Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Ni hivi hakuna kitu muhimu kwa mwanadamu na Serikali kama kujua falsafa uliyoiamini na kuifata.

Kuna falsafa ya Mungu na Falsafa za Wanadamu.

Kazi moja kubwa ya falsafa za Wanadamu ni kugawa jamii ktk makundi makuu mawili.

1. Binadamu aliyekamilika.
2. Binadamu nusu.

Binadamu aliyekamilika wanafalsafa wanasema ndiye anaepaswa kuwa kiongozi.

Na binadamu nusu ni yule mtawaliwa.

Kwa uoni wangu hali ya waislam tokea Uhuru na sasa matokeo ya kukumbatia falsafa ya ujamaa na itikadi ya Usekyula bila kujua madhara yatayayowakuta.

Ninyi ni watawaliwa na ndio kwa maana mko mnakimbilia siti za nyuma ktk bus.

Ujamaa ni imani kama zilivyo imani nyengine. Ujamaa ni imani isiyoamini uwepo wa Mungu. Na Usekyula ni kujitenga serikali na dini.

Tunahitaji kuwa na Falsafa mpya ya nchi.

Falsafa na itikadi itakayounganisha imani ya uwepo wa Mungu na kuheshimu haki za kila mtu wakiwemo wenye imani za dini.

Na kwamba hakuna anayefaidika au kupungukiwa kwa sababu ya imani yake.

Ujamaa ni Kielezo tosha kuwa ni Vikwazo kwa waislam. Na Serikali ya Ujamaa ni kandamizi na ingawa kuna sheria ndogo za serikali za mitaa inayokataza bucha za nguruwe kuwa karibu na makazi ya watu kama ilivyo kwa baa na kumbi za starehe lkn Serikali za kijamaa hufanya Upendeleo kwa vikundi vya kidini mojawapo?!

2. Na hutunga Sheria na sera zinazozuia uhuru wa kidini kwa wengine!???!

3. Serikali za kijamaa zinawawekea mipaka ya kuafuamini kwa kidini?!?!

4. Na kunyanyasa kwa vikundi vya kidini.

Kuandika historia hii ni hatua moja. Lkn inapotokea wanachama wa CHADEMA wanaungana na vyama vya Kijamaa (CCM na ACT) ktk sakata hili in wazi waislam watahitaji chama kingine kitakachotunza utamaduni, mila na desturi za kila jamii. Ili pale mtz anapoamua kwenda kuishi ktk jamii yenye utamaduni, na mila tofauti na za kwake. Aziheshimu.

Hili ndilo tatizo lililopo kwa tz kwa sasa.

Pale jamii za wachungaji wanapokuja kwa Waswahili na kuwatawala na kutaka kuwalazimisha tamaduni za watu wa mufindi na arusha na mbeya kulala na nguruwe ktk zizi moja wanadhani watu wenye ustaarabu na huo watavumilia.

Na suluhisho ya mambo haya ni tuje na chama kipya kitakachokuja na falsafa mpya. Falsafa ya serikali ya shirikisho.

Kila kanda iwe na serikali iliyo na mamlaka zaidi ya kujiamulia mambo yao wenyewe.

Ukienda arusha hutoshangaa kuona mabucha kila baada ya nyumba 10. Huo in utamaduni wao. Tusiwalazimishe kubadili. Kama vile mufindi nguruwe zinazurura kama mbuzi. Huo ni utamaduni wao.

Lakini wanapokuja ktk mini yenye ustaarabu tofauti wasitake kulazimisha.
Wanapaswa kukubaliana na utamaduni wao.
 
SSasa
KII,
Mimi utaalamu wangu uko katika historia ya Uislam.
Hii ndiyo sababu kila unaposoma utawasoma.

Labda ungeniuliza kwa nini nimesoma somo hili?
Sababu ni kuwa wanahistoria wetu walipuuza historia ya Waislam kiasi yote ilifutika.

Mimi nikaamua kutafiti na kuiandika.
Ikiwa wewe unakereka na hili acha tu kusoma post zangu.
Sasa huko london frankfurt unafwata nini kwà wakristo si ukaishi maka madina na jeda
 
Tanzania ina Waislamu wa ajabu sana. Nakiri mimi ni Mkristu ila nimebahatika kutembea vya kutosha kwenye nchi za Kiislamu kama Malaysia, Indonesia, Dubai, Iran, Abu Dhabi, Sudan na Turkey.

