TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

Muhammed Said, this is not about you!

Nimewahi kukueleza si mara moja, umesoma-soma, ndio, lakini hukuelimika.

Tanzia ya mwenzio unaianza na story kuhusu WEWE ulivyokaa Dubai Carlton Hotel.

Aya ya pili interview yako WEWE na BBC kuhusu maisha na kifo cha Nyerere

Aya ya tatu kitabu chako WEWE kuhusu historia ya TANU na maisha ya Gerezani na Kariakoo

That's bad form, unbecoming a gentleman commentator, huo sio uandishi wa kiuungwana.
Kuna kaji ka ukweli fulanihivi ,
ila kwa vile mimi kwa kuwa si muandishi mahiri nilidhani ndio sikufahamu mada yake.
Ni aina ya uandishi wenye Deep ubdrstanding of story.
Ilipaswa iwe kwanza habari za Kifo chake kisha ndio ifuatie maelezo mengine.

Lakini Maandiko yenyewe pia ni matamu kasoro ni mpangilio tuu ndio ume tutatiza,
 
ila kwa vile mimi kwa kuwa si muandishi mahiri nilidhani ndio sikufahamu mada yake.
Sio wewe tu, watu kibao hatuelewi hiki kituko cha tanzia.

Muhammed Said anaangalial kila kitu duniani katika lenzi ya TANU, Nyerere, wazee wa Aggrey na Tandamti, na mfumo uliowanyima vyeo baba zake wadogo wa Gerezani.

Tanzia gani haisemi nani kafa bali maisha ya Muhammed Said ?
 
Sheikh Mohamed Said: Eid Muvarak belates! Kile kitabu chako kizuri cha Abdulwaheed Sykes the Forgotten Struggle mbona huyasemi haya? Kumbe mdogomtu alikuwa Balozi wetu Mexico wakati Pele anashinda World Cup 1970? Akawa balozi kwa Ben Bella na Sahrawi, wewe iwehe unasema ni "forgotten"? Umetumia mada hii adhimu kujinadi CV yako safari za majuu, uk9 tayari kusifia Wamanyema na Waislamu wa Kariakoo zaidi, madobi na wapiga mnada, wengine wote hadi Mexico vipi huwaoni? Nchi imeanza kubadilika sasa: tuna Rais Mzenj, tena Mwanamke, na tena ni Islamu. Hiyo Tanganyika yako ya AMNUT na Abduwaheed haipo tena. Majuzi ulimuona Askofu Mkuu akiongoza Ibada maziko ya Magufuli ule Chati? HighTable mbele ya Altare zaidi ya 90% walikuwa ni Waislamu - Rais na Jaji Mkuu wawiliwawili - na hata Mufti! Badilika Kaka, tunapendana asantenyerere!
 
Watu wanashindwa kutambua kuwa uwandishi ni sanaa kama sanaa nyingine mfano kuchora na kupiga tarumba

Umenikumbusha juzi kuna barua nilikuwa naandika CD wangu akaikataa eti kisa haina formality anayotaka yeye na sio kwamba office ina formality ya burua ni anataka anacho amini yeye kwenye kuandika

Kukariri ni kitu kibaya sana
 
Sheikh Mohamed Said: Eid Muvarak belates! Kile kitabu chako kizuri cha Abdulwaheed Sykes the Forgotten Struggle mbona huyasemi haya? Kumbe mdogomtu alikuwa Balozi wetu Mexico wakati Pele anashinda World Cup 1970? Akawa balozi kwa Ben Bella na Sahrawi, wewe iwehe unasema ni "forgotten"? Umetumia mada hii adhimu kujinadi CV yako safari za majuu, uk9 tayari kusifia Wamanyema na Waislamu wa Kariakoo zaidi, madobi na wapiga mnada, wengine wote hadi Mexico vipi huwaoni? Nchi imeanza kubadilika sasa: tuna Rais Mzenj, tena Mwanamke, na tena ni Islamu. Hiyo Tanganyika yako ya AMNUT na Abduwaheed haipo tena. Majuzi ulimuona Askofu Mkuu akiongoza Ibada maziko ya Magufuli ule Chati? HighTable mbele ya Altare zaidi ya 90% walikuwa ni Waislamu - Rais na Jaji Mkuu wawiliwawili - na hata Mufti! Badilika Kaka, tunapendana asantenyerere!
Najaribu kuelewa ulichoandika ila sijapata hata moja sijui ulitaka kusema nini ili kumaanisha kitugani maandishi yako hayaeleweki
 
