Najaribu kuelewa ulichoandika ila sijapata hata moja sijui ulitaka kusema nini ili kumaanisha kitugani maandishi yako hayaeleweki
Ewe Mnyamwezi wa Fundikira: nashukuru umekiri uelewa wako ni mdogo, nitakusaidia bure nami nilipata bure. Mosi, nilimtakia Sheikh Moh'd Eid el Faitr nami nikakiri nimechelewa.
Pili, nilimkumbusha kitabu chake kizuri kinaitwa "Abdulwaheed Sykes the Forgotten Struggle", ambamo aliwachachafya TANU eti kwa kudogosha mchango wa familIa ya Sykes (asili yao Wazulu kutoka Natal baba yao Mzee Mbokweni alikuja kama soldier wa Jarumani WW2). Ushakisoma hiki kitabu? Ninacho, tuwasiliane upenuni. Lazima uchukue kile cha Kiingreza, alijatoa translation ya Kiswahili akawa amekichakachua kile orijino. Mie ninavyo vyote Alhamdullilah nitakupa tukikutana Inshaallah.
Tatu, nikamsema kwamba amelalamika kina Sykes kutothaminiwa, ndipo hilo tangazo la CCM nikampa, likisema Sykes mdogo (Abbas, wa mwisho, walikuwa 3) kumbe alishapewa nafasi adhimu kuwa Balozi wa JMT nchi karibu 20 zikiwemo Mexico, Algeria, Ufaransa na Sahrawi. Maana yangu ni kuwa kumbe kina Sykes walithaminiwa, alichosema kitabuni kwake si kweli.
Aidha, nikaendelea kumkumbusha kuwa kile kitabu chake alijikita mno kusifia Waislamu, hususan wa Kariakoo khasa Wamanyema (sina hakika lakini sintoshangaa kama Shehe wetu ni Mmanyema wa Kariakoo) kana kwamba ni wao tu waliopigania uhuru wa Nji hii. Nikafafanua kuwa hii nayo si kweli, nikampa mfano wa Rais Samia na Waziri Mkuu na Mufti wetu na Mufti wa Zanzibar na Jaji Mkuu wa Zanzibar na Jaji Mkuu wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Makamo wake wawili, wote ni Waislamu walikuwa 70% ya frontbench kwenye Ibada ta Askofu kumzika Magufuli. Wakristo pekee walikuwa ni CDF Mabeyo na Supika Ndugai (ofkozi wangekuwa watatu lakini Dr Mpango alikuwa bado hajateuliwa).
Do you see my point?
Nikamwambia Sheikh anazeeka vibaya, bado ana kumbukumbu zama za AMNUT, Bantu Group na Mzee Ng'winamila wote Wanyamwezi wenzenu.
Niongeze kuwa BAKWATA kawasema vizuri kwenye kitabu chake (kile cha Kimombo, alipofanya translation akawageuka!) ambao kwa sasa wanakaa nafasi ya juu kabisa katika mshikamano wa Taifa letu baada ya novena ya pamoja kuombea tunusurike Corona. BAKWATA walichangia uhuru wa Nji hii walipokataa kurubuniwa na wadini eti wajitenge kama Pakistan ya India.
Mwisho, nikamkosoa kwa kujikita zaidi kutangaza CV yake badala ya CV ya marehemu, hili waliliona wachangiaji wengine bila shaka ukiwamo nawe.
Are we together?
Sasa rudi usome tena tuone kama utaelewa. Kama bado nitafute upenu nikupeleke IFM (shule ya Sheikh Mohamed!) tujajadili naye kwa faragha.