Elections 2010 BUNGENI: Upinzani upo ndani ya kambi ya upinzani?

Elections 2010 BUNGENI: Upinzani upo ndani ya kambi ya upinzani?

Kwa kweli jambo la kuzingatia wakati huu ni kujua kwamba we have a common enemy and that is CCM. So kwa mawazo nyangu mimi hatupaswi kuangalia tumuache nani kwenye kambi ya upiazani. wote ni wapinzani hivyo wote tuwe kitu kimoja kummbana CCM na serikali yake fidhuli. tatizo ni pale vyama vya upinzani vinapokua vibaraka wa CCM kuisambaratisha upinzani. lets be careful:juggle:
acha mawazo ya upupu kuna mapandikizi kaka! umesahau yaliyowakuta NCCR-Mageuzi?
 
ukiwa na mtazamo mfupi na usiyo yakinifu kwenye upembuzi wa mambo
utaona Chadema ni wakolofi, na huyo Hamad Rashidi yuko sahihi, hapo panahitaji elimu sana
busara na hekima kung'amua cuf hawako makini kwa sasa na Chadema
si chama cha maamuma ni chama kilichosheheni watu makini kuliko mtu anavyo
weza kujua, ni uwazi usio Pingika kuwa Cuf ni chama toto ya CCM
 
Malimbukeni utawajua tu wanakua wanajiona kama hakuna kamawao,ama kweli kipofu kaona mwezi,je tungewapa nchi hawa wabinafci nawalafi wamadaraka chadema ingekuaje?kwa hakika mtanzania mwenye akilitimamu hawezi kurudia kosa lakuipa kura chadema tena,kwahakika hawafai hata kuongoza tarafa wacha taifa,kwa ubinafci huu naudiniwao naukanda naukabila wao watapotezwa kama upepo wa kusi unavopita marikebu,hawafai kabisa,eeh mungu ulie juu tuepushe na lichadema kupata ushindi wowote ktk chaguzi zataifa hili wasije wakaliingiza taifa kta vita yaudini na ukabila kwa ubinafci wao Aaaaameen!
Do you know what you are talking about?
 
Malimbukeni utawajua tu wanakua wanajiona kama hakuna kamawao,ama kweli kipofu kaona mwezi,je tungewapa nchi hawa wabinafci nawalafi wamadaraka chadema ingekuaje?kwa hakika mtanzania mwenye akilitimamu hawezi kurudia kosa lakuipa kura chadema tena,kwahakika hawafai hata kuongoza tarafa wacha taifa,kwa ubinafci huu naudiniwao naukanda naukabila wao watapotezwa kama upepo wa kusi unavopita marikebu,hawafai kabisa,eeh mungu ulie juu tuepushe na lichadema kupata ushindi wowote ktk chaguzi zataifa hili wasije wakaliingiza taifa kta vita yaudini na ukabila kwa ubinafci wao Aaaaameen!

Tunaomba ufafanuzi naona article imejaa jazba na hamaki ! tupe ubinafsi na udini wa Chadema ili tuwarekebishe tabia ikibidi tupe na FACTS kwani inatishia amani ya taifa letu

mwenye macho haambiwi tazama,ila ukipenda chongo utasema ni kengeza,
 
Kepteni wa taarabu nini? ahaaah! nilisahau wazee wa chama cha majungu ccm
unamacho huoni,unamasikio husikii,unaambiwa huku kuna moto unasema hapana,shauriyako kaa na ushabiki wako usio nakichwa wala miguu,kama hutaki kutawaliwa na ccm hamia burundi,kwahapa tz tunatawaliwa na ccm kwasasa narais keshaapishwa ambae anatoka ccm,kama hupendi kajitundike.
 
kwanza nasikia kinyaa nikiona visiwa vidogo kama vya znz ambavyo ukilinganisha vyote havilingani hata na wilaya mbili za mko wa arusha vinakuwa na utitiri wa wabunge . huu nii upupu , ingekuwa tunalinganisha wa bunge wa znz na bara huku bara tungekuwa na wabunge zaidi ya 5000. wasepe kwao watuache huku na mambo yetu .
Ama kwa upande wangu najisikia u ha ro kwa jinchi kubwa lenye ufisadi ,unafiki na ukatili kwa wanadamu wenzao kama Maalbino kuambiwa imeungana na kajivisiwa vya kinyaa kwa ajili ya kuvifisadi!
 