Aah, wapi! Huyo Mohamed Said huwa anajua historia ya watu wasiozidi kumi; Abbas na Abdul Sykes, Dosa Aziz, Bibi Titi, Rupia na wengine wachache. Na hao wote ni wa Kariakoo mitaa ya Aggrey na Tandamti! Hajui kingine chochote zaidi ya hiyo mitaa!!!
Haya basi wewe tuletee historia ya watu wawili tu unaowajua wewe kutoka huko kwenu mahenge ili na wewe tupate kukusoma na pia kuwasoma hao wachimba udongo wenzio

Watanzania mtabadilika lini na mambo yenu ya kishamba na ya kizamani kujifanya mnakandia na kusagia vya watu wakati wewe huna hata vya kuponda wala vya kupapasa

Acheni ushamba
 
Najaribu kuelewa ulichoandika ila sijapata hata moja sijui ulitaka kusema nini ili kumaanisha kitugani maandishi yako hayaeleweki
Ewe Mnyamwezi wa Fundikira: nashukuru umekiri uelewa wako ni mdogo, nitakusaidia bure nami nilipata bure. Mosi, nilimtakia Sheikh Moh'd Eid el Faitr nami nikakiri nimechelewa.

Pili, nilimkumbusha kitabu chake kizuri kinaitwa "Abdulwaheed Sykes the Forgotten Struggle", ambamo aliwachachafya TANU eti kwa kudogosha mchango wa familIa ya Sykes (asili yao Wazulu kutoka Natal baba yao Mzee Mbokweni alikuja kama soldier wa Jarumani WW2). Ushakisoma hiki kitabu? Ninacho, tuwasiliane upenuni. Lazima uchukue kile cha Kiingreza, alijatoa translation ya Kiswahili akawa amekichakachua kile orijino. Mie ninavyo vyote Alhamdullilah nitakupa tukikutana Inshaallah.

Tatu, nikamsema kwamba amelalamika kina Sykes kutothaminiwa, ndipo hilo tangazo la CCM nikampa, likisema Sykes mdogo (Abbas, wa mwisho, walikuwa 3) kumbe alishapewa nafasi adhimu kuwa Balozi wa JMT nchi karibu 20 zikiwemo Mexico, Algeria, Ufaransa na Sahrawi. Maana yangu ni kuwa kumbe kina Sykes walithaminiwa, alichosema kitabuni kwake si kweli.

Aidha, nikaendelea kumkumbusha kuwa kile kitabu chake alijikita mno kusifia Waislamu, hususan wa Kariakoo khasa Wamanyema (sina hakika lakini sintoshangaa kama Shehe wetu ni Mmanyema wa Kariakoo) kana kwamba ni wao tu waliopigania uhuru wa Nji hii. Nikafafanua kuwa hii nayo si kweli, nikampa mfano wa Rais Samia na Waziri Mkuu na Mufti wetu na Mufti wa Zanzibar na Jaji Mkuu wa Zanzibar na Jaji Mkuu wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Makamo wake wawili, wote ni Waislamu walikuwa 70% ya frontbench kwenye Ibada ta Askofu kumzika Magufuli. Wakristo pekee walikuwa ni CDF Mabeyo na Supika Ndugai (ofkozi wangekuwa watatu lakini Dr Mpango alikuwa bado hajateuliwa).

Do you see my point?

Nikamwambia Sheikh anazeeka vibaya, bado ana kumbukumbu zama za AMNUT, Bantu Group na Mzee Ng'winamila wote Wanyamwezi wenzenu.

Niongeze kuwa BAKWATA kawasema vizuri kwenye kitabu chake (kile cha Kimombo, alipofanya translation akawageuka!) ambao kwa sasa wanakaa nafasi ya juu kabisa katika mshikamano wa Taifa letu baada ya novena ya pamoja kuombea tunusurike Corona. BAKWATA walichangia uhuru wa Nji hii walipokataa kurubuniwa na wadini eti wajitenge kama Pakistan ya India.

