Buriani Amina Chifupa!

Buriani Amina Chifupa!

Status
Not open for further replies.
PM yuko dodoma kwa ajili ya kupitisha fedha za kujitajirisha, amemtuma waziri wa nchi masuala ya Bunge akamwakilishe, hii kali kuwakilishwa MSIBANI!! Huyu Shein naona at least ndio kivuli chao yaani atawawakilisha ingawa sijawahi kusikia mtu akiwakilishwa msibani!!!
 
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Kwa hakika cha kupita lazima kipishwe kwa hali zote na hata kisipopishwa kipite kitapita tu.Hivyo basi mambo yote yanayomtokea mwanadamu tayari yameshaandikwa katika madaftari na kwa hakika kalamu zimenyanyuliwa na sahifa zimekauka. Yote yanayotokea hutokea kwa Kudra ya Allah Subhanahu Wa Ta'ala hivyo basi mja mwema anapaswa kuwa na subira na matumaini. Sisi Waislamu tunapaswa kutokata tamaa kwa kuwa Makafiri tu ndio hukata tamaa. Mawazo mengi yataongeza msiba na majonzi hivyo basi tusimame kidete na kujitia motisha kwamba Inshaa-Allah mambo yatakuwa mazuri kwa siku zitakazokuja.Pia, tanabahi yakwamba yale yote yamekukumba yamewakumba wengine waliokuwa kabla yako na yatawakumba wajao kwa hivyo usirushe mikono hewani kisha ukashika tama na kuwaza mawazo yasokuwa na kipimo.Allah (S.W.T) lazima atufanyie mitihani ili azitikise imani zetu.Kitu kingine muhimu cha kujua ni kwamba sote tuko katika bahari ya mitihani inayotoka kwa Allah (S.W.T).Hivyo basi kwake tumtegemee na tumpe shukrani na tumwabudu kwa dhati kwa kujikurubisha kwake kwa kumhimidi,kumsabihi na kumtakabiri ili atulipe hapa duniani na kesho akheri. Tunamwomba Allah (S.W.T) atulinde na mitihani migumu na atuimarishie imani zetu na atulipe na mema hapa duniani na kesho akhera na atuepushie adhabu ya kaburi na moto.Amin!
 
Jasusi,
Eeeeh kumbe EN atakuwepo Dar?.... haaya nasubiri kusikia hilo vagi!
 
Siku zimeshapita na mambo yake yameshatoweka, hutonufaika kitu kwa kuendelea kubeba uchunguzi wa maiti kwa kurudisha magurudumu ya historia.



Anayerudi katika hali ya maisha ya nyuma, ni kama mtu anayekanda unga ambao umeshakandwa mwanzoni na ni kama anayechonga unga wa mbao kwa msumeno. Wamesema watu wa kale: "Usimtoe maiti kaburini".



Msiba wetu ni kutokuweza kupambana na wakati tulionao,Wangelijumuika watu na majini kurudisha yaliyopita hakika wangelifeli. Watu hawapaswi kuangalia ya nyuma wala kuangaza yaliyowapita, kwa sababu upepo unaelekea mbele na maji yanatiririka mbele, na msafara unaelekea mbele, basi usiende kinyume na desturi ya maisha!
 
tunachohitaji kujua ni nini kimemuua huyu binti, suala si kutafuta nani mchawi
 
Raia,
Tukumbuke hotuba ya Mwisho ya binti huyu akiwa Mbunge kuhusu swala la Bwimbwi!...

Alisema:-
"Nafahamu ninapambana na watu hatari, lakini kesho (leo) namuomba Mwenyezi Mungu aniamshe salama, ili niweze kuliweka bayana suala hili mbele ya waandishi wa habari MAELEZO. Nimekusudia kusema ukweli wote kuhusu suala langu," alisema Amina.

"Daima nasimamia ukweli na sababu ya dhamira yangu. Nipo tayari kufungwa au kuchukuliwa hatua yoyote iwapo nitaonekana sina nidhamu... hata ikibidi kupoteza ubunge na uanachama wangu wa CCM. Mimi si mwanasiasa wa 'ndiyo mzee'," alisema Amina baada ya kuulizwa iwapo ukweli anaotaka kusema hautamgharimu.