CUF wao waache tamaa,wao washaungana na CCM kule Zanzibar sasa wanataka nini tena??????????? Hawa CUF ni sawa na mwanamke anayetaka kuolewa na mabwana wawili,sasa CUF wao walishaolewa na CCM hawaridhiki tu, hawafikishwi kileleni??? CUF go to hell

Samahanini kama nitakuwa nakuguseni ndipo. Wengi wa ndugu zetu wa Bara (hasa CHADEMA) mna Choyo sana. Choyo chenu kipo kila mahali na ndio maana mnapigana kila siku. Mnagombana kila siku ndani ya chama chenu lakini hili la Zanzibar mliwache kama titi la......... kwani si jambo linalowahusu.
 
Wana JF,

Ningependa kuongea na kuhoji swali la msingi kwa uongozi wa CUF, Ukiungana na Chama tawala na kuwa ndani ya serikari ya chama tawala nadhani unapoteza hadhi ya kuwa chama cha upinzani! sasa CUF nadhani watakuwa wamepoteza status ya kuwa opposition party kwa sababu wana maslahi ya kiutendaji na ki utawala ndani ya serikari ya CCM, Na ukizingatia wabunge wake wote isipokuwa wawili wanatoka Zanzibar na wapo kwa maslahi ya zanzibar hivyo wanafanya kazi kwa maslahi ya serikari yao ya CCM na CUF hivyo hawawezi kupinga mambo yanayosimamiwa na serikari yao, ni vizuri wabunge wa CUF wakaamua either kuwa independent au ku caucus na ccm, that will make sense.

Waache kucheza michezo ya akina dada poa! kwani mtaka yote kwa pupa moja humponyoka au hukosa yote

Nashangazwa na wasomi nyie! Hivyo mpaka leo hamjajuwa kuwa Zanzibar ni Zanzibar . mnashangaza kuwa hata hamuelewi serikali ya Kitaifa ikoje. Mnachotaka nyie ni kuona watu wa Visiwa vile wakigombana na mnapenda sana kujitia kimbelembele kwa mambo yasiyokuhusuni. Nyie ndio mnao ungangania muundo huu wa Muungano na baadae mnataka Wazanzibari wasiwakilishwe. Wazanzibari wana haki ya kuchaguwa nani awaongoze kwenye chombo chenu mlichokiweka. Halafu kwani wale jamaa zenu mliokuwa mkiwabeba Bunge lilipita huku wakiwa CCM mlikuwa mna maana gani iwapo kwa fikira yenu kuwa lazima kuweko upinzani ndio serikali ipate mkosoaji?
 
CUF wasanii tuu....upinzani uliotulia bungeni utakua CHADEMA + NCCR + UDP ya bwana mapesa. kungekua na usawa tanzania, CUF ingekua na wabunge wasiozidi 10, sema hako kaupendeleo ka zanzibar ndio kinawavimbisha vichwa!
 
Ngwendu, Bunge lililopita CUF hawakuwa na wabunge wa kutosha wala aasilimia 12% kuweza kuunda kambi ya upinzani hivyo ilikuwa lazima waungane na chadema kuunda kambi ya upinzani, BUNGE LILILOPITA CUF walikuwa na wabunge 38 tu hivyo walikuwa hawatoshi kuunda official kambi ya upinzani pekee yao they needed another party kukidhi hiyo idaddi ya asilimia 12% therefore kama CUF wangekuwa na idadi kamili ya wabunge basi wangeweza kuunda kambi hiyo bila kushirikisha chadema, hata hivyo kutokuwa kwenye uongozi wa kambi ya upinzani sio kwamba upinzani wao umekoma la hasha! vile vile kushirikisha CUF wakati wao ni stakeholder na chama tawala wanaweza ku subbotage mambo muhimu bungeni kwani wamekwisha uungana na CCM, HIVYO KUWA ONBJECTIVE AND SEE THE BIG PICTURE KABLA YA KUANZA KULALAMA

