Siku zimeshapita na mambo yake yameshatoweka, hutonufaika kitu kwa kuendelea kubeba uchunguzi wa maiti kwa kurudisha magurudumu ya historia.
Anayerudi katika hali ya maisha ya nyuma, ni kama mtu anayekanda unga ambao umeshakandwa mwanzoni na ni kama anayechonga unga wa mbao kwa msumeno. Wamesema watu wa kale: "Usimtoe maiti kaburini".
Msiba wetu ni kutokuweza kupambana na wakati tulionao,Wangelijumuika watu na majini kurudisha yaliyopita hakika wangelifeli. Watu hawapaswi kuangalia ya nyuma wala kuangaza yaliyowapita, kwa sababu upepo unaelekea mbele na maji yanatiririka mbele, na msafara unaelekea mbele, basi usiende kinyume na desturi ya maisha!