Bungeni: Mjadala wa dharura kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta nchini. Mbunge asema tozo mbili zinaongeza 792 kwenye bei
January analeta story ambazo kila mtu anazifahamu bafala ya kuleta pointi za msingi!!!
 
Leo May 5, mbunge Kilindi, Omary Kigua ametoa hoja ya kuahirisha shughuli zake za kawaida ili kujadili dharula ya ongezeko la bei ya mafuta.

Kigua amesema kuna changamoto ya kupanda kwa haraka sana kwa mafuta ya taa, dizeli na petroli ambapo hivyo vikipanda ni kimepandishwa kila kitu na Tanzania nzima kelele ni suala la mafuta na Bunge linalo wajibu mkubwa wa kuisimamia Serikali katika jambo husika.

Kigua amesema anaamini Serikali ya Tanzania itafanya jambo kama ambavyo Serikali nyingine duniani zinavyochukua hatua kwasababu wananchi hawawezi kulalamika halafu Serikali isichukue hatua yoyote.

Spika Tulia amesema pamoja na kwamba Waziri Mkuu ameshachukua kutua, hoja hiyo ambayo imeungwa mkono na wabunge wengi itajadiliwa na wabunge kama kazi yao ya kuishauri Serikali ifanye nini kwenye jambo husika.

MUSUKUMA
Mbunge Joseph Kasheku amemshukuru Spika kwa kukubali kuwasikiliza na amesema kwa wao wanaotoka majimbo ya vijijini na kununua mafuta kwenye vidumu wananunua 5,000 kwa lita.

Musukuma ameiomba Serikali ieleze ukweli kwani mafuta yaliyopanda juzi yamenunuliwa mwezi wa pili. Musukuma amesema wafanyabiashara yeye akiwa mmojawapo wanacheza na namba.

Musukuma amesema iliwahi kushuka bei ya korosho na Serikali ilipeleka Jeshi ku-rescue suala la korosho na mpaka leo hakuna mtu anachezea bei ya korosho kwasababu wanajua Serikali inaweza kuingia kuchukua biashara.

Musukuma amesema kuna kuna kodi ziliwekwa kodi za mafuta, iangaliwe namna ya kuziondoa kwa dharula ya miezi mitatu ili mafuta yarudi kuwa chini.

Musukuma amemaliza kwa kusema nchi inakubalika kukopa kimataifa na inakopa hivyo wakope kufidia gharama ili mafuta yaweze kushuka, hakuna mtanzania atamudu na kudai hata wabunge linawapiga kwasababu wanalipwa mileage za kwenda vijijini na ya kwake inaishia Shinyanga.

Musukuma: Mheshimiwa spika mimi pia ni msafirishaji, yaani kwasababu watanzania tuna nidhamu ya kuiheshimu Serikali na kuwapa muda, hebu jiulize msafirishaji aliyekuwa anapeleka abiria kwa shilingi 30,000 Mwanza, leo mafuta yamefika 3,400 nauli bado 30,000 Hili haliwezekani, tukubaliane tuishauri Serikali na ije na kauli nzuri.

SONGE
Simon Songe: Naishauri Serikali mambo mawili, kwanza kutafuta fedha kwaajili ya kupeleka ruzuku kwenye mafuta walau kupunguza gharama za mafuta na kupunguza gharama za vitu vingine ambazo vinaenda kupanda bei.

Tuna tozo nyingi tumeweka kwenye mafuta kwaajili ya nchi na kwaajili ya bajeti tuliyoipitisha, sisi ndio wabunge na sisi ndio tulioipitisha, kuna haja ya kuangalia baadhi ya tozo tuweze kuziondoa kwa dharula kwa miezi miwili.

MHAGAMA
Joseph Mhagama: Kati ya mwezi January 2021 mpaka Mei 2022 mafuta ya petroli yamepanda kwa asilimia 92 kutoka Tshs 1,695 mpaka elfu tatu mia mbili na kitu.

Tozo mbili za fuel levy na exercise duty kwa pamoja zinachangia Tshs 792, waziri au Serikali waangalie ni namna gani tutatoka, tunajua umuhimu wa tozo za ujenzi wa mabarabara na maji hizo zibaki lakini nyingine tunaweza kupunguza matumizi ya Serikali tukaenda kuboresha maslahi ya watanzania.