Mwisho, nikamkosoa kwa kujikita zaidi kutangaza CV yake badala ya CV ya marehemu, hili waliliona wachangiaji wengine bila shaka ukiwamo nawe.

Are we together?

Sasa rudi usome tena tuone kama utaelewa. Kama bado nitafute upenu nikupeleke IFM (shule ya Sheikh Mohamed!) tujajadili naye kwa faragha.
 
Marehemu na yule aliyekuwa meya wa Dar miaka ile ya 2000 mwanzoni ni ndugu wa tumbo moja?.

Hawa ni watoto wa kaka yake na Marehemu Ali Sykes mwenye nyumba kule baharini kabisa mbezi beach?.

Mtoto wa Ali Sykes kwa miaka mingi biashara yake imekuwa pale karibu na ilipokuwa mbowe hotels kama unaelekea ule msikiti wa mbele pale kwenye ile roundabout iliyo karibu na Hindu Mandal Hospital.

Mwaka 2001 tulianzisha umoja wa watu tulioishi mitaa ile ya ocean road mpaka posta mpya na yule meya ndio aliyekuwa mlezi wetu. Maisha yanakwenda kasi sana.
 
Nilikuwa Dubai, nilipigiwa simu na BBC kutaka kunihoji hapohapo nilikuwa Tanga nikifuatilia katika TV......


Visa vya kutunga tunga vina shida zake
Yuko sahihi labda wewe kama ulizaliwa 2000, kuugua kwa mwl. Nyerere ilichukua muda kidogo, na mazishi nayo yalichukua muda kudogo.kwahiyo inawezekana akawa Dubai, London na Tanga
 
"Mimi sikupata kujuana na Mwalimu lakini katika utafiti wangu wa maisha ya Abdul Sykes na harakati za uhuru nimemjua kwa karibu Mwalimu Nyerere kushinda wale waliokuja kuwa karibu na yeye baada ya uhuru.

Katika utafiti nimekutana na Mwalimu Nyerere ndani ya Nyaraka za Sykes na ndani ya nyaraka hizi nimesoma barua zake akiwa Rais wa TAA na kisha TANU katika miaka ya mwanzoni ya 1950, nimezungumza na Ally Sykes na Dossa Aziz na Mama Daisy (mke wa Abdul Sykes) watu waliokuwanae toka siku ya kwanza wanaanza mapambano ya kudai uhuru"

Kwanza nilitaka kuanza kuamini unayoandika. Nikagundua kuwa ingawa umeandika kwa vielelezo vingi, na reference ambazo ni questionable, lakini cha ajabu sana ingawa uwmeishi muda wote na Nyerere ( Nyerere living era, hata baada ya kustaafu); kumbe wala hujawahi hata kuongea naye. Umesimuliwa na watu, na watu uliosimuliwa nao ni wale wale ambao hata mie nitajiuliza mara nyingi je hawakuwa wanalalia upande mmoja yani bias. History ambayo ni changamoto na madai makali yako wala hukuuona kuna sababu hata ya kumsikiliza mlengwa mweneyese akuambie? Maana umeishi tangu TAA, TANU hadi CCM, kuna ulazima kumhoji mlengwa moja kwa moja ili tuone naye ana mawazo gani. Umeanza kumsema huyu mtu baada ya kufa.

Mbona wenzio akina Mtikila walimsema alipokuwa mzima? Kambona alirudi wala hakuhukumiwa. Wewe ambaye ulikuwa una compelling reason, kwa nini hukujitokeza uongee naye ujiridhishe? Hapo ndipo uongo hujitenga na ukweli.
 
Ningependa kukufahamisha kuwa sijamsema Nyerere.
TANU imeundwa mwaka wa 1954 mimi nina umri wa miaka miwili.

Kitabu changu kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Kitabu kimetoka mwaka wa 1998 na Nyerere aikuwa hai na kakisoma.

Kitabu hiki nimeandika baada ya kuona kuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981 si sawa.

