Wanabodi,
Moja ya kazi za Bunge ni Kuisimamia serikali. Bunge la Mhe. Job Ndugai, lilituhumiwa kuwa ni Bunge dhaifu kuwahi kutokea, hivyo Spika Job Ndugai kuhesabika ni Spika dhaifu kabisa kuwahi kutokea, hivyo kupachikwa jina la "Bora Spika" Kwa kuanzia mimi niliisikia sauti hii
Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...
Job Ndugai alipojiuzulu tukasema
Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa?
Kwa vile Dr. Tulia alikuwa ni Naibu Spika wa Spika dhaifu, alipochaguliwa kuwa Spika, kuna watu walidhani Bunge la Tulia litakuwa ni Bunge Dhaifu kama Bunge la Ndugai.
Nilitoa ushauri huu
Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!
Sasa hiki ndio kinatokea Leo,
Bunge la Dr. Tulia, sasa limeanza kuisimamia Serikali kiukweli ukweli!, leo limesimamisha shughuli zake zote kujadili hoja ya dharura ya Mhe. Omari Kigua, kujadili kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol na dizeli.
Hongera Sana Spika Tulia, Bunge sasa linaisimamia serikali
Keep Watching Bunge Live
na Kazi iendelee!.
Paskali.