumu la Uchumi wa ulaya.....
Hivi bila uchumi imara unaweza kuwatunishia Misuli wazungu? Bajeti tegemezi, technology bado tegemezi halafu utegemee kushindana nao kweli?
 
Back
Top Bottom