Imesadifu kuwa historia hii ni historia ya wazee wangu kwa ajili hii nikaamua kufanya utafiti na kuandika historia ya TANU kama tunavyoifahamu sisi wajukuu na watoto wa hawa waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Nyerere ameingia katika historia hii kwa kuwa waliompokea na kumtia katika uongozi wa juu wa TAA ni watu wanaofahamika.

Halikadhalika waliounda TANU pia wanafahamika.
Bahati mbaya historia iliyoandikwa ikawa imewafuta.

Mimi nimewarejesha wote waliofutwa katika historia.
Hakika katika historia hii sikuwa na la kumuuliza Mwalimu Nyerere.

Nyaraka za Sykes zilinitosha kabisa achilia mbali kuwa babu yangu kashiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika toka enzi za TAA mwaka wa 1929.

Lakini nitakutoa shaka.

Mwaka wa 1968 Aisha "Daisy" Sykes alimhoji Nyerere mbele ya baba yake Abdul Sykes nyumbani kwa Mwalimu Msasani kuhusu TANU.

Mwalimu alimweleza Daisy kila kitu.
 
Unapoandika kitabu cha history, hasa cha kuongea history ya nchi siyo mchezo, lazima unafanywa utafiti mwingi na mpana, tunafunua vitabu vingi, tunakutana na watu wengi na tunahoji, na mifano. Kuna usemi kuwa ukiwa huna ushahidi basi usiseme. Research yoyote lazima ionyeshe reference, method/methodology uliyotumia. Baadaye unachambua qualitatively na quantitavely.

Hapo juu unasema ulikuwa huna haja ya kumwona Mwalimu kwa sababu hekaya za Sykes zinakutosha, je kwa nini hukugundua kuwa you want to convince people like me kuhusu hizo facts, ambazo zinatengeneza concept zima to perspective. Ungekuwa na hekaya za Sykes, Nyerere na uchanganye na wengine kama 6, ungekuja kwenye conclusion nzuri sana. Labda ndiyo maana hiki kitabu hakitumiwi mashuleni, kwa sababu wewe umekuwa impartial. Kitabu ambacho kingeweka wazi majibu ya maswali mengi mno. Kwa hiyo hata suala la kuwa ulifanya urejeshaji wa kilichofutwa inabaki kuwa hypothesis, hujahakikisha. Na kama kuna watu wamehakikisha basi ni wale tu wa mlengo wako. Unafurahishwa kuandika kile ambacho kinakupendeza siyo matokeo halisi ya utafiti.

Aisha "Daisy" Sykes hata kama ni mmoja wa shaidi wako au source, unategemea atasemaje kuhusu Nyerere?

Labda challenge iliyopo ni hivi, mengi hayakuandikwa kutokana ya ufinyu wa tafiti ya historia yetu, wengi mno walifanya mchango kwa ukombozi ulioanza tangu zama za Mkwaw na Wajerumani, Kinjekitile na Wajerumani, huo wako ni muendelezo tu. We need to add more in our history books.
 
Kitabu nilichoandikia si "hekaya," kama ulivyosema.
Lakini umekiita hivyo kwa kuwa umeghadhibika.

Hujapenda kuwa mimi niandike haya nilliyoandika.
Walioandika hekaya ni Chuo Cha CCM Kivukoni.

Historia ya TANU kuundwa kwake wakaiegemeza sipo.
Historia hii imekuwapo kuanzia uhuru 1961 hadi 1998 kilipochapwa kitabu changu.

Wewe ndugu yangu miaka yote hiyo umekuwa kimya wala hukuwaambia Kivukoni iweje waandike historia ya TANU hawajasoma Nyaraka za Sykes?

Chepesi kwako wewe ni kuja na "hekaya."
Au hukuwa unajua kuwa Kleist Sykes ndiye katibu muasisi wa African Association mwaka wa 1929?

Au hukuwa unajua kuwa wanae wote Abdulwahid, Ally na Abbas wote kwa pamoja walishiriki katika kuiasisi TANU?

Ally kadi yake ya TANU No. 2 Abdul No. 3 na Abbas No. 7.
Ulitaka haya nikamuulize Nyerere ilhali hawa mimi ni baba zangu na najua yote waliyofanya?

Kitabu changu kilipotoka kilishtua wasomi mabingwa wa historia ya Afrika na katika hawa watatu walikifanyia review: John Iliffe, Jonathan Glassman na James Brennan na hizi review zipo katika Cambridge Journal of African History.