Kwani kuwa mpinzani kwa kuunda kikundi na kuwa mpinzani kwa kuwa si mbunge wa chama tawala kuna tofauti gani? Zaidi ya kupata priviledge fulani kwa viongozi kuna cha zaidi ? Kichwa ngumu na kujiona kwa CHADEMA hakutoiathiri CUF bali Chadema yenyewe. Chukulia mfano wa kubwagwa Marando. CUF ina wabunge wengi kutoka Zanzibar na kama tunavyojuwa Bunge ni kwa faida ya Tanganyika peke yake na CUF ni maboya tu hadi iwe katika kumchachafya Pinda kwa kuukataa unchi wa Zanzibar. Nionavyo mimi pengine kwa kuelewana na CUf , CHADEMA wangepata support.
 
Mimi naona hii opportunity kwa Chadema na wala sio kitu kibaya. Ni vizuri kwa Chadema kujua kuwa wanatakiwa waeze kujiimarisha na kusimama imara kwani jamaa hao wameshanunuliwa. Sasa hivi wanaona poa ngoja mawaziri watangazwe Zenji ndi watajua chama tawala ni nani! Watapewa wizara bomu bomu tuu na watakuwa kwishney kwani hawawezi furukuta tena ila kazi itakuwa ni kugombania vyeo.
 
baada ya cuf kuwa chama cha upinzani tuliona jinsi cuf ilivyowapa nafasi chadema ktk serekali kivuli.
lkn baada ya chadema kuapta wao wamewaweka kando cuf na sasa nafasi zaote wamechukua. jee hii inaashiria nini katika siasa za chadema? watz wengi sasa tumefumbuka macho. 2015 chadema = 0
What is Serikali kivuli? Inasaidia nini ? Kitu gani cha maana ilicholeta? Hizo ni sababu zisizo na msingi za kujitetea. Kila mtu anajua kuwa CUF imeshanunuliwa zamani na kilichobaki ni kuichimbia kaburi tuu. Hakuna mtu anayeshangaa CUF sasa kukubali kila kitu CCM inachotaka kwani uroho wa madaraka cheap ya muafaka ndio kinachowawewesa kwa sasa. Chama chenu kimeshachakachuliwa.
 
mwenye macho haambiwi tazama,ila ukipenda chongo utasema ni kengeza,

Tetea hoja kwa facts ukileta nasaha za kiswahili upo msemo una " wanukao hawajijui." Dhana za udini na ukabila ni hatari kwa jamii yetu naomba facts za udini wa Chadema, usiongee kwa dhana bila kutoa mifano halisi.
 
CUF lazima wakubali kuwa lazima wawe chini ya CHADEMA

Hapana, CUF ina mwafaka na CCM, kwa hiyo haiwezi kuwa upande wa upinzani.

- Wa-Tanzania ifike mahali tuiruhusu Demokrasia ii-play its hand, ni lazima tuhimize competition kati ya Chadema na CUF au na chama chochote kile cha upinzani, through hizi competition ndio tutapata chama imara cha upinzani watakaoshindwa watakua hawana jinsi ila kujiunga na washindi ndio hasa the heart and soul ya Demokrasia,

- Tusipende vitu rahisi rahisi, Chadema should not waste their time na Wapinzani wengine wasiotaka kuelewa political mood ya wananchi, waacheni wafu wajizike wenyewe!


William.

Ni kweli kabisa; CUF imegeukia upande wa pili wa siasa za Tanzania ambako ni tofauti kabisa na upend wa CHADEMA. Hawawezi kufanya kazi pamoja; ni wajibua CHADEMA kijiandae kufanya kazi za bunge bila kutegemea msaada wa CUF

baada ya cuf kuwa chama cha upinzani tuliona jinsi cuf ilivyowapa nafasi chadema ktk serekali kivuli.
lkn baada ya chadema kuapta wao wamewaweka kando cuf na sasa nafasi zaote wamechukua. jee hii inaashiria nini katika siasa za chadema? watz wengi sasa tumefumbuka macho. 2015 chadema = 0

Ni kweli, CUF ilishirikisha vyama vyote vya upinzani. Lakini kwa vile sasa hivi CUF siyo chama cha upinzani kutokana na mkataba wake na chama tawala. Inabidi kisijihusishe na siasa za upinzanei tena, ibaki kuwa branch ya CCM.
 
