Bunge lapitisha Muswada unaotaka wake wa Marais na Maspika wastaafu kulipwa kiinua mgongo

Nani atawapa kiinua mgongo wake za walimu, wanajeshi wetu JWTZ, polisi, madaktari na wauguzi, na watumishi chungu nzima?

Imagine Mke wa Rais awamu ya 4,Ana haja ya kiinua mgongo kweli? πŸ˜€πŸ˜€, yeye analipwa mafao ya mke wa Rais na mafao ya mbunge? Naambiwa alikuwa mwalimu, je amefikiria kuhusu kiinua mgongo cha mke wa mwalimu?

CCM mbele kwa mbele πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€Karibuni mnisakame
 
Ni kwanini wamewaacha watoto wa marais wastaafu? Napendekeza watoto, mashemeji, wakwe, mabinamu, wajomba na mashakazi wa marais wastaafu nao waanze kulipwa kiinua mgongo, tusibague.

Nchi maskini ambayo hata kuendesha bandari imewashinda ila watu wanawaza kujaza matumbo yao tu. Pesa ni nzuri lakini tukumbuke kwamba hazijawahi kutosha. Mishahara mikubwa,marupurupu mengi lakini bado ufisadi hauishi, hamjifunzi?

Ukiambiwa waliopitisha hiyo sheria baadhi yao kwenye majimbo yao kuna watoto wanasoma huku wamekaa chini na hawana madarasa ya kutosha huwezi kuamini.
 
Pesa haijawahi kitosha mkuu, hata wewe huwezi kutosheka pesa. Lakini kuna wakati mtu inampasa kuona aibu, mtu sasa unakuwa na tamaa hadi unatia aibu. Wananchi watakushangaa!
 
Bunge Kwa Sasa linatumia muda uliobaki kupitisha vitu vya ovyo Kwa sababu ni la chama kimoja, ila wakumbuke Yana mwisho
 
Kuna kamsemo vijana wa hovyo hua wanasema kwamba "Tanzania ni channel ya vituko kuzimu" nakubaliana kabisa na haka kamsemo, wanalipwa kiinua mgongo kwa kazi gani waliyo ifanyia serikali πŸ€”πŸ€”πŸ€” hata aibu hawaoni kwa upumbavu kama huu πŸ€”πŸ€” wanafunzi kwenye vijiji vingi tuu wanakaa chini na kusomea chini ya miti kwa kukosa madarasa na madawati, lakini watu wanakaa na kuamua kupitisha wizi kama huo πŸ€”πŸ€”

Kuna wabunge wengine wamepitisha huo wizi na majimboni kwao maji ya kunywa tuu ni mgogoro

kama kuna vitu vinatia hasara hii nchi basi ni lile jengo la Dodoma na waliomo ndani yake, pamoja na chama cha mboga mboga yani ni msiba wa taifa 🀦🀦🀦
 
Leo Mwanasheria mkuu wa Serikali ametoa taarifa kwenye vyombo vya habari na kusema kwamba wenza wawastaafu sasa ni wakati wa kulipwa kiinua mgongo kwakuwa wenza wao wanakuwa wamelitumikia taifa kwa uzalendo mkubwa.

Hata hivyo waliowengi wameshindwa kuelewa kama ni kwa wafanyakazi wote wa serikali kuanzia ngazi za chini au sheria hiyo itahusu wafanyakazi kama raisi, makamu wa raisi, spika, na waziri mkuu pamoja na majaji

Maoni yangu ni kwamba kama sheria hii imepitishwa tunawajibu wa kupinga sheria hiyo na ikafutwa kabisa kwan kodi za wananchi inaonesha imefikia mahali ambapo zinatumika kwa faida ya watu wenye vyeo vikubwa serikalini , viongozi tulionao hawataki kujali matatizo ya wananchi wanajitengenezea sheria za ulaji ambazo hazipo kumsaidia mtu wa chini.

Nawatakia usiku mwema
 
Tija ya hao wenza kulipwa ni nini haswa?
 
Iz ni moja ya sababu kwanin Mataifa ya Africa yana rasilimali nyingi lkn hayaendelei. sababu ni iz wenye nacho ndo wanazidi kujirimbikizia mahari na asiye nacho anabaki alivyo ama anazidi kushuka chini zaidi kiuchumi. Fikiria hao pesa watakazokuwa wanalipwa ni nyingi sana. Kiasi kwamba sehemu kubwa sana bado wanachi wa kawaida hawana huduma muhimu kama hospital, madarasa, maji, barabara n.k.. Na kama haitoshi wako watumishi wana mishahaa kiduchu sana hao hawafikiriwi kunyenyuliwa bali wenye nacho ndo wanajifikiria wao kuzidi kupaa tu. serikali utasikia haiajiri kwasababu haina pesa za kutosha vijana wengi ni wahitimu wako mtaani kazi hawana, wakubwa wao wanachowaza ni matumbo yao tu. Dah! inauma sana na tutafika tumechoka sana na c kufika hatutofika kwa stahili hii cc walala hoi, bali tutalala mauti tukiwa tumechoka sana!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…