Bunge laondoa kigezo cha kupitia JKT na JKU kuajiriwa vyombo vya ulinzi

Bunge laondoa kigezo cha kupitia JKT na JKU kuajiriwa vyombo vya ulinzi

Mkuu dunia inaenda kasi, nyakati zimebadilika mno. Tafsiri ya uzalendo kabla ya uhuru, baada ya uhuru na sasa hivi ina mukthadha tofauti kabisa!

Wengi wetu tuliopita huko na waliopo sasa kwenye ngazi za maamuzi, uzalendo wao upo wanting kwa kiwango kikubwa! Wamekuwa mfano mbaya!

Teknolojia zimebadili na kutanua wigo wa ajira kwa kiasi kikubwa. Vyombo hivyo vya kujenga uzalendo na ukakamavu vipo kwenye mindset ya kijamaa wakati dunia ilishaama huko!

Ushauri wangu taasisi hizo zibadilishwe kuwa military technical and research colleges!

Serikali iweke mazingira mazuri ya wawekezaji wa ndani na nje kuzalisha ajira za kutosha ndio iweke kigezo hicho kwenye ajira za serikali, sio kwa namna ilivyo kwa sasa.

Kwa sasa hali ilivyo, ikatokea cheche ya uasi ikashika moto kwa namna mambo yalivyo kombo na msoto mkubwa wa ajira kwa vijana walio na mafunzo ya kijeshi itakuwa balaa! Ni hatari sana!

Kipindi cha Magufuli vijana wa JKT waligoma, kitendo ambacho ni kinyume cha utaratibu wa taasisi hizo! Ile ilikuwa taa nyekundu!

Tulia kaona mbali sana!
 
View attachment 2906380


Mamilioni ya watanzania wazalendo wamepaza sauti zao kupinga kuondolewa kwa kigezo cha mtu kuruhusiwa kuingia jeshi baada ya kupitia JKT.

Watanzania kwa umoja wao wamepinga azimio la Bunge kwa kuwa ni kichekesho na umaamuma mkubwa. Kitendo cha Bunge kupitisha azimio hilo kinaenda kuua kabisa nguvu ya vyombo vya dola.

Wakichangia katika mtandao wa X almaarufu Twitter watanzania wengi wameshangazwa na haya ndio maoni yao.

Ikumbukwe mapema kabla ya maamuzi hayo Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba alipinga mpango huo akilitaka bunge lifikirie kwa umakini maamuzi hayo kwani yanagusa maslahi ya vyombo vya ulinzi na usalama lakini spika Dkt Tulia alipuuzilia mbali hoja hiyo bila kutafakari unyeti wa suala hilo.

Tayari kuna minong’ono ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya maamuzi ya Spika Tulia Ackson.

Nimeambatanisha video fupi na screencaptures za maoni ya watanzania.View attachment 2906370
View attachment 2906371
View attachment 2906372
View attachment 2906373
View attachment 2906374
View attachment 2906375
View attachment 2906376
View attachment 2906377
View attachment 2906378
Tumuunge Mwigulu Kwa lipi? Kick seeker anaungwa mkono na Chawa wake Sisi hatuna Muda naye. Kwani huko JKT wanajifunza nini zaidi ya kupalilia Maharage? Kigezo cha JKT ulikuwa uhuni usio na faida maana Mafunzo wanayokwenda kupata CCP na Kiwira ni tofauti na JKT.
 
Sina hoja coz upuuzi mtupu, Op yetu wengi walinyimwa ajira na wakaajiriwa ambao hawajapita Jkt, TISS ndyo kabisa JKT hawaitaki.
Ukiona Jkt wapo TISS ujue kuna maelekezo maalumu.
Kwahyo haina haja ata wangeifuta tu

Hawsitaki kwa sababu wanata kuajiri watoto wao na sio lingine
 
Uzalendo ndio nini, haya mambo ya kubaguana wenyewe kwa wenyewe au sisi kwa sisi. Mtu ni mtanzania, anavigezo vilivyo hainishwa apewe ajira, iundiwe sheria. Kama wanataka wote twende au tupitie huko waweke utaratibu wote twende. Lakini wasifanye ikawa kigezo cha kubaguana.

Jeshini huwa ile sio ajira kama bank ; jeshini tunaandikishwa
Listing / recruit - kuruta
 
Sio kweli kama wanataka kuingiza watoto wao wakaacha kuwaweka kwenye taasisi kama BoT, TPA au TRA.

