Bunge lasimama kujadili na kutoa azimio la kumpongeza Rais Samia kwa kuimarisha Demokrasia na Diplomasia ya Uchumi

Badala ya kusaka wezi wa fedha kwenye report ya CGA wanahangaika na sifa. Kwa hivi hatutoki
 
Huyo anayetoa pongezi nenda jimboni kwake kaangalie raia walivyo choka!
Unampongeza Rais kutimiza wajibu wake,kweli!
 
BUNGE LA TANZANIA MSIFANYE KAZI YA CHAMA CHA SIASA, WANANCHI HATUWAELEWI. Kwanza, kama kweli walikuwa wanakerwa na kutokuwepo na demokrasia, lini waliwahi kama bunge kujadili suala la demokrasia nchini?
Mambo ya demokrasia na uhuru wa habari ilikuwa ni vita iliyokuwa inapiganiwa na wapinzani pekee. CCM walikuwa wanaimba wimbo kusema Tanzania haitaji mikutano ya siasa, tumuache rais afanye kazi. Lini CCM iliwahi kukerwa na ukiukwaji wa haki za binadamu na kuminywa kwa demokrasia na uhuru wa kujieleza?
Si ndio hao hao CCM ambao walikuwa wanasema Rais haitaji kuzurura NJE YA NCHI anatakiwa apate muda kutatua kero za wananchi. Wakaenda mbali zaidi na kusema hatutaki ubeberu. Leo mbona wanageuka. Simamieni basi msimamo wenu huo.
Lakini pia Mama tumeshampongeza sana. Wakati wa Womens' day tumempongeza, baada ya week, UWT na wadau wengine wakampongeza, leo tena bunge linapoteza muda kumpongeza badala ya kujadiili mambo ya kimkakati. Haya ni mambo ya kujipendekeza na kukosa kuwa na vipaumbele. Msitufanye sisi wajinga, mambo ya kukubali demokrasia ni baada ya kubanwa na mataifa makubwa, Mbona wakati wa JPM mliufYata???
 

MHE. ENG. EZRA CHIWELESA AWASILISHA BUNGENI AZIMIO LA KUMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 11, Kikao cha Kwanza tarehe 04/04/2023 limeazimia kwa dhati na kauli moja kumpongeza Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha Demokrasia nchini na kukuza Diplomasia ya Uchumi.

Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa Mbunge wa Biharamulo aliwasilisha Azimio hilo katika Mkutano wa 11 kikao cha kwanza kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Bunge tukufu ambapo hoja iliungwa mkono na Wabunge wote.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-06 at 09.30.04.jpeg
    26.3 KB · Views: 1
Wameona mabango waliyoweka nchi nzima hayatoshi bado watumie na muda wa bunge!!!

Oooh my poor country!!!
 
Lisimame tu. Kwanza wananchi wanao lifuatilia hilo Bunge nchini, naamini ni wachache sana.
 
Lazima BAVICHA wapinge hata maridhiano ya kitaifa

USSR
Mkuu hivi Bavicha walikufanya nini? Maana kila kukicha wewe unaangaika nao tu badala ya kufanya yako
 
Badala ya kusaka wezi wa fedha kwenye report ya CGA wanahangaika na sifa. Kwa hivi hatutoki
Wengi ni wanafiki, hata ile 1.5 tr aliyotupiga jiwe mpaka leo hatujui lile swala liliishaje
 
Tanzania ni channel ya vichekesho hilo nimethibitisha kabisa.
 
Sio kla Raisi anataka kupongezwa kama yule mjomba wenu mungu mtu watu wwngne wanapenda kazi iongee sio maneno

Watu wanakufa na njaa kwa sababu ya mfumuko wa bei ya basic needs halafu mnasema kazi iendelee; kazi gani hiyo? Mnawaongezea Wananchi TOZO huku mnazichukua Shs .80 billioni mnakwenda kufanyia sherehe ya kupongeza kushindwa kusimamia wizi wa fedha za Wananchi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…