Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,351
- 9,855
Hongera Mzee Mohamed Said kwa kutujuza historia ya nchi yetu. Kuna wakati nashangaa kwanini historia imepindishwa makusudi hivi na kumnyenyua mtu mmoja na kuwapotezea wahusika wakuu. Maana kila mtu anajua Nyerere alitoka mashambani huko akaja mjini akakutana na magwiji wakamshika mkono. Walimpa miongozo, fedha, chakula,malazi, connection nk bure. Lakin ghafla historia ya nchi hii imekuwa ni yeye tu! Yaleyale ya Magufuli kujifanya nchi nzima yeye ndo mzalendo peke yake.. mungu mtu, ndo hulka zile zile za Nyerere. Walichotofautiana ni kuwa Nyerere alikuwa smart. Lakin the same character. Huwezi andika historia ya nchi hii ukaacha kuwaweka mbele kina Sykes, Rupia, Kambona,Mwapachu nk.. lakin hawasemwi. Asante kwa kutupa ukweli. Ubarikiwe sana Mzee Mohamed [emoji120]