Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameahirisha vikao vya Bunge hadi Machi 30, 2021, na kusema kuwa serikali ipo kwenye utekelezaji wa kujenga shule mpya 1026, kwa kutumia mkopo wa Benki ya Dunia ili kusaidia elimu ya Tanzania na kupunguza uhaba wa shule na madarasa nchini.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo Februari 13, 2021, Bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge ambapo amesema serikali kwa kiwango kikubwa imeshakamilisha mipango yake ya maendeleo hivyo kila Mtanzania ashiriki katika kuinua elimu ya Tanzania.
"Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasa naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu liahirishwe hadi tarehe 30 Machi 2021 siku ya Jumanne saa 3:00 asubuhi katika ukumbi huu hapa jijini Dodoma", amesema Waziri Mkuu.