KAKUNDA
Joseph Kakunda: Nilikuwa Kenya na nilikutana na waziri wa fedha, nikamuuliza mmepata wapi fedha kwenye bajeti yenu za kutoa ruzuku karibu Tshs bilioni 900, akasema wamezikopa IMF. Kwanini sisi Serikali yetu isikope kwaajili ya kupunguza maumivu kama hayo.

Ningependa kuishauri Serikali yangu, wananchi wanahitaji kupata matokeo ya haraka. Kama kuna mbinu mbadala za kuagiza mafuta ambazo zitashusha bei ya mafuta kwa haraka basi zitumike badala ya mbinu ambayo sasahivi imesababisha ongezeko la bei ya mafuta.

WAITARA
Mwita Waitara: Nchi kama Zambia, dizeli ni 2,470 lakini tunajua mizigo yao wanapitisha hapa lakini dizeli Tanzania imetangazwa bei ya EWURA zaidi ya Tshs 3000, wamezungumza bei ya mafuta Zanzibar na wanajaribu pia kutugawa.

Ni jambo ambalo Serikali lazima ichukue hatua za dharula.
Hamna kitu hapo.
 
Mwita Waitara: Nchi kama Zambia, dizeli ni 2,470 lakini tunajua mizigo yao wanapitisha hapa, dizeli Tanzania imetangazwa bei ya EWURA zaidi ya Tshs 3000, wamezungumza bei ya mafuta Zanzibar na wanajaribu pia kutugawa.

Ni jambo ambalo Serikali lazima ichukue hatua za dharula.
Sijasikia Kauli ya MwanaFA , Mwami Tale tale, Gambo, Lusinde, Temba n.k
 
Huo mjadala uwe kweli na immediate impact, sio wanajadili tu halafu mambo yanabaki vile vile huku bei ya mafuta ikizidi kupanda na kuwaumiza watumiaji.

Rais kuruhusu bei za vitu kupanda kwasababu ya vita ya Urusi na Ukraine haya ndio matokeo yake, tunaumizwa wananchi na mafisadi wajanja kwenye wizara ya nishati.

Watz tumezubaa sana.
usitarajie kitu cha maana hapo kwa Tulia Ackson.
 
Itakuwa vizuri tukajua mapato yanayopatikana kutokana na mafuta kwa mwaka 20/21 na Jun 2021 to March 2022 TBS, EWURA, Weights & Measures , TPA, Railway levy, Halmashauri levy na cost ya vinasaba, cost ya bulk procurement. Inawezekana haya makato yana contribution kubwa katika recurrent expenses zao.
 
Huyu makamba ukimsikiliza utajua anaongea la maana Ila upuuzi mtupu. Ana kaZi ya kujisifia sjui Nimeongea na Nani sjui na Nani Bila kutatua Matatizo yaliyopo. Ujinga mtupu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
walivyokua wanapitisha matozo na makodi ya ajabu kwenye mafuta walitegemea Bei zitabaki vilevile. wabunge tulio nao sio wawakilishi wa wananchi ila ni wawakilishi wa chama Chao ndio maana kwenye matatizo ya wananchi hawawanyanyui midomo ila wakiona Jambo litawahalibia chama chao wanaanza kujifanya kuongea
Well Noted Mkuu...
 
wao wanashida gani si wana miposho ya kumwanga , wananchi hawawahusu kabisaaaa, waendelee kusifiana tu na kuupiga mwingi. Wananchi wapambane tu na hali zao kama wakiona noma wahamie Burundi maana sio kesi
Atakaye waamini hao jamaa ajitafakari. Hao wanazuga tu wala hawana nia yoyote nafsini mwao.
 
walivyokua wanapitisha matozo na makodi ya ajabu kwenye mafuta walitegemea Bei zitabaki vilevile. wabunge tulio nao sio wawakilishi wa wananchi ila ni wawakilishi wa chama Chao ndio maana kwenye matatizo ya wananchi hawawanyanyui midomo ila wakiona Jambo litawahalibia chama chao wanaanza kujifanya kuongea
Ukweli mtupu
 
Back
Top Bottom