CUF haijawahi kuwa chama cha upinzani huku Tanganyika hata siku moja, upinzani wao ni Zanzibar. Hili ni fundisho kwa Tanganyika, linapokuja suala la Uzanzibari hawa jamaa huungana, upinzani ni kule kwao.
Kwa mantiki hii, chadema ndio chama cha upinzani kwa Tanganyika, hao NCCR, UDP, TLP wanajidanganya sana kuungana na CUF kuikandamiza Tanganyika.
Huu ndio wakati muafaka kwa Watanganyika wenye uchungu na nchi hii kuungana na kukipa nguvu CHADEMA kwani hiki ndicho chama cha kweli cha upinzani kwetu.
Maalim Seif hajawahi hata siku moja kuwa na nia ya kweli ya mageuzi ya nchi hii, siku zote ameweka mbele maslahi yake. Muangalieni tangu pale muafaka uliomrudishia maslahi yake ya waziri kiongozi, hajawa na nguvu tena. Prof Lipumba ni boya tu pale CUF hana nguvu yoyote, anatekeleza anachokitaka Seif na sio vinginevyo na siku zote lazima kiwe kwa maslahi yake na Zanzibar na sio Tanganyika.
Naelewa nitaambiwa adui wa Muungano, au mbaguzi, lakini huo ndio ukweli, CUF ilipoteza muelekeo siku walipomkaribisha Maalim Seif, ukitaka ukweli muulize Msabaha, huyu ni miongoni mwa waanzilishi na ndio waliomkaribisha Seif pale CUF mara baada ya kukorofishana na jamaa zake wa CCM..