Bunge limepoteza Wabunge wengi lakini bado hawajali kwa kuvaa barakoa


Kwani wanamuwakilisha nani hadi tuhoji?
 
Sio mbaya kujikinga lakini kama barakoa ni kujizuia na kifo watu wengi kule kwa wenzetu wasingekufa kwa korona
 
 
Ila huyo fundi mungu wako kashindwa kuitengeneza ccm, anakwama wapi?
Hivi huoni CCM sasa inaanza kupata sura ya Chama Cha siasa baada ya yule dhalim kuigeuza genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala? Uzuri umekiri kuwa CCM ilihitaji matengenezo.
 
Hivi huoni CCM sasa inaanza kupata sura ya Chama Cha siasa baada ya yule dhalim kuigeuza genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala? Uzuri umekiri kuwa CCM ilihitaji matengenezo.
Matengenezo yaliyokuwa yanahitajika kwa ccm tokea kabla hata Magufuli ni ilikuwa ni kuindoa madarakani maana ilishachokwa na kipindi chote mnasema ipo pale madarakani kwa sababu ya wizi wa kula na kutumia dola.
 
Utazani we unavaaga.
 
kamati ilitoa summary tu pale, ukitaka kujua details kaombe ripoti yote usome.

Magufuli alikuwa akipiga propaganda kuhusu Corona kwa sababu alisema eti maombi ya siku tatu ndio yameonoa Corona Tz na kupiga marufuku mtu yeyeote kutangazwa kafa kwa Corona. Hizi ndio propaganda, Samia kaanza vizuri kwa kuunda tume huru ifuatilie na iktoe mapendekezo. wewe unayeibishia tume umefanya utafiti gani?
 
Sijabisha nimehoji nimetaka tuambiwe tumeathirika kiasi gani kwa kipindi chote hicho cha propaganda za Magufuli ila badala ya kutuambia hilo wao wamekimbilia kupendekeza chanjo. Sasa yale waliyoyaeleza ndio ndio unasema ni utafiti?

Wangetueleza hali ya corona ikoje sasa Tanzania kisha ndio wakatoa mapendekezo kulingana na hiyo hali tuliyonayo hapo ndio tungeita ni utafiti ila vinginevyo kulikuwa hakuna haja ya kuunda kamati maana kila kitu kinajulikana nini kinatakiwa kufanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…