Ni kweli maneno yako maana ndio maana hawakuwashirikisha wenzao kuunda kambi ya upinzani bungeni kwa kujiona wao ndio wapinzani peke yao, hawakuwashirikisha kwa kuwapa japo umakamu.

Nadhani tuangangie bila kusahau historia inasemaje. Kwanza, ni CUF katika uchaguzi mdogo wa mbeya walimwekea pingamizi Shitambala ambaye ni dhahiri alikuwa anashinda. Ni kwa mwendo huo CCM wakashinda. Pili ni A.L Mrema alisema ndani ya mkutano mkuu wa CCM kuwa CCM haikamatiki na imekuwa inakula kwake kila siku, ili hali alikuwa na mgombea urais. Tatu,NCCR siku zote imekuwa inapingana na misimamo ya chadema ikiegemea CCM. Mfano Tarime ngome ya Chadema, CUF na NCCR walisimaisha wagombea walioasi chadema, matokeo yake kura zikagawanyika na jimbo kwenda ka CCM.
Hivi kwa mwenendo huo kuna sababu ya kuwa na ushirikiano na watu hawa kweli! Kuna makovu ya kuhujumiana na kwa mtazamo wangu Chadema wako sahihi. Kama ni ushirikiano basi hao washirikishwe lakini isiwe ni sharti kwa sababu wameshawaumiza Chadema sana.
 
sio kila ushauri unaotolewa na mtoto wa kambo ni ushauri mbaya wakati mwingine unaweza ukafaa
cuf lazima mkubali kuongozwa na CHAMA MAKINI yaani CHADEMA.
 
Jamani jana nimesikia mahojiano BBC ambapo Mh Mbowe alikuwa akitoa ufafanuzi wa jinsi ambavyo CUF hawakutaka kuungana na Chadema baada ya kuombwa kwamba wafanye alliance katika upinzani. Mbowe alisema kuwa aliambiwa na Hamad Rashid kuwa wao hawataungana na Chadema lakini wataungana na vyama vingine vya upinzani, ingawa wanajua kwa hakika kuungana kwao hakuwezi kuwaezesha kuunda serikali kivuli.

Na hapo hapo alihojiwa Hamad Rashid wa CUF kuhusu kutoridhia kwao kujiunga na Chadema, na alisema kuwa wao walikataa kujiunga na Chadema kwa kuwa kilikataa kufanya alliance na vyama vingine vya upinzani. Alichukulia mfano wa bunge lililopita ambalo wao walishirikiana na vyama vingine vya upinzani kuunda serikali kivuli.

Kwa maoni yangu napenda niwakumbushe CUF kwamba Chadema pekee sasa ina uwezo wa kuunda serikali kivuli bila kushirikiana na chama chochote. Na ni haki ya Chadema kama chama kilicho na uhalali wa kuunda serikali kivuli, kuchagua chenyewe ni nani wa kuwa naye katika kambi yake na ni yupi hafai kuwa katika kambi yake. CUF kama anayekaribishwa katika serikali ya umoja kivuli hana haki ya kuichagulia chadema chama rafiki. Utakuwa ni uhuni kudai kwamba ili washirikiane lazima vyama vyote vinavyoitwa vya upinzani vishirikishwe. Hii ni kuilazimisha Chadema kufanya jambo ambalo haitaki na jambo hili halikubaliki.

Kuna mfano utokanao na wao CUF, kwamba hata wao wakijua kwamba kuna vyama vingi vya siasa na wakijua wao kwamba ndio Chama kikuu cha upinzani Zenji waliamua wao pekee bila kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ambavyo vilikuwepo kukaa na Serikali ya CCM na kufanya muafaka ambao unawanufaisha wao tu na si vyama vingine. Hakuna ambaye amewapigia kelele kwa jambo hili bali vyama vingi vimekaa kimya vikijaribu navyo kuona kwamba vinajaribu kujijenga ili na vyenyewe vifike hatua waliyofikia CUF. Ni uhuni kujifanya CUF kuwa wao wana uchungu wa kushirikiana na vyama vingine sasa katika bunge hili, wakati hata wao hawaamini rohoni mwao hiyo dhana kwamba ni sawa.

