Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hatari kweli kweli....Duh🙄
Tanzanians are doomed🤔
Hii nchi haina bunge toka livunjwe kupisha uchaguzi wa mwaka 2020 uliogeuka kuwa 'uchafuzi'.Bunge lipo kwa maslahi ya watawala na si Wananchi
Nani atawapa kiinua mgongo wake za walimu, wanajeshi wetu JWTZ, polisi, madaktari na wauguzi, na watumishi chungu nzima?Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.
Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.
Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.
Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.
#MillardAyoBUNGENI
Nani atawapa kiinua mgongo wake za walimu, wanajeshi wetu JWTZ, polisi, madaktari na wauguzi, na watumishi chungu nzima?
Imagine Mke wa Rais awamu ya 4,Ana haja ya kiinua mgongo kweli? 😀😀, yeye analipwa mafao ya mke wa Rais na mafao ya mbunge? Naambiwa alikuwa mwalimu, je amefikiria kuhusu kiinua mgongo cha mke wa mwalimu?
CCM mbele kwa mbele 😀😀😀Karibuni mnisakame
Bunge Kwa Sasa linatumia muda uliobaki kupitisha vitu vya ovyo Kwa sababu ni la chama kimoja, ila wakumbuke Yana mwishoBunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.
Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.
Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.
Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.
#MillardAyoBUNGENI
Tija ya hao wenza kulipwa ni nini haswa?Leo mwanasheria mkuu wa serikali ametoa taarifa kwenye vyombo vya habari na kusema kwamba wenza wawastaafu sasa ni wakati wa kulipwa kiinua mgongo kwakuwa wenza wao wanakuwa wamelitumikia taifa kwa uzalendo mkubwa.
Hata hivyo waliowengi wameshindwa kuelewa kama ni kwa wafanyakazi wote wa serikali kuanzia ngazi za chini au sheria hiyo itahusu wafanyakazi kama raisi, makamu wa raisi, spika, na waziri mkuu pamoja na majaji
Maoni yangu ni kwamba kama sheria hii imepitishwa tunawajibu wa kupinga sheria hiyo na ikafutwa kabisa kwan kodi za wananchi inaonesha imefikia mahali ambapo zinatumika kwa faida ya watu wenye vyeo vikubwa serikalini , viongozi tulionao hawataki kujali matatizo ya wananchi wanajitengenezea sheria za ulaji ambazo hazipo kumsaidia mtu wa chini.
Nawatakia usiku mwema