BUNGENI: Peter Serukamba(CCM) atukana tusi kali, "F*** you"

Mimi mwenyewe nimelisikia na nimeshitushwa sana na hilo tusi la Mh Serukamba, hapa ndiyo sasa watanzania tufahamu fika sheria za bunge zinawalenga wapinzani peke yao ila ccm haziwahusu kabisa...2015 mwisho wao.
 
Ni angalizo tuu natoa kutokana na mwenendo mzima wa sasa wa bunge letu tafadhalini sana kwa wale wenye familia kwepa kuangalia bunge na familia yako maana watakuuliza maana ya matusi yanayosemwa huko utashindwa jibu. Pia nashauri TBC muiwekee password maana kwatunaotoka asubuhi nakurudi jioni tutashindwa jibu maswali ya wanetu. mfano leo watoto wakikuuliza neno alilosema Serukamba utamjibuje?? Ni angalizo tuu natoa
View attachment 90326View attachment 90326
 
Serukamba huyuhuyu ambaye hakushinda 2010 , lakini ajabu yuko bungeni ? Na anapata nguvu ya Kutukana ! Kweli Tz ni shamba la Bibi .
 
hatushangai kabisa mana tushawachoka hao maccm
 
Kama hili neno ni "rasmi" Mods waturuhusu na sisi tulitumie...
 
KWA HILI NASHAURI SPIKA AWAJIBISWE ACHUKULIWE HATU BILA KUJALI CHAMA (nimemnukuu kiongoz ccm mwanza tupo hapa tunajadili tusi la leo kwa maslahi ya wote sio chama chochote)
 
Napita tu jamani...

Chezea Lekatutigite wewe......

Bangi ya Manyovu hiyo, .. Halafu hivi inawezekana hawakumsikia kweli? Duuu... Kumbe Matusi ni ya kiswahili tu .. Kiingereza hapana... au Kifaranza no na mimi nasema hivi Putant..
 
227 kamtoa huyo mbunge nje kama alivyoahidi jana? kama hajamtoa basi alikuwa akimaanisha wabunge wa cdm wakitukana, na actually sio wakitukana, maana kutukana ni nadra, huwa wanatumia lugha kali wanaambiwa wametukana. wanaotukana wanakenuliwa meno. tushakusoma bi mkubwa, endelea tu na hadithi zako hapo mjengoni
 
ndugu hata mm nililisikia nikafikiri nimesikia vibaya, lakin I m sure nilisikia vyema, nimeverify nilichosikia kwenye sound clip link iliyowekwa na mdau humu.
jamani hawa ndo vinana wanopiga chapuo tunataka raisi kijanaaa, kijanaaa... akina desh desh na akina desh desh aaa wapi tuna safari defu bado
 
Phrase
---- you!
(idiomatic, dismissal) (offensive & markedly vulgar) Go away!
---- you-I'm not giving you any!
You've done enough to ruin our outing, so ---- you!
(idiomatic, offensive, markedly vulgar) Expression to show discontent with the other party, or to show contempt
You dare come here dressed so horribly? Well, ---- you!
(idiomatic, vulgar, offensive) A curse meaning "go to hell".
---- you-why did you eat all that cake?
Used other than as an idiom: see ----,‎ you.


Source:Wiktionary

ukitranslate kwa google kwenda swahili ni balaa haviandikiki humu
 

Mkuu story yenyewe ilikuwa hivi:
Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliitaka serikali iwachukulie hatua kali wahusika wote wanaohusika na matukio ya utekwaji na uteswaji wa baadhi ya watu,kwa kutolea mifano ya Dr.Ulimboka na Kibanda;katika hotuba hiyo,kambi imeonesha kutoridhika na mwendendo wa utendaji wa idara ya usalama wa taifa.Aidha hotuba hiyo kuna mahali imemtaja Rwakatare na mwenendo wake kabla ya kukamatwa.

Shida imeanza pale ambapo Mh.Serukamaba aliomba mwongozo wa spika,na kusema kuwa,kuna baadhi ya maswala yaliyomo ktk hotuba hiyo( hasa kuanzia ukurasa wa 1-4) yanazungumzia kesi ya Rwakatare ambayo tayari ipo mahakamani.Na kwamba kuendelea kusomwa kwa hotuba hiyo ingekuwa ni kuingilia mwenendo wa kesi na kwamba hapo ingekuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Katika kutetea hoja zao,wabunge watatu wa kambi ya upinzani(H.Mdee,J.Mnyika na T.Lisu) walisimama na kujaribu kuonesha uhalali wa hoja zao.Wote watatu walijieleza kwa kadiri walivyoona inafaa.Baada ya hapo ndipo aliposimama Mh.Serukamba na kusisitiza uhalali wa hoja yake.Sasa kile kitendo cha yeye kusimama tena,inaonekana kulikuwa na minong'ono upande wa pili(lkn hiyo haikusikika) ndipo kwa kujisahau alipojikuta ametupia hewani hicho kitu!

Kwa jinsi alivyotukana,aliunganisha haraka na maelezo yake kiasi kwamba kama Mh.J.Ndugai(aliyekuwa akiongoza) hakumkatisha;akamwacha aendelee.Baada ya maelezo ya Mh.Serukamba,naibu spika(mwenyekiti) alituoa kauli yake rasmi.Ndugai amesema kuwa mgogoro huu una mtazamo wa kikanuni,kwa hiyo ameagiza kamati ya kanuni ya bunge ikutane mara moja kujadili swala hilo kisha itoe ushuri kwa kiti cha sapika jinsi gani ya kshughulikia mambo hayo yanayoonekana yana utata.Aidha amesema hotuba hiyo ya kambi rasmi ya upinzani itaendelea kusomwa kipindi cha jioni.

Baaya ya kusema hayo Mh.Ndugai aliahirisha kikao haraka,kitendo kilichofanikiwa kuzima ukinzani wowote ambao,ni dhari ulikuwa ujitokeze.Baada ya hapo hakuna kilichoedelea tena.Kwa wenye roho ngumu,nashauri mtazame hilo bunge la baadaye,naamini kabisa hili jambo litajitokeza tena!

Kwa kifupi haya ndiyo,kwa uwezo wangu,naweza kueleza juu ya kisa hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…