Bunge limepoteza Wabunge wengi lakini bado hawajali kwa kuvaa barakoa

Bunge limepoteza Wabunge wengi lakini bado hawajali kwa kuvaa barakoa

Ndani ya miezi sita wabunge watatu wameshafariki lazima tuhoji kulikoni hata kama wengine tuliambiwa walipata ajali.

Kwani wabunge wakichukua tahadhari ya Corona watapungukiwa na nini?

Spika pale mbele anakaa peke yake (social distance) huku third class kwa akina Halima Mdee full kubanana na kupumuliana.

Uhai ni jambo binafsi mjue, shauri yenu.

Kazi Iendelee!

Kwani wanamuwakilisha nani hadi tuhoji?
 
Sio mbaya kujikinga lakini kama barakoa ni kujizuia na kifo watu wengi kule kwa wenzetu wasingekufa kwa korona
 
Kwani kuna mtu kawazuia kujikinga kama kuna tishio la kuhitaji kujikinga ndg! Mbona mnaongea saaaana😜! Hebu njoo huku kwenye usafiri wa mabasi na 55 uone tunavyosafiri kwa social proximity mpaka raha na maisha yanaendelea kwa aman kabisa!

Nyie waoga ndio mtakufa kwa uoga wenu! Sisi watz bado tunayaenzi maono ya JPM ya kumtanguliza aliye Mkuu kuliko covid-19 yenyewe.. Mungu Muumbaji anaeendelea kutulinda🙏 na kuilinda nchi yetu Tanzania!
 
Ila huyo fundi mungu wako kashindwa kuitengeneza ccm, anakwama wapi?
Hivi huoni CCM sasa inaanza kupata sura ya Chama Cha siasa baada ya yule dhalim kuigeuza genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala? Uzuri umekiri kuwa CCM ilihitaji matengenezo.
 
Matengenezo yaliyokuwa yanahitajika kwa ccm tokea kabla hata Magufuli ni ilikuwa ni kuindoa madarakani maana ilishachokwa na kipindi chote mnasema ipo pale madarakani kwa sababu ya wizi wa kula na kutumia dola.
 
Ndani ya miezi sita wabunge watatu wameshafariki lazima tuhoji kulikoni hata kama wengine tuliambiwa walipata ajali.

Kwani wabunge wakichukua tahadhari ya Corona watapungukiwa na nini?

Spika pale mbele anakaa peke yake (social distance) huku third class kwa akina Halima Mdee full kubanana na kupumuliana.

Uhai ni jambo binafsi mjue, shauri yenu.

Kazi Iendelee!
Utazani we unavaaga.
 
Ni uvivu wako tu wa kufikiri ndio ambao unakufanya usijusumbue kufikiri na kuishia kumuhusisha Jiwe kila jambo, kabla hata ya jiwe kuanza kuwa na mitazamo yake kuhusu corona mie nilishaonaga ni propaganda kitambo tu kwenye corona. Mmeunda kamati haijatuambia tumeathirika kiasi gani na propaganda za Jiwe ila imekimbilia kushauri chanjo.
kamati ilitoa summary tu pale, ukitaka kujua details kaombe ripoti yote usome.

Magufuli alikuwa akipiga propaganda kuhusu Corona kwa sababu alisema eti maombi ya siku tatu ndio yameonoa Corona Tz na kupiga marufuku mtu yeyeote kutangazwa kafa kwa Corona. Hizi ndio propaganda, Samia kaanza vizuri kwa kuunda tume huru ifuatilie na iktoe mapendekezo. wewe unayeibishia tume umefanya utafiti gani?
 
Sijabisha nimehoji nimetaka tuambiwe tumeathirika kiasi gani kwa kipindi chote hicho cha propaganda za Magufuli ila badala ya kutuambia hilo wao wamekimbilia kupendekeza chanjo. Sasa yale waliyoyaeleza ndio ndio unasema ni utafiti?

Wangetueleza hali ya corona ikoje sasa Tanzania kisha ndio wakatoa mapendekezo kulingana na hiyo hali tuliyonayo hapo ndio tungeita ni utafiti ila vinginevyo kulikuwa hakuna haja ya kuunda kamati maana kila kitu kinajulikana nini kinatakiwa kufanyika.
 
Back
Top Bottom