Bunge laondoa kigezo cha kupitia JKT na JKU kuajiriwa vyombo vya ulinzi

Bunge laondoa kigezo cha kupitia JKT na JKU kuajiriwa vyombo vya ulinzi

Bunge limepitisha azimio la kuondoa kigezo cha kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa vijana wanaoomba nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Source BUNGE.
Wanataka wapeleke watoto wao tiss
 
Mkuu kwa TISS hata hicho kigezo cha Jakata kingeendelea kuwepo kwao siyo ishu, huko ni special case kwanza wote ni kina baba kanituma tu, na wasio na magamba ni wengi kuliko wenye nayo
Duh sawa mkuu
 
Hivi wabongo mfanyiwe nini ndio mridhike? wakifanya hivyo lawama wasipo fanya lawama
Ndugu zama hizi ajira ngumu.
Watoto wa maskini waliojitolea na waliojiunga JKT kwa majibu wa Sheria wakirudi mtaani baadhi yao hupata ajira kwenye hivi vyombo kwakuwa ushindani si mkubwa sana.
Imagine kwa hali ya Watanzania ilivyo ikitokea wilaya Moja wanahitajika vijana 10 kujiunga na jwtz.
Mbunge ataweka wake
DC ataweka wake
DED ataweka wake
OCD ataweka wake
DSO ataweka wake
DPO ataweka wake
DMO ataweka wake
Hapo sijagusa vyeo vingine.
Kwa ufupi maskini hatoboi .
Mimi nimepita jkt na nimewahi kuajiriwa direct nikiwa depo na taasisi moja nikafanya kazi nikaacha.
Nina experience ya mambo mengi ya hovyo yanayofanywa na viongozi kwenye mchakato wa ajira za ulinzi na usalama.
 
Kwa maslahi ya watoto wao wameondoa hicho kigezo.
Wameona iwe shortcut kwa vijana wao wanaotaka kuwa maafisa wa Majeshi yetu.
Kwa ufupi mmekwisha.
Hakuna mtoto wa maskini atakayeweza kuingiza pua huko majeshini.
Kwisha.

Watoto wa viongozi ni wengi kiasi gani kiasi cha kujaza ajira zote za majeshi?
 
Back
Top Bottom