Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tulimsikia Waziri wa Sanaa na Michezo wa nchi hii, Mohamed Mchengerwa, Katika kusoma bajeti yake ya mwaka huu, kuwa analiomba Bunge hilo liweze kuidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 10, kwa ajili ya kuvikarabati viwanja hivyo vya CCM, ambavyo alidai kuwa vipo Katika Hali mbaya
Ikumbukwe kuwa nchi hii ipo kwenye mfumo wa vyama vingi, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara 3(1)
Sasa inashangaza kwa chama kimoja cha siasa, kuliomba Bunge, kuidhinisha pesa, eti kwa ajili ya kuvikarabati viwanja vyake!
Hiyo ni uvunjaji wa waziwazi wa Katiba ya nchi yetu, kwa hiyo tunamuimba Waziri wa Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, aondoe mara moja hilo ombi lake, kwa kuwa utakuwa ni wizi wa waziwazi kabisa, kwa pesa za walipa kodi wa nchi hii, ambao ni wanachama wa vyama vingine.
Japo hilo ni jukumu la Bunge letu, kukemea vikali uvunjifu huo wa waziwazi wa Katiba yetu, lakini kwa namna ya Bunge letu namna lilivyowaingiza wabunge hao kwa njia "haramu" Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, sitegemei hilo litokee.
Hivyo basi kama Waziri huyo wa Sanaa na Michezo atakaidi na kuendelea na bajeti yake na wabunge wa Bunge la Jamhuri, wakaunga mkono ubadhirifu huo mkubwa wa pesa ya Umma, basi wategemee kuwa watanzania tutazipaza sauti zetu bila kuchoka, Ili watanzania waweze kuiondoa madarakani, Serikali hii ya CCM, ambao ni mabingwa wa kuivunja Katiba ya nchi yetu