Badala yakuelezea mabadiliko kwenye kujenga mfumo mpya wa elimu kwani tulionao unalalamikiwa kutotoa wataalamu wanaohitajika zama hizi... mnang'ang'ana kujenga madarasa zaidi.
Tunashida kubwa kwenye mifumo tunahitaji "big brains" zakuibadili mifumo dhoofu kuliko akili ndogo zinazohangaika na mawe,matofali na mchanga kuliko ufahamu!!
Badala ya kuboresha mmefuta seminars,workshops etc ambazo watu walikutana kuongeza maarifa mnapambania vitu vyakushikika tuu majengo kilasiku... Utaalamu ukowapi??? Hakuna sekta inafanyika kitaalamu kuanzia kilimo,uvuvi,ufugaji,utendaji serikalini,afya nk. Kutwa kutishiana na kufukuzana kazi badala ya kuendelezana kielimu/teknolojia!!
Mnashindwa kuandaa semina za online kuboresha utendaji na ufatiliaji Leo huyu anajenga kwa bilioni moja mwenzie nne kitu hichohicho kwakukosa taarifa sahihi!!
Waziri mkuu ameshindwa kuiunganisha serikali kiuweledi,viongozi wangeshea wanafanyaje mipango yao kupitia semina za online (bilaposho) tungekuwa na utendaji wa standard bora kabisa nchi nzima badala ya kuzunguka hovyo na kugombeza gombeza watu ambao hujawapa utaalamu wa kuifanya kazi.