Nakiri kuwa nimewahi kula nyama ya nguruwe kwenye hoteli za 5 Star nchini Dubai, Malaysia na Turkey. Ni aibu kwa Waislamu wa Tanzania kuanzisha vurugu sababu ya mboga.

Sasa huyu marehemu Hassan Chikusa pengine kwa kupoteza kazi NBC sababu ya ujinga wa kuvunja mabucha kunaweza kukawa kulimuathiri kwa kipato na akashindwa kulea familia yake vizuri including kiwapa elimu wanae.

Lesson Learnt:
Muislamu usile nyama ya nguruwe kwa vile ni haramu period, lakini usihangaike na Wala nguruwe na mali zao.
Kuna utofauti baina kufanya kitu public na private, huko ulipotembelea kitimoto kipo ila hawauzi public na pia hawawauzii waisilamu bila wao kujua.

Sikuwa na fahamu kipindi hicho cha mabucha, ila kuchanganya nyama na kuwauzia waisilamu kitimoto bila ufahamu wao si jambo la kistaarabu hata kama wewe ni mkristo unatakiwa ulikemee.

Kama kuna demand ya mabucha ya Nguruwe yawe ni ya nguruwe na yatambulike ili musilamu ayaepuke.
 
Kwa mfano J K Nyerere alikuwa ni Mkatoliki safi lakini kwenye suala la Palestine alikuwa ni supporter kuhusu wao kuwa na nchi yao dhidi ya uvamizi wa Israel. Ndiyo maana akawapa na ruksa ya kufungua UBALOZI Tanzania
Palestina si Nchi ya kiisilamu, huwa nashangaa sana wabongo wanaodhani Palestina kule wanaoteswa ni waisilamu tu. Kuna mapadri kibao na wao wanakula kisago, huyu mwandishi wa juzi aliekuwa assasinated pia si muisilamu.
 
Kuna utofauti baina kufanya kitu public na private, huko ulipotembelea kitimoto kipo ila hawauzi public na pia hawawauzii waisilamu bila wao kujua.

Sikuwa na fahamu kipindi hicho cha mabucha, ila kuchanganya nyama na kuwauzia waisilamu kitimoto bila ufahamu wao si jambo la kistaarabu hata kama wewe ni mkristo unatakiwa ulikemee.

Kama kuna demand ya mabucha ya Nguruwe yawe ni ya nguruwe na yatambulike ili musilamu ayaepuke.
Sizani kama kutakuwa na ukweli unaposema "wanawauzia waislam bila kujua"

Madai hayo yangekuwa ya ukweli endapo zingevunjwa bucha zote lakini mtoa mada amesema kuvunjwa kwa mabucha ya kitimoto.

Kwa tafsiri hiyo ni kwamba mabucha hayo yalikuwa targeted na yanafahamika kuwa yanauza kitimoto.
 
Sizani kama kutakuwa na ukweli unaposema "wanawauzia waislam bila kujua"

Madai hayo yangekuwa ya ukweli endapo zingevunjwa bucha zote lakini mtoa mada amesema kuvunjwa kwa mabucha ya kitimoto.

Kwa tafsiri hiyo ni kwamba mabucha hayo yalikuwa targeted na yanafahamika kuwa yanauza kitimoto.
Nimetoa kwenye uzi wa mzee

Kilichotokea ni kuwa kijana alitumwa nyama na muuza nyama pengine kwa kutokujua akamuuzia huyu kijana nyama ya nguruwe.

S
ababu ya fujo ni ni mtu katumwa nyama ya kawaida akapewa kitimoto. Hapa inawezekana ikawa bahati mbaya ama kimakusudi mfanya biashara hakuwa mwaminifu labda alikuwa nayo nyingi nyama ya nguruwe akamchomekea.
 
Viongozi walitupa lawama kwengine na kusema kuwa waliovunja mabucha nia yao ilikuwa kupindua serikali.

