Bunge liazimie Bwawa la JNHPP libadiilishwe jina liitwe Magufuli hydro project power. Marais wote walishindwa aliweza JPM pekee

Jambo jema naunga mkono hoja,ila
Watanganyika hatutaki majina ya viongozi kwenye miradi tunachohitaji ni tija na ufanisi wa miradi hiyo sawa sawa na malengo yake.
 
Weee ni nnyaa!
 
Haitaondoa hata nukta ya uovu wake.
 
Achana na unafiki.

Mbona hujaorodhesha na maovu yake ambayo yalivunja rekodi ya nchi?
 
Magufuli mwenyewe ndiye alipendekeza jina hilo wewe ni nani kupingana na marehemu?
 
Kwani hilo jina la sasa sio la marehemu?

Nadhani mchangiaji, hoja yake siyo kuitwa jina la marehemu, bali kiimani, ni yale mambo yanayoweza kuambatana na baraka au laana ya hilo jina. Hiyo ndiyo sababu za kiimani, kwa nini watu wanaobatizwa au kuslim hupewa majina mengine, na majina hayo huwa ya watu wema, huku kukiwa na imani kuwa unaweza kubarikiwa kwa fadhila zile ambazo mwenye jina hilo alikuwa nazo. Japo mara kadhaa tumeshuhudia watu wenye majina ya watu wema sana, wakiwa na matendo mabaya sana.

Imani hiyo ndiyo sababu mojawapo ya kutowasikia watu wenye majina ya watu ambao walikuwa waovu kupindukia. Umewahi kumsikia mtu akiitwa Hitler au Stallin?
 
Vijana hata hawajui historia ya nchi yao. Hajui kuna umeme wa Maji wa kidatu. Hajui kuna bwawa la Maji ya umeme kule Dodoma la Mtera. Yote hayo alijenga Nyerere.

Vijana hawajui kuna miradi mingine midogo midogo alijenga Nyerere miaka hiyo wakati hata teknolojia ipo chini.
 
Naunga hoja
Hii Hata NYERERE MWENYEWE alinyoosha mikono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…