Ifaamike kwamba JWTZ ina misingi yake iliyo imara sana. Kozi inayofanyika RTS au TMA sio kozi lelemama kwanba wanaweza kuwapenyesha vijana wao, ata kwa waliopitia JKT/JKU habari wanayo ila kupitia huko ilikua ni moja wapo ya mchujo ambao ulikua unapunguza watu kwenye usaili wanapohitaji.

Sasa fikiria wakitangaza nafasi za kujiunga na jeshi bila kigezo cha JKT nadhani watafanyia huo usaili Uwanja wa Taifa maana idadi itakuwa kubwa mno.
 
Waondoe na kigezo cha umri kwa taasisi za kiserikali miaka 30 sio mingi kiivo kumwabia mtu asiombe kazi akiwa na miaka iyo wakati ni kipindi kirefu walikua hawaajiri
 
Waondoe na kigezo cha umri kwa taasisi za kiserikali miaka 30 sio mingi kiivo kumwabia mtu asiombe kazi akiwa na miaka iyo wakati ni kipindi kirefu walikua hawaajiri
Naunga mkono hoja Mkuu.
Tena walitakiwa waseme kipaumbele ni kuanzia 35 hadi 45.
 
Kwa maslahi ya watoto wao wameondoa hicho kigezo.
Wameona iwe shortcut kwa vijana wao wanaotaka kuwa maafisa wa Majeshi yetu.
Kwa ufupi mmekwisha.
Hakuna mtoto wa maskini atakayeweza kuingiza pua huko majeshini.
Kwisha.
Hapo wanataka kuingiza uvccm kwenye jeshi.
 
Miaka ya zamani sana, TPDF ilikua inafanya direct recruitment kutoka uraiani lakini baadae ikaja kusitisha baada ya kuibuka layer ya askari/maafisa wasio na weledi. Unakuta mtu alikua jambazi, changudoa, mwizi etc. lakini anavumilia miezi minne ya depo tayari anakua muajiriwa. Hakuna kipindi kinachopima uvumilivu kama cha u-service man. Tena kwa sisi tuliopitia vikosi vya malezi kama 837KJ kipindi hiko, fatiki za shamba ni za kutosha hadi wengine wakaanza kujiengua mmoja mmoja kwa kutoroka. Kwa msoto unaopitia JKT, ukibahatika kuajiriwa lazima uwe na weledi na nidhamu ya hali ya juu tofauti na mtu aliyepitia moja kwa moja uraiani. Somehow hata kwa maafisa , unaweza ukaona tofauti kati ya afisa aliyepitia JKT, akapitia maisha ya uaskari na baadae kwenda officer cadet, na wale madogo wa BMS ambao wanachukuliwa mujibu wa sheria wanaenda miaka 3 TMA wanapewa kamisheni. Wengi wao hua wana lack leadership skills, hata uwapeleke exposure popote wakirudi kwenye loc zao wanaonesha unanga wao.
 
Bado suala la kuajiri wenye certificate na kuwaacha ama kuwababagua wenye diploma na degree kwa kigezo kwamba wana elimu kubwa hivyo serikali itashindwa kuwalipa mishara mikubwa.

Kwenye majeshi hili ni tofauti, taasisi za kiraia sijajua. Currently majeshi yanahitaji askari wengi zaidi kuliko officers. Hao degree na diploma hawatokaa kwenye u askari kwa muda mrefu watapanda haraka na kuacha gape kubwa. Na askari ndio watekelezaji wa kazi
 
Jeshini mazoezi ayajali wewe mtoto wa nani! Na ata huko JKT ndo principal (akuna kujuana) mazoezi na shuruba zote ni za wote. Kulikuwa na nafuu ya Wakufunzi wa vyombo vyetu vya usalama kwa vijana waliotoka JKT kwani basics za Jeshi wana kuwa tayari wanazijua so inawapunguzia kazi. Kwa sasa kitakachotokea 1. Wote kuanza upya wafikapo mafunzoni au kuwe na group mbili waliopitia JKT wafundishwe kivyao na hawa fresh from home wakumbane na mziki mnenne

Kwa uzoedu wangu kuwatenga waliotoka jkt wafundishwe kivyao is bad idea.
Waendelee kuchanganywa humo humo.
Kuwatenga ni kutengeneza double standard, kitu ambacho hakitakiwi kuwepo jeshi lolote.
 
Bunge limepitisha azimio la kuondoa kigezo cha kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa vijana wanaoomba nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Safi sana.
Yaani ilikuwa ni maajabu,unatoka nafunzo ya jkt badala ya kwenda ofisini au kazini moja kwa moja inabidi upitie tena chuo cha kijeshi tena.
Sasa hivi itakuwa unanyooka mpka chuo cha kijeshi bila kupitia kulima mashamba ya jkt😀
 
Back
Top Bottom