Bungeni: Mbunge wa CHADEMA amtimua mpangaji wake ambaye ni Askari Polisi, adai haoni maana ya kushirikiana nae, Waziri Lugola amtisha

Nyumba ni mali yake Binafsi, kwa hiyo ameona ni heri aifanye kuwa store au afugie kuku, yuko sawa Mh Mbunge wangu
 
Kesho nyumba yake itawekwa ex..iko barabarani
 
Ibara ya 100 ya katiba ya jamuhuri ya muungano inasemaje kwani?
 
Kweli "kujisaidia ajisaidie kuku akijisaidia bata kaharibu" wao kauli zao huwa hazivunji amani ila wengine amani inavunjika,basi wengine wana kauli kali
 
Waziri umechemsha big time, this is purely contractual. Polisi inaingiaje, hapo???
 
Rais ana mamlaka ya ku revoke hati ya Nyumba ya mtu yeyote kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyumba ya huyo mbunge itaifishwe igeuzwe makazi ya Askari ‘Line police’ iwe fundisho kwake na wahuni wenzie huyo Mama

Kuna siku ataibuka kufukuza Waislam au Wakristo kwenye Nyumba anayopangisha au mwenye Basi pa abiria atawashusha Abiria kwa kuwa tu ni Wachaga au Wasukuma
 
Kusema sitaki kishirikiana ni uvunjifu was amani? Kwa vipi bwana waziri
 
Rais ana mamlaka ya ku revoke hati ya Nyumba ya mtu yeyote kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyumba ya huyo mbunge itaifishwe igeuzwe makazi ya Askari ‘Line police’ iwe fundisho kwake na wahuni wenzie huyo Mama
Hiyo sio sababu, son sheria ya Ardhi. Acheni watu wapumue
 
Mbunge wa viti maalimu kamfukuza mpangaji wake askari Polisi kwa vile kagundua polisi wamekuwa hawana uhusiano mwema na RAIA.
Huo ni mfano sahihi na kama tukifanya hivyo wote katika kila jambo kuwatenga watapata elimu ya bure kuhusu ujirani mwema.
Kwa kuunga mkono juhudi za mheshimiwa mbunge, Leo nimemnyima Lift kwenye mkweche wangu mchana huu. Ilikuwa hivi, nimewakuta jamaa wawili na huyo askari polisi. Kwa vile wananifahamu na wanajua naelekea wapi wakanipiga mkono lift. Sikufanya hiana nikasimama, polisi kama vile ana madaraka mpaka kwenye gari yangu akaingia mbele na kipiga sambusa! Wewe! Ndio alimjua Chakaza ni nani kwani nilimpa point blank kuwa siwezi kumpa lift asubiri gari zao, wengine twende.
Story zilizofuata nikajua kumbe nimeungwa mkono 100% ña hawa wawili.
Hongera mhe. Mwakagenda kwa kuonyesha njia
 
Rais ana mamlaka ya ku revoke hati ya Nyumba ya mtu yeyote kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyumba ya huyo mbunge itaifishwe igeuzwe makazi ya Askari ‘Line police’ iwe fundisho kwake na wahuni wenzie huyo Mama
Sheria gani inamlazimisha mtu kushirikiana nae???? Kama sikupendi sikupendi tuuuu....!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…