Bungeni Dodoma: Hotuba Ya Waziri Mpango, Akiwasilisha Bajeti kuu Ya Mwaka 2020/2021 kiasi cha Tsh.Trilioni 34.88

Bajeti imegeuzwa kuwa kampeni, matokeo yake hata humu mitandaoni hamna uchangiaji wowote wa maana. Ni kama vile bajeti imepuuzwa na watu wenye mitazamo huru.

mimi pia nilitegemea mijadala iwe ya hoja za msingi za kuisaidia serikali kuona maeneo mahususi ya kuzingatia kuokoa sekta kama za kilimo, utalii na Biashara ndondogo
 
pongezi nyingi kwa waziri wa fedha ndg.phipo mpango kwa umakini na uhodari, hakika anastahili kuwa waziri wa fedha.
Mungu akulinde urudi tena mwakani.

tunaomba bajeti ilenge kile kilicho kusudiwa, haswa kuinua uchumi wa watu wa chidi hadi juu
 
mimi pia nilitegemea mijadala iwe ya hoja za msingi za kuisaidia serikali kuona maeneo mahususi ya kuzingatia kuokoa sekta kama za kilimo, utalii na Biashara ndondogo

Kitendo cha bajeti kugeuzwa uwanja wa kampeni za ccm, usitegemee michango yoyote ya maana. Huu ni mrejesho halisi wa watu kujitambua na kutoridhishwa na mwenendo wa mambo.
 
Ni waziri wa fedha atakayeondoka na rekodi mbaya kipindi kile alibishana na gavana Benno Ndulu kuhusu kuweka vat kwenye makato ya benki pale ndio tulijua nani ni dr halisi wa uchumi
 
Maadui wa ndani ni wale wapinga maendeleo
 
mfano mtu anapata 1m itakua kwenye kundi lipi hapo au ndio hakuna kodi

Mkuu nakudadavulia kama nilivyoelewa swali lako. Karibu.

Kumbuka kiasi cha fedha kilichotajwa ni kwa mapato kwa mwaka siyo kwa mwezi. Hivyo, kama hiyo 1m ni kwa mwezi basi unazidisha mara 12 kupata mapato kwa mwaka. Kwa hiyo, kwa 1m maana yake anapata 12m kwa mwaka. Unabeba hiyo tarakimu ya 12m na kwenda nayo kwenye jedwali.

Ukiangalia Jedwali Na. 1b." Viwango Vinavyopendekezwa ", Kwa mwenye kupokea 12m anaagukia kwenye mstari wa namba nne(4) wa jedwali tajwa hapo juu. Yaani yeye kipato hakizidi 12m, hivyo basi kodi yake kwa mwaka mzima itakuwa Shilingi ( 846,000/= + ((12,000,000 - 9,120,000) x 0.25))/=) = 1,566,000/= kwa mwaka mzima.

Hivyo kwa mwezi kodi atakuwa alipa (1,566,000 /12) = 130,500/= kulinga na kanuni zanazoongoza kukatwa kodi kwenye mshahara wake. Kuna baadhi, huwa wanakatwa kodi baada ya kuondoa malipo mengine yanayokatwa kwenye mshahara.

Hivi ndivyo nilielewa swali lako na majibu yangu ndiyo hayo. Karibu kwa maswali na ukosoaji kwa namna nilivyofanya ukokotozi huu.
 
Wa Tanzania watu wa ajabu sana.
I thought Unge focus kwenye content ya hotuba ya Bajeti, eti uka concentrate kwa Waziri kusimama Muda Mrefu Bila kunywa Maji na kukunja goti.
Hii nchi tatizo lake kuu kabisa ni akili za Wananchi wake...
[emoji23][emoji23][emoji119]
 
Mkuu ni hivi aliyenufaika ni anayepata below TZS 270,000/= kwa mwezi ndio hatakatwa kodi, Na wanaopata kuanzia TZS 271,000 hadi TZS 1000,000/= kwa mwezi ndio Kodi zao zimepungua. Wanaozidi TZS 1000,000/= kwa mwezi, ni kwamba kodi zimeongezeka.
Ohoooooo
 
Huku akitumia zaidi ya nusu saa kumsifia Magufuli !
 
nimekusoma mkuu kumbe jedwali ni la mwaka ni si mwezi
 
Hii ni bajeti ipi tena ...Mbona jedwali tofauti na lililomo kwenye bajeti ya Waziri Mpango?
Mkuu la Mpango lile liko ki mwaka, kuleta uelewa mzuri tumelileta kimwezi baadhi ya wadau wapate mnyumbuliko kama ambavyo wameuliza hapo juu.
 
Nimeangalia jedwali la makato ya Kodi kwa waajiriwa, serikali imejitahidi sana kuwapunguzia mzigo mfano: Mtumishi mwenye mshahara wa 760,000 alikuwa analipa 98,700 kodi ila atalipa 70,500 baada ya hii bajeti kupita. Hiyo 28,200 itamsaidia kupunguza ugumu wa maisha.
Angefanya hivi tangua 2015 angewaacha pazuri. Hizi hesabu kucalculate inabidi ujue maana unaweza usinielewa kama hauna elimu ya ukokotoaji Kodi kwa kutumia Income Tax Act.
 
Mpango ataiongoza Fedha for 10 years na kuandika history
 
pongezi nyingi kwa waziri wa fedha ndg.phipo mpango kwa umakini na uhodari, hakika anastahili kuwa waziri wa fedha.
Mungu akulinde urudi tena mwakani.

tunaomba bajeti ilenge kile kilicho kusudiwa, haswa kuinua uchumi wa watu wa chidi hadi juu
No. Yako ya simu umesahau mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…