Bunge laondoa kigezo cha kupitia JKT na JKU kuajiriwa vyombo vya ulinzi

Bunge laondoa kigezo cha kupitia JKT na JKU kuajiriwa vyombo vya ulinzi

Bunge limepitisha azimio la kuondoa kigezo cha kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa vijana wanaoomba nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama.

JKT iliwafanya watoto wengi wakishua wakache jeshi, sababu kama msoto upo kwenye majeshi yote tena kwa wananchi ndio zaidi, ila sasa wakishua kashazoea mkate na jibini anaambiwa anzia kwanza JKT halafu ukimaliza tu unaenda huku nakokupigania after all ni miezi mitatu tu

Sasa akishaonja mziki wa kule ndio anasusa mazima hataki kurudia makosa tena na kuishia jkt tu, kitu kinachowakera mabosi maana akiingia moja kwa moja ujedani hana ujanja atahenyeka weee ila akitoka ametoka na ajira yake, sasa huku kujenga taifa ambako unatoka halafu unarudi uraiani kusikilizia kwenda tena kwingine ndio kunawafanya wasuse wasirudie makosa
 
Ngoja tuone itamnufaisha nani. Ukiona wanadai maslahi kwa lugha moja ujue wananeemeka nayo kama ilivyo kwa wanavyovifumbia macho.
 
Kwa maslahi ya watoto wao wameondoa hicho kigezo.
Wameona iwe shortcut kwa vijana wao wanaotaka kuwa maafisa wa Majeshi yetu.
Kwa ufupi mmekwisha.
Hakuna mtoto wa maskini atakayeweza kuingiza pua huko majeshini.
Kwisha.
Acha mawazo hasi..
Kumbuka kwenda jkt Kwa mujibu wa Sheria ngazi ya kidato Cha sita siyo wote Huwa wanachaguliwa kwenda JKT, hivyo kutumia kigezo Cha JKT ktk ajira nyingi hasa za ulizi unakuwa unawakatili Hawa ambao hawakubahatika KUJIUNGA na hyo JKT
 
Yani hiki kigezo kilikuwa kinawanyima vijana wengi frusa na ukiangalia kwa asilimia kubwa izi taasi ndo zinabeba idadi kubwa ya vijana upande wa ajira like Uhamiaji, zima moto, migration, TAKUKURU n.k

Walikuwa wanazingua sana, huna kambi za kupeleka vijana wote JKT ila kazi zikitoka unabagua wakati ni wewe ulishindwa wapeleka
Exactly
 
Bunge limepitisha azimio la kuondoa kigezo cha kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa vijana wanaoomba nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama.


Kuhusa vijana kuajiriwa bila kupitia JKT na JKU​


60500007_605-1024x576.webp

Bunge limeazimia vijana wote wapewe fursa sawa katika ajira pale ambapo wamekuwa wametimiza masharti mengine yote yanayohusika na nafasi ya ajira husika isipokuwa cheti cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) hadi pale ambapo serikali itakuwa na uwezo wa kuwapokea vijana wote wanaomaliza kidato cha 4 na cha 6.
Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ameyasema hayo leo Februari 16, 2024 bungeni mjini Dodoma wakati akiahirisha shughuli za Bunge la 12.


More info :

TOKA MAKTABA:
13 June 2023

JESHI LATOA TAMKO KUSITISHWA KUPOKEA VIJANA WA JKT, BRIGEDIA JENERALI MABENA AFUNGUKA


View: https://m.youtube.com/watch?v=90Nd8wEnTWw
 
IMG_5606.jpg



Mamilioni ya watanzania wazalendo wamepaza sauti zao kupinga kuondolewa kwa kigezo cha mtu kuruhusiwa kuingia jeshi baada ya kupitia JKT.

Watanzania kwa umoja wao wamepinga azimio la Bunge kwa kuwa ni kichekesho na umaamuma mkubwa. Kitendo cha Bunge kupitisha azimio hilo kinaenda kuua kabisa nguvu ya vyombo vya dola.

Wakichangia katika mtandao wa X almaarufu Twitter watanzania wengi wameshangazwa na haya ndio maoni yao.

Ikumbukwe mapema kabla ya maamuzi hayo Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba alipinga mpango huo akilitaka bunge lifikirie kwa umakini maamuzi hayo kwani yanagusa maslahi ya vyombo vya ulinzi na usalama lakini spika Dkt Tulia alipuuzilia mbali hoja hiyo bila kutafakari unyeti wa suala hilo.

Tayari kuna minong’ono ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya maamuzi ya Spika Tulia Ackson.

Nimeambatanisha video fupi na screencaptures za maoni ya watanzania.
IMG_5596.jpg

IMG_5597.jpg

IMG_5598.jpg

IMG_5599.jpg

IMG_5600.jpg

IMG_5601.jpg

IMG_5602.jpg

IMG_5605.jpg

IMG_5604.jpg
 
Mitanzania mingi ni Mimaskini kuanzia akili mpaka roho.