Je, huoni kuwa hapo yapo mengi ya kujifunza?
Kifupi waislamu wavunja mabucha ya nguruwe walikuwa waislamu wachache ulilinganisha na idadi ya waislamu wala nguruwe

Ndio maana ile agenda ilipinga kuanzia na viongozi waislamu wakalaumiwa wavunja mabucha ya nguruwe

Ni sawa na leo waislamu wachache waseme tunavunja baa zote upinzani wataupata kuanzia kwa viongozi wa Serikali waislamu wenzao

Kifupi dini hailazimishwi mtu anatakiwa adhibiti nafsi yake na matamanio

Ndio maana kwenye Ukristo kufunga siku 40 na hoteli hawafungi wanakuuzia chakula bila shida

Kwa waislamu hawawezi kudhibiti matamanio ya mioyo yao ndio maana huvunja mabucha ya nguruwe, kupiga wanawake wavaa nusu uchi na kuweka sheria kali mwezi wa Ramadhani kuwa marufuku mtu kula hadharani anawapa matamanio wengine

Kifupi waislamu walio wengi hawana uwezo wa kudhibiti matamanio yao kama wakristo!! Ndio maana huhitaji sharia kali za Serikali kudhibiti matamanio yao!!! Ikiwemo kutaka.mabucha ya nguruwe yavunjwe sababu udenda unawatoka wa matamanio wakiona nyama ya nguruwe iwe buchan au inapikwa
 
Daah moyo wangu huumia sana napopata historia juu ya maonevu wanayoyapitia waislamu hapa nchini.Ndani ya Tanzania waislamu ndiyo jamii pekeee iliyoumizwa Mara nyingi zaidi huku wakiwa dhariri na hakuna wa kuwatetea.
Inferiority complex jumlisha na ujinga ndio vinavyowasumbua...kwa akili ya kawaida unaenda vunja biashara za watu katika nchi ambayo ni non secular huo sio upunguani na kuukosa akili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mambo ya kutengeneza haya. Ndyo maana hao ma mujahedeen yakakamatwa yote na kuswekwa ndani sababu chanzo cha fujo ni feki: haiwezekani muuza nyama ya ng'ombe na mbuzi akupe nyama ya nguruwe. Ni uwongo. Kwanza nyama ya ngururwe ina bucha zake tofauti na nyama nyingine.
 
Kitimoto mara nyingi zipo pub. Na zimetengewa eneo lake maalum mbali na jiko kuu. Hakuna sehemu: bucha au jiko, inayochanganya nguruwe, ng'ombe, mbuzi , samaki, kuku etc.
 
Mbona habari haieleweki,nileo hii nimekula kilo nzoma na ndizi 2 hapo hapo manzese,tena sio mara moja,kitimoto saafi kabisa,hawa jamaa walinitembeleaga nyumbani wakakuta nimechinja mbuzi wangu eti wakagoma kula,niliwalisha haragwe wiki nzima,japo wengine niwateja wazuri tu wa kiti moto.
 
Hui...
Nimewasilisha mada nzima Kenyatta University kuhusu sakata la kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.

Mimi ukiniulliza kwa nini hili lilitokea nitakwambia kuwa serikali ililishughulikia vibaya tatizo hili.

Watendaji walikosa busara.
Wewe kila mara ukibanwa unakuja na haya majigambo yako ulialikwa chuo fulani Ughaibuni, lakini ujue wewe upo upande mmoja tu wa Story. Hao wanaokualika huko wanaalika Wasomi wengine wenye alternative views and theories, halafu wanaaacha audience ku balance na kung'amua ukweli upo wapi. Kwahiyo usijidai kwamba umealikwa vyuo kadhaa wa kadhaa Ughaibuni, wewe hao wanaokualika tayari wanajua upo upande gani, plus na sisi tunajua wewe ni Islamic activist ,and intellectual objectivity isn't your forte.
 
Ndo maana uighur mnadokolewa vichwa , acheni mambo ya ajabu.

Religion Is the opium of the mind.
 
Loyol...
Maswali kama haya si lazima nijibu mimi unaweza hata wewe mwenyewe kufanya utafiti utapata majibu unayoyatafuta.

Wajomba zangu wawili Sheikh Pazi na Shomari Lupindo wakiishi Manzese kwa miaka mingi toka mimi ni mtoto na sasa nina miaka 70.

Kwa hiyo naijua Manzese vizuri sana.
Nimezaliwa Dar es Salaam.
Wewe si umefanya utafiti wako wa undani zaidi wa ule wa Polisi, hadi ukaitwa Chuo Kikuu kutoa lecture? Basi mtaje huyo kijana wa Kiislamu, jina la bucha aliyouziwa nyama ya nguruwe badala ya ng'ombe/mbuzi, siku, saa na mazingira yaliyojiri hadi kupelekea kuchukua nyama ya nguruwe badala ya ng'ombe/mbuzi?
 
Back
Top Bottom