Bungeni: Mbunge wa CHADEMA amtimua mpangaji wake ambaye ni Askari Polisi, adai haoni maana ya kushirikiana nae, Waziri Lugola amtisha

Zaidi ya huu ubaguzi rais aliopandikiza kwenye nchi hii? Huyo mbunge kumbuka ndio wale rais aliwaita ni magunzi, sasa gunzi litashirikiana vipi na battery, je tochi itawaka?
Hebu imagine mtu anajaza fomu kutoka chama cha upinzani na kuandika ACT wazalendo, anaambiwa kakosea, kwa kuwa anahitajika kuandika kirefu, na hivyo jina lake linaenguliwa, kuwa siyo mgombea!

Lakini papo hapo mwingine anaandika huko cha cha CCM, anaambiwa amepatia na kupitishwa kama mgombea halali!
 
Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

Si angemuagiza wampe kota akakae tu, Hawa wateule wa Jiwe vipi
 
Mpaka hivi sasa bado natafuta Mantiki ya Kumfukuza Askari Nyumbani Kwako ambako umempangisha kwa sababu tu za Kisiasa na Hasira. Askari Kufukuzwa kuna Uhusiano gani za matatizo ya Kiuchaguzi au ya Kisiasa? Hivi ukija kuwa Mzee na ukasikia nawe Mwanao ambaye labda amekuwa Askari nae akifanyiwa hivi kama Mama utajisikiaje?

Leo hii unaposema kuwa umemfukuza Askari Kwako kwakuwa huoni umuhimu wake hivi na Wao Askari ambao kwa bahati nzuri Sisi Wananchi tunawahitaji sana kwa Ulinzi na Usalama wa Mali zetu Siku ikitokea nawe ukapatwa na matatizo wakikususia na yakakukuta makubwa utamlaumu nani?

Kama unajinasibu kuwa Wewe ni mpenda Demokrasia na unapambania Haki za Watu unapomfukuza Askari Kwako ulikompangisha uliangalia pia na upande wake wa Pili wa Familia yake ambayo ni kama vile umeinyanyasa? Kwa Kitendo hiki unategemea Kweli upate hata Mwanachama Mmoja ndani ya hiyo Familia ambaye pengine Kura yake hiyo moja na nyinginezo zingeweza Kuitoa CCM Madarakani kama unavyotaka?

Ni kweli Askari wanaweza wakawa na Changamoto zao ila Kumfukuza Nyumbani Kwako halafu unakuja Kujisifia na Kuutangazia Umma wa Watanzania ni Uthibitisho wa aina ya Roho mbaya yenye Ukatili mwingi uliyonayo. CCM haitotolewa Madarakani kwa Kuwachukia Mapolisi bali itatolewa kwa Sera, Mipango na Mikakati thabiti.

Na kilichoniuma na kunisikitisha zaidi ni kwamba haya Maamuzi yamefanywa na Mwanamama ambaye nilikuwa naamini kuwa ndiyo Jinsia ambayo Kiasili imetawaliwa na Huruma kuliko hata Wanaume. Na hakuna Kitu kibaya kama Kutengeneza Bifu na Mapolisi na leo anaweza akafurahi ila natabiri mapema kuna Hatari naiona inaelekea kwa aliyemfukuza Askari Nyumbani Kwake.

Tujifunze Kutenganisha Hasira na Utu.
 
Kangi kamshindwa Musiba atamuweza Mwakagenda ?
Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

Naapa weekend hii kuna jamaa huwa anagongea sana pombe na kapitishwa bila kupingwa ujumbe wa serikali za mitaa. Eee Mungu nipunguzie hii ghadhabu maana nimedhamiria kumpeleka.. Nadhani nimeeleweka.
 
Kwa ujinga huu unaofanywa kuwaonea wasio wana CCM, ni vema wanaotengwa, washikamane na kushirikiana wenyewe na kuwaacha CCM washirikiane wao kwa wao.
 
Mpaka hivi sasa bado natafuta Mantiki ya Kumfukuza Askari Nyumbani Kwako ambako umempangisha kwa sababu tu za Kisiasa na Hasira. Askari Kufukuzwa kuna Uhusiano gani za matatizo ya Kiuchaguzi au ya Kisiasa? Hivi ukija kuwa Mzee na ukasikia nawe Mwanao ambaye labda amekuwa Askari nae akifanyiwa hivi kama Mama utajisikiaje?

Leo hii unaposema kuwa umemfukuza Askari Kwako kwakuwa huoni umuhimu wake hivi na Wao Askari ambao kwa bahati nzuri Sisi Wananchi tunawahitaji sana kwa Ulinzi na Usalama wa Mali zetu Siku ikitokea nawe ukapatwa na matatizo wakikususia na yakakukuta makubwa utamlaumu nani?

Kama unajinasibu kuwa Wewe ni mpenda Demokrasia na unapambania Haki za Watu unapomfukuza Askari Kwako ulikompangisha uliangalia pia na upande wake wa Pili wa Familia yake ambayo ni kama vile umeinyanyasa? Kwa Kitendo hiki unategemea Kweli upate hata Mwanachama Mmoja ndani ya hiyo Familia ambaye pengine Kura yake hiyo moja na nyinginezo zingeweza Kuitoa CCM Madarakani kama unavyotaka?

Ni kweli Askari wanaweza wakawa na Changamoto zao ila Kumfukuza Nyumbani Kwako halafu unakuja Kujisifia na Kuutangazia Umma wa Watanzania ni Uthibitisho wa aina ya Roho mbaya yenye Ukatili mwingi uliyonayo. CCM haitotolewa Madarakani kwa Kuwachukia Mapolisi bali itatolewa kwa Sera, Mipango na Mikakati thabiti.

Na kilichoniuma na kunisikitisha zaidi ni kwamba haya Maamuzi yamefanywa na Mwanamama ambaye nilikuwa naamini kuwa ndiyo Jinsia ambayo Kiasili imetawaliwa na Huruma kuliko hata Wanaume. Na hakuna Kitu kibaya kama Kutengeneza Bifu na Mapolisi na leo anaweza akafurahi ila natabiri mapema kuna Hatari naiona inaelekea kwa aliyemfukuza Askari Nyumbani Kwake.

Tujifunze Kutenganisha Hasira na Utu.
Mimi kesho namfukuza mwanaccm kapanga kwenye Nyumba yetu.. Na leo nimemtumia meseji aachie nyumba...

Njoo unikamate Niko Moro.
 
Back
Top Bottom