Mbunge au Mwanasiasa mwenye madaraka ya juu hawezi kuhangaika kumpeleka mwanae ktk majeshi huko..

Yaani Aache kumpangia mwanae sehem nzuri kama BOT etc au connection huko CRDB , NMB then ampuganie mwanae aje kuwa polisi?

Kigezo cha JKT ni cha kipumbavu, kuna watu wamesoma nje.. wanauwezo mkubwa sana kusaidia haya MAJESHI yetu wanakosa sifa za kujoin kwa kuwa hawana certificate ya JKT kitu ambacho ni very useless..

Dunia inapoelekea ni akili sana na sio nguvu na ukakamavu.

Kwanza JKT yenyew (Mujibu) watu wanaenda miez 3 sas kuna kip kipya zaid ya kupotezeana muda.

Msifikirie kwamba hawawezi kuchomeka watu wakiamua iwepo au isiwepo hiyo JKT mtu atachomekwa tu.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Kama kigezo cha kuzitaka kura zetu kwa propaganda hizi mtashika sana masikio watu hii nchi inadharau sana shida yule mwanasesere kazi yake ni kurembua tu
 
JKT kwa sasa haina uwezo wa kuwachukua wale wote wa lazima na pia wa hiari hivyo kigezo hicho kina ubaguzi. Hakitoi fursa sawa kwa wote.
Ukikitoa kigezo hicho ina maana wote wanatafuta ajira wanaweza kudahiliwa wakikidhi vigezo vingine. Wale watakao pita ndio watafanya mafunzo ya awali ya jeshi bila ubaguzi.
 
Sina hoja coz upuuzi mtupu, Op yetu wengi walinyimwa ajira na wakaajiriwa ambao hawajapita Jkt, TISS ndyo kabisa JKT hawaitaki.
Ukiona Jkt wapo TISS ujue kuna maelekezo maalumu.
Kwahyo haina haja ata wangeifuta tu
 
Iyo JKT ifutwe kabisa mana sio Kila raia anapata Fursa ya kupitia huko, wanao pinga kufutwa kwa kigezo hicho ni wapinga maendeleo , au wanajitoa ufahamu kuwa jeshi alibebi raia wote
Ni ujinga mtupu huu unaolitia taifa hasara ya kuwaweka mbuzi zizini na kuwalaza na kuwalisha na gharama za mavazi juu kwa kodi zetu.
Huu upuuzi ulikuwa wa siasa za kuogopesha wananchi wakati ule eti tutavamiwa na mabeberu kurudi kwenye ukoloni wakati hao mabeberu wanashikilia rimoti, hata hawahitaji kukuvamia
 
Nimesikiliza sehemu ya mjadala na kuona kuwa ubovu wa mjadala wote ulisababishwa na spika mwenyewe kwani alikuwa hawasikili wote waliokuwa wanapinga kuwapo kwa kipengele hicho. Spika wa bunge sasa ni mtu wa hovyo sana linap[okuja swala la kujadili mambo nyeti ya nchi. hakuweza hata kuelewa kuwa JKT na JKU huvuta vijana wa kujitolea kusudi wapate nafasi za kujiunga na majeshi ya Ulinzi na usalama. Badala ya kuondoa hiyo advantage, hakutakuwa na haja ya mtoto kujiunga na JKT tena. Mwigulu alijitahid kutetea hoja hiyo, hata hivyo yeye mwenyewe hajui kujenga hoja.
 
JKT naona huwa wanawazalishia mali wakuu wa kambi tu na wala siyo Taifa kwa sehemu kubwa.
Kingine, siyo wote wanaotamani kuingia JKT hupata hiyo nafasi.
Hivyo, kukiweka kama kigezo, ni ujinga.
 
Uzalendo ndio nini, haya mambo ya kubaguana wenyewe kwa wenyewe au sisi kwa sisi. Mtu ni mtanzania, anavigezo vilivyo hainishwa apewe ajira, iundiwe sheria. Kama wanataka wote twende au tupitie huko waweke utaratibu wote twende. Lakini wasifanye ikawa kigezo cha kubaguana.
 
Imagine mtu aliyemaliza form four na kujiendeleza Kwa utaalamu Fulani na chombo Cha ulinzi au usalama wanahitaji mtaalamu wa fani hiyo ( mfano - fundi seremala ) na hakwenda JKT Kwa mujibu wa Sheria. Watampata wapi. Urudi utaritibu wa zamani wa kutoa Tangazo bila kuzingatia kigezo Cha kupitia JKT Ili kutoa fursa Kwa Kila mwananchi aweze kujiunga na kulitumikia taifa lake. Mchujo ufanyike ndani ya chombo husika kwa vigezo na masharti ya kozi fulani
 
Back
Top Bottom