Toka siku hiyo maisha ya AC hayakuwa tena salama!....Hakpupewa nafasi wala ruksa ya kuyataja majina ya wahusika ila kuyawasilisha kwa rais!...Na hata alipotaka kusafisha jina lake ktk janga la ndoa,pia alizuiwa kwa kupitia baba yake....
watanzania tumebaki kizani kwani shahidi wa Wananchi kisha tutoka na hakuna mwenye ukweli ila mwenyezi Mungu. Bi. AC alikuwa kichaa kabisa siku zake za mwisho! kapagawa kama vile mtu aliyekuwa na shetani..
Hapo Bongo hadi sasa naambiwa kuwa huo msafara wa mazishi yake ambao unaendelea hadi sasa hivi ni mkubwa kuliko yote iliyowahi kutokea tukiacha wa baba wa Taifa marehemu mwl. Nyerere.
 
Hatutafuti mchawi hayo ni mambo ya ushirikina! tunachotaka kutaka kujua na kuzuia kutokea tena ni nani amehusika ama sivyo, watu wataogopa kuitetea nchi hii kwa sababu orodha yao itazidi kuongezeka... ! Kama kuna mchezo mbaya ni lazima tujue nani alifanya nini kwani tukikubali kukaa kimya na kusema ni "mapenzi ya Mungu".. tutaendelea kupukutika hivi hivi! Kama hakuna mchezo mbaya serikali haina cha kupoteza, ila wakikataa kuruhusu uchunguzi huru ni wao watakaozidi kupoteza imani ya watu na kuwafanya watu waanze kujaa madoa ya shaka ndani ya mioyo yao.
 
I bid farewell to you my friends
For my stay with you here ends
I came with a purpose
I came with reasons

Now I wish you all well for all the coming seasons
My departure was sudden
Because it was my hour and fate
I had a merry time with many of you
Before the divine power opened its gate

As I leave you for my final abode
I truly know how blessed I was
For all the love I was shown
A new family in you all I have known

Do not weep for me
For it would hurt my soul
But if you think of me any time
Wear a smile with my thoughts
Because that is how I wish to be remembered
Long after I am gone.


AMEN! AMEN!
 
Sikumaanisha kuwa nani kamroga na kadhalika, hapa tunahitaji ukweli wa jambo hili, nani hasa kahusika na kifo hiki kwa sababu statement za huyu binti zilikuwa na uzito ndani yake ikiwemo ile ya kumuomba mungu amuamshe salama ili atoe dukuduku lake na kuueleza umma wa watanzania na ulimwengu alichokuwa anakiamini yeye. Bahati mbaya baba yake mzazi akamzuia na mpaka kifo cha binti huyu hakuna anayejua alitaka kusema nini, labda baba yake au familia inaelewa fika jambo hili.
Rest in Eternal Peace Amina.
 
Tangulia Amina!
Tangulia kamanda!
Kalale pema peponi.
Amina.


...hakika serikali iangalie watu wasipoteze imani nayo...

Angalizo:
Nimezoea kusikia "...Bush administration...", au "...Blair administration...", na "...Iranian regime...", au "...Mugabe's regime...".

Sasa nimeshangaa na kushtuka kusoma mahali "Kikwete regime"!

Inawezekana tunaelekea kubaya ndiyo maana baadhi ya wazungumzaji wameanza kuitaja serikali kwa kutumia neno hilo "regime"?
 
Siku zimeshapita na mambo yake yameshatoweka, hutonufaika kitu kwa kuendelea kubeba uchunguzi wa maiti kwa kurudisha magurudumu ya historia.



Anayerudi katika hali ya maisha ya nyuma, ni kama mtu anayekanda unga ambao umeshakandwa mwanzoni na ni kama anayechonga unga wa mbao kwa msumeno. Wamesema watu wa kale: "Usimtoe maiti kaburini".



Msiba wetu ni kutokuweza kupambana na wakati tulionao,Wangelijumuika watu na majini kurudisha yaliyopita hakika wangelifeli. Watu hawapaswi kuangalia ya nyuma wala kuangaza yaliyowapita, kwa sababu upepo unaelekea mbele na maji yanatiririka mbele, na msafara unaelekea mbele, basi usiende kinyume na desturi ya maisha!

Kwahiyo somo la HISTORIA halina umuhimu kwako?Au tuseme hata wanaoadhimisha siku zao za kuzaliwa ni wapuuzi (coz walizaliwa in the past)?

Usipoangalia ulipojikwaa una uhakika gani kuwa in your next step hutajikwaa tena na kuvunjika mguu?The past is as important as the present and the future.Binadamu sio vipepeo (kwa kunukuu busara za Mwanakijiji) ambao wanafyonza ua then muda mfupi baadae wanarejea kwenye ua hilohilo wakisahau kuwa walishalivyonza kabisa.