Haya ni mambo yaliyofanyika miaka 23 iliyopita.
Nashangaa wewe unaamka leo kutaka tujadili.

Prof. Haroub Othman yeye alinikabili mimi kutafuta ukweli wa kitabu changu na akaenda pia kwa Nyerere kupata yakini ya maneno yangu.

Hofu yake alimwambia Nyerere ni "legacy," yake katika kuunda TANU.
Mbona hakupata kumtaja Abdul?

Kisha akaenda kwa Ahmed Rashad Ali rafiki kipenzi wa Abdul Sykes kuuliza maswali yake.

Prof. Haroub aliingiwa na simanzi.

Rashad alimwambia Prof. asishangazwe na Abdul kuunda TANU mwaka wa 1954 ashangazwe pia na baba yake kuunda African Association mwaka wa 1929.

Mimi nimeandika historia yangu.
Yangu kwa maana nimeandika historia ya baba na babu zangu, historia ya wajomba na shangazi zangu.

Nyerere ameingia katika historia hii kwa kuwa katika maisha yake alipata kuishi na wazee wangu hapa Dar es Salaam na wakapigania uhuru wa Tanganyika pamoja.
 
Samahani sana, hekaya nilimaanisha simulizi wala siyo kudharau kitabu chako, ni neno ambalo nilifikiri lingetumika kama vile "story". Kumbe hekaya siyo neno zuri?
 
Tangulia, hiyo ni safari ya wote ila huwa ni suala la muda tu.
 
Marehemu na yule aliyekuwa meya wa Dar miaka ile ya 2000 mwanzoni ni ndugu wa tumbo moja?.

Hawa ni watoto wa kaka yake na Marehemu Ali Sykes mwenye nyumba kule baharini kabisa mbezi beach?.

Mtoto wa Ali Sykes kwa miaka mingi biashara yake imekuwa pale karibu na ilipokuwa mbowe hotels kama unaelekea ule msikiti wa mbele pale kwenye ile roundabout iliyo karibu na Hindu Mandal Hospital.

Mwaka 2001 tulianzisha umoja wa watu tulioishi mitaa ile ya ocean road mpaka posta mpya na yule meya ndio aliyekuwa mlezi wetu. Maisha yanakwenda kasi sana.
Ngoja ntoke nje ya mada hii!
Nkuulize kitu..unamkumbuka/unampata songoro

Ova
 
Unamvika sifa isiyo yake,Shekh Said ni mtu wa kujisifu na kuwasifu watu wa deen yake.

Akikusimulia kuhusu Mwl Nyerere robo tatu ya simulizi zitahusu Wazee wake wa Kariakoo.Robo nyingine zitahusu mihadhara yake yeye halafu page mbili za mwisho atamtia Mwl Nyerere kiduchu.
Ngongo,
Umesema kweli kabisa.
Imenichukua muda kidogo kuweza kuipata staili hii ya uandishi na wengi wanaipenda.

Lakini kama wasemavyo Waingereza, ''One man's meat is another man's poison.''
Hili la kujisifu inawezekana nikawa nalo katika baadhi ya hali na nyakati.

Unajua mimi jina langu na huu Uswahili wangu na kalamu yangu hunikaribishia matatizo mtu akaja kwa nia ya kutaka kunifedhehesha atajitahidi kuandika na kujaza Kiingereza kama kutaka kunitisha vile.

Basi mimi nitamwambia ndugu yangu hebu kuwa na subra mimi nina First Class English Oral Cambridge Exams.
Hapa kidogo anatulia.

Hufanya mfano wa haya sana lakini mpaka nikimuona huyu mtu hana adabu kwangu.

Hili la kuwasifu Waislam hakika nimelifanya na nimewaandikia kitabu kizima kueleza mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sababu ya kufanya hivi ilikuwa kurejesha heshima yao iliyotaka kuporwa.

Ndiyo nikaandika kitabu ambacho kimekuwa maarufu: ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.''

Yote uliyosema kuhusu mimi kwa hakika ninayo ingawa mengine ni kwa kiasi kidogo.
 
Back
Top Bottom