Kwa upande mwingine nawashauri viongozi wa Chadema kutokubali kuungana na CUF kabisa katika serikali kivuli maana leo CUF sio chama cha upinzani. Ni uongo na ulaghai kabisa tukiita CUF kuwa ni chama cha upinzani Tanzania. Kwani wanampinga nani wakati wote wako serikalini? Kawaida mnapokuwa mnaendesha serikali ya mseto ina maana wote mnakuwa na makubaliano katika uendeshaji wa serikali sasa hapo nani anayepinga mwingine wakati wote nyie ni watawala? CUF kwa sasa hivi kinatumika kusambalatisha upinzani kwa kujivika sura ya upinzani lakini ukweli ni kwamba wao kwa sasa hivi hawapo upinzani tena bali wako serikalini! Nawasihi viongozi wa Chadema wasijaribu kabisa kujishirikisha na CUF.

Pia napenda kuwashauri Chadema kushirikiana na Chama cha NCCR tu kama kitaonyesha kuhitaji kufanya hivyo pamoja na tofauti zilizopo. Vyama hivi vinaweza kuingia makubaliano na kushirikiana. Najua kuwa kuna mtafaruku wa mwenyekiti wao kuhusiana na mambo ya uchaguzi lakini bado naamini hayo ni mawazo yake binafsi lakini kichama, Chama kinaweza kuwa na mawazo tofauti. Nasema hivi kwa sababu Chama si Mbatia, bali Mbatia ni sehemu ya Chama. Lakini wakiona wao hawawezi kushirikiana nanyi waacheni.

Nawatahadhalisha sana Chadema kuepuka kuungana na TLP na UDP maana wao walishajipambanua wazi kuwa wao si wapinzani. Wao na CUF wako sawa. Ni mapandikizi ya CCM na wanaweza wakaiunga mkono CCM if they wish na at the end historia itawahukumu. Waache wakae wanavyotaka, wakitaka kuwaunga mkono sawa, wasipotaka waache maana sisi wananchi tuliowapigia kura nyingi nyie tunajua nini la kufanya na tutawamaliza wakati ujao.

Nihitimishe kwa kuomba tena viongozi wa chadema kufanya kazi kwa nguvu bila kujali nani atawaunga mkono au la, na huku mkijua sisi wananchi tuko nyuma yenu. Mtu au kikundi chochote kisiwatishe maana wananchi bado tuna imani na nyie. Simamia haki na sheria na sisi tutawapa reward. Msishinikizwe na chama chochote kwa tishio la kutowaunga mkono. After all, vyama vyote tofauti na CCM, viko vichache tu. Na hata kama mungeweka msimamo mmoja, wingi wenu hauwezi kubadilisha maamuzi ya CCM. Kwa hiyo kujitoa kwa CUF na wengine hakuwezi kuwatisha tena. Wacha waendelee kushirikiana na wala nchi maana nia yao ni kula nchi pia. Sisi Chadema nia yetu ni kuona mabadiliko katika Katiba, siasa na uchumi. Tutasimamia kile tunadhani ndio sahihi na mwisho agenda zote tutazirudisha kwa wananchi wenyewe waamue. Nina hakika kwa kansa iliyokwisha kamata CCM hakutakuwa na mabadiliko ya maana kwani ahadi zao hazitekelezeki, ufisadi utadumu kwa kasi zaidi, na tumesha anza kuona indicators za mfumuko mkubwa wa bei sasa kwa kila kitu kuanza kupanda bei kwa kasi ya ajabu.

HIMA TUKAZE BOOT NA TWENDE MBELE BILA WOGA.
 
My deduction on CUF-CHADEMA SAGA: - If CCM-bara and CCM-VISIWANI is equal and if CCM is equivalent to CUF in Znz then CUF both in bara and ZNZ is equivalent to CCM in bara and visiwani. That is to say CUF=CCM au ukipenda weka hivi CUF=CCM (B) au CCM chipukizi
 
Back
Top Bottom