Pamoja na kutoa rambirambi,namna bora ya kjaribu kuzuia possibility ya "wasemaji wa umma" (eg Sokoine,Katabalo,na sasa AC) kunyamazishwa na "nguvu za giza" ni kuwasuta hao tunaohisi kuwa katika tamaa zao za madaraka na kuthamini matumbo yao na nyumba ndogo zao wako tayari kutoa roho za binadamu wenzao.Tunapaswa kukumbuka maneno ya AC mwenyewe kuwa maisha yake yalikuwa hatarini baada ya kuanzisha vita yake dhidi ya wauza unga.Hivi jamani,kama mtu ametamka bayana kuwa anadhani kuna wanaowinda roho yake then hicho alichosema kinatokea,bado tutaendelea kudai kuwa tuachane na past?
 
nnazani kunisoma vyema , kuna mambo nnayamaanisha hapo na ambayo kuyapigania sana hayatusaidiii na hilo hasa ndio lenggo la post yangu hapo juu

you cant have a better tomorrow if you are thinking about yesterday every time
 
mtumwitu, ungependa uchunguzi huru ufanyike ili kujua ni nini kilichojiri, au wewe ikishatoka imetoka ikirudi pancha!?
 
jk, ccm, nchimbi and the mob ( na kuna wengi zaidi ya hawa wanaotajwa hapa ) nani aliyeshughulikia kila kitu, wanakamati wa mpango wa kumuua dada yetu, wachawi wao etc watajwe.
 
Mimi ni muumini wa dini na natambua kuwa kama waja wa Mola hatuna nafasi ya kupingana na matakwa yake.

Lakini kuna wakati niliwahi kumsikia mwanafalsafa flani wa "siasa za mtaani" aliyesema kuwa kulia na kuomboleza peke yake pasipo kutafuta namna ya kuzuia vilio na maombolezo zaidi sio jambo la busara.Aliendelea kusema kuwa wanadamu tuna silika tofauti,na ni ukweli usiopingika kwamba wapo wanaoishi kwa kukanyaga wenzao migongoni na hata kuwapeleka kaburini ili wao wafikie matakwa yao.Kuna nyakati ambapo watu wanafikia hatua ya kumlaumu Muumba wao kwa kuwanyima mvua.Wasichojua ni kwamba Muumba analeta mvua ila wajanja "wanaidaka juu kwa juu."Hiyo ni sawa na nchi wahisani zinavyomwaga misaada lakini wajanja "wanailia denge" kabla haijawafikia walengwa.

Kwa mantiki hiyo,wakati tunakubaliana kuwa kwa vyovyote ilivyo kifo cha Amina ni kwa mapenzi yake Mola,hatupaswi kuishia kuomboleza tu pasipo kufanya "vijishinikizo" vya hapa na pale kuzuia vilio na maombolezo mengine.Kuna watu kama akina Dr Slaa ambao wanatumia kila nguvu waliyonayo kuanika maovu hadharani,kuna akina Anna Kilango wanaowaomba majambazi wa uchumi wetu wawe na huruma kwa Watanzania wenzao,na kuna wengine wengi wanaopiga kelele kwa maslahi ya watanzania wenzao.Hawa hawana ulinzi,na kwa vyovyote vile wanajiingiza kwenye orodha ya wawindwa wa hao majambazi wa uchumi wetu.Only way we can be of help to them (watetezi wetu) ni kuwaweka hadharani wale wote tunaoamini kuwa wako tayari hata ku-emport Polonium-210 kulinda maslahi yao.

Kulia na kisha kusahau kilichotuliza hakutasaidia kutolia tena in the future.The evil forces are still there,so let's join hands to expose them
 
Yatosha tukimuombea maisha mema akhera!! ya dk Nchimbi tuyaache!!!
 
mimi nimepitwa kidogo ila nataka kulekebisha hapa,
""Daima nasimamia ukweli na sababu ya dhamira yangu. Nipo tayari kufungwa au kuchukuliwa hatua yoyote iwapo nitaonekana sina nidhamu... hata ikibidi kupoteza ubunge na uanachama wangu wa CCM. Mimi si mwanasiasa wa 'ndiyo mzee'," alisema Amina baada ya kuulizwa iwapo ukweli anaotaka kusema hautamgharimu.""

Maneno haya Amina aliayasema wakati yupo kkwenye kipindi redio kwamba kesho yake atalipua bomu kwamb kigogo gani ndio amesababisha kuvunjika kwa ndoa yake.
Sasa inatia shaka kama huyo kigogo aliye kua kichwani kwa Amina at the time ndio amechangia kwenye kifo chake!?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom