Bunge lasimama kujadili na kutoa azimio la kumpongeza Rais Samia kwa kuimarisha Demokrasia na Diplomasia ya Uchumi

Bunge lasimama kujadili na kutoa azimio la kumpongeza Rais Samia kwa kuimarisha Demokrasia na Diplomasia ya Uchumi

Mhandisi Ezra Chiwelesa amewasilisha azimio la Bunge kumpongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuimarisha demokrasia nchini na kuimarisha diplomasia ya Uchumi.

Mhandisi Ezra pia amemshukuru Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kwa kuruhusu na kumpa fursa ya kuwasilisha hoja ya azimio.

Mhandisi amesema mambo muhimu yaliyochangia kuimarisha demokrasia ni
  1. Uamuzi wa kuruhusu shughuli za siasa hasa mikutano ya hadhara
  2. Kuanzisha vikao vya maridhiano ya kisiasa miongoni mwa vyama vya kisiasa nchini
  3. Marekebisho ya kimfumona kisheria yanayoongoza shughuli za kisiasa
  4. Kuundwa kikosi kazi masuala yanayohusu demokrasia
Hoja imeungwa mkono kwa kishindo na kinachoendelea kwa sasa ni wabunge wanaendelea kutoa hoja zao kumsifu Rais Samia.
Badala ya kusaka wezi wa fedha kwenye report ya CGA wanahangaika na sifa. Kwa hivi hatutoki
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa Kumi na Moja, Kikao cha Kwanza, tarehe 04 Aprili, 2023, limeazimia kwa dhati na kauli moja:

(a) Kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuimarisha Demokrasia nchini;

(b) Kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukuza Diplomasia ya Uchumi; na

(c) Kumuunga mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika majukumu yake ya kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumuombea afya njema, baraka na ulinzi wa Mwenyezi Mungu katika kutekeleza majukumu yake.View attachment 2576007View attachment 2576008View attachment 2576011View attachment 2576015View attachment 2576017
Huyo anayetoa pongezi nenda jimboni kwake kaangalie raia walivyo choka!
Unampongeza Rais kutimiza wajibu wake,kweli!
 
BUNGE LA TANZANIA MSIFANYE KAZI YA CHAMA CHA SIASA, WANANCHI HATUWAELEWI. Kwanza, kama kweli walikuwa wanakerwa na kutokuwepo na demokrasia, lini waliwahi kama bunge kujadili suala la demokrasia nchini?
Mambo ya demokrasia na uhuru wa habari ilikuwa ni vita iliyokuwa inapiganiwa na wapinzani pekee. CCM walikuwa wanaimba wimbo kusema Tanzania haitaji mikutano ya siasa, tumuache rais afanye kazi. Lini CCM iliwahi kukerwa na ukiukwaji wa haki za binadamu na kuminywa kwa demokrasia na uhuru wa kujieleza?
Si ndio hao hao CCM ambao walikuwa wanasema Rais haitaji kuzurura NJE YA NCHI anatakiwa apate muda kutatua kero za wananchi. Wakaenda mbali zaidi na kusema hatutaki ubeberu. Leo mbona wanageuka. Simamieni basi msimamo wenu huo.
Lakini pia Mama tumeshampongeza sana. Wakati wa Womens' day tumempongeza, baada ya week, UWT na wadau wengine wakampongeza, leo tena bunge linapoteza muda kumpongeza badala ya kujadiili mambo ya kimkakati. Haya ni mambo ya kujipendekeza na kukosa kuwa na vipaumbele. Msitufanye sisi wajinga, mambo ya kukubali demokrasia ni baada ya kubanwa na mataifa makubwa, Mbona wakati wa JPM mliufYata???
 

MHE. ENG. EZRA CHIWELESA AWASILISHA BUNGENI AZIMIO LA KUMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 11, Kikao cha Kwanza tarehe 04/04/2023 limeazimia kwa dhati na kauli moja kumpongeza Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha Demokrasia nchini na kukuza Diplomasia ya Uchumi.

Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa Mbunge wa Biharamulo aliwasilisha Azimio hilo katika Mkutano wa 11 kikao cha kwanza kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Bunge tukufu ambapo hoja iliungwa mkono na Wabunge wote.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-06 at 09.30.04.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-06 at 09.30.04.jpeg
    26.3 KB · Views: 1
Wameona mabango waliyoweka nchi nzima hayatoshi bado watumie na muda wa bunge!!!

Oooh my poor country!!!
 
Lisimame tu. Kwanza wananchi wanao lifuatilia hilo Bunge nchini, naamini ni wachache sana.
 
Badala ya kusaka wezi wa fedha kwenye report ya CGA wanahangaika na sifa. Kwa hivi hatutoki
Wengi ni wanafiki, hata ile 1.5 tr aliyotupiga jiwe mpaka leo hatujui lile swala liliishaje
 
Tanzania ni channel ya vichekesho hilo nimethibitisha kabisa.
 
Sio kla Raisi anataka kupongezwa kama yule mjomba wenu mungu mtu watu wwngne wanapenda kazi iongee sio maneno

Watu wanakufa na njaa kwa sababu ya mfumuko wa bei ya basic needs halafu mnasema kazi iendelee; kazi gani hiyo? Mnawaongezea Wananchi TOZO huku mnazichukua Shs .80 billioni mnakwenda kufanyia sherehe ya kupongeza kushindwa kusimamia wizi wa fedha za Wananchi!
 
Back
Top Bottom