Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

BURIANI HASSAN CHIKUSA MSOMI MKIMYA
Naamini si wengi wanamfahamu Hassan Chikusa na yote yaliyomsibu katika maisha yake.

Mimi nilimjua Hassan Chikusa kwa kuwa alikua jirani yangu akiishi kwa ndugu yake Masaki jirani na nyumba niliyokuwa naishi mimi na familia yangu.

Wakati ule alikuwa kijana mdogo ndiyo kwanza amemaliza masomo yake na anafanya kazi Makao Makuu National Bank of Commerce (NBC), Sokoine Drive.

Tulizoeana sana na wakati mwingine akija nyumbani kwa mazungumzo na akipenda mazungumzo yangu katika vitabu, historia na muziki kama ilivyo kawaida ya vijana.

Hassan alikuwa akiweka shajara yaani akiandika, ''diary.''

Hassan alikuwa kijana akiipenda dini yake sana kwa mapenzi makubwa.
Mwaka wa 1993 pakawa na sakata la uvunjaji mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe Wilaya ya Kinondoni baada ya sala ya Ijumaa.

Kilichotokea ni kuwa kijana alitumwa nyama na muuza nyama pengine kwa kutokujua akamuuzia huyu kijana nyama ya nguruwe.

Palikuwa na malalamiko kuhusu haya mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe lakini walioshika madaraka hawakujali wala kutia maanani malalamiko ya Waislam.

Mjini Dar es Salaam kulikuwa na mabucha 29 ya kuuza nyama ya nguruwe kwenye sehemu wanazoishi Waislam na hii ilikuwa kinyume cha sheria.

Tatizo hili Waislam wakalifikisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mustafa Nyang;anyi lakini hakuna kilichofanyika na likafikishwa pia kwa Waziri Mkuu, John Samuel Malacela.

Waswahili wanamsemo wanasema yale yalikuwa sawa na kutwanga maji katika kinu.

Hili tatizo la mabucha likashushwa chini hadi kwa Mkuu wa Wilaya, Wilson Mkama na yeye akawaita ofisini kwake maimamu wa misikiti mitano ya Wilaya ya Kinondoni kwa mazungumzo.

Serikali haikuwa tayari kufunga mabucha hayo kwa kile walichokiona ni shinikizo kutoka kwa Waislam wenye, ''siasa kali.''

Bwana Mkama akawaeleza maimam kuwa hayo mabucha yapo kihalali na wana leseni walizopewa na serikali kufanya biashara hiyo kwa ajili hii serikali ina dhima ya kuzilinda hizo bucha.

Mkutano ukamalizika na maimamu wakarejea misikitini kwao kuwaeleza Waislam kauli ya serikali kuhusu mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Waingereza wana msemo, ''The straw which broke the camel's back,'' yaani ujani uliowekwa juu ya mgongo wa ngamia ukauvunja.

Waislam walighadhibika sana kwa uamuzi wa serikali kuwapuuza.
Siku ya pili ilikuwa Ijumaa Kuu.

Baada ya sala ya Ijumaa vijana wa Kiislam walipomaliza sala waliziendea zile bucha zilizokuwa Wilaya ya Kinondoni wakazivunja zote kwa mpigo.

Dar es Salaam ilizizima.
Haya hayakupata kutokea katika kipindi chote cha uhuru.

Rais Ali Hassan Mwinyi akiwa Zanzibar akasema katika kulani kuvunjwa mabucha ya nguruwe kuwa nguvu za dola ziwaangukie wale waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Jioni yake BBC hwakuchelewa wakafanya mahojiano na Waziri Mkuu John Samuel Malecela.

Malecela akasema kuwa waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe ni wahuni wanotaka kuchukua serikali kupitia dini.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu Augustine Mrema yeye akasema mabucha yamevunjwa kutokana na nguvu kutoka nchi ya Kiislam ili kuivuruga Tanzania.

Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba yeye akahitimisha kwa kusema kuwa waliovunja mabucha si Waislam ila ni wahuni wanaotaka kupindua serikali.

Kufika asubuhi siku ya Jumamosi masheikh 40 wakawa wamekamatwa usiku wa manane kwa taadhira kubwa majumbani kwao mfano wa majambazi na kutiwa korokoroni.

Wahariri wa magazeti asubuhi yake siku ya Jumamosi wakawa katika burdani kubwa ya kuandika kuvunjwa kwa mabucha ya kuuza nguruwe na kukamatwa kwa masheikh.

Asubuhi ile ya Jumamosi kundi dogo la Waislam wakaenda Kituo Cha Kati cha Polisi kufuatilia masheikh waliokamatwa usiku na kuwekwa korokoroni hapo.
Hawa nao wakakamatwa na kuwekwa ndani.

Haukupita muda baada ya habari kuenea kuwa Waislam waliokwenda kuwauliza masheikh na wao wamekamatwa Waislam wakaja kwa wingi kituoni siku ya pili yake Jumapili iliyokuwa Easter Sunday.

Siku hiyo Waislam wakakusanyika pale kituoni ikawa kama vile kituo kimezingirwa na sala ya L'Asr ilipoingia ikapigwa adhana pale nje ya ya kituo watu wakasali barabarani.

Polisi wakataka kuwapiga mabomu ya machozi lakini pakawa na kutokubaliana baina ya askari wenyewe.

Hawakupendezewa na kitendo kile.

Askari Waislam wakawaambia wenzao hilo haliwezi kufanyika kuwapiga mabomu Waislam wanaosali kwani ni kufuru kubwa Waislam hawajafanya fujo wamekuja kituoni kufuatilia masheikh wao walioko korokoroni.

Jua lilipotua Waislam wakaondoka pale kituoni wakaamua wakutane siku ya pili Msikiti wa Mtoro washauriane.

Siku hii ya Jumapili yaani Easter Sunday mimi ndiyo niliingia Dar es Salaam nikitokea Le Havre, Ufaransa nikaja Paris kwa muda wa siku mbili kisha nikaenda London kisha Cardiff na kurejea London kupanda ndege kurudi Dar es Salaam.

Nilipofika nyumbani ndipo nilipopata taarifa ya masheikh kukamatwa na kati ya masheikh hao alikuwa mjomba wangu Sheikh Pazi wa Manzese.

Sikusubiri nikaenda kwa Hassan Chikusa wakati huo akiishi Mwananyamala kwani nilijua pamoja na kupita kwa jamaa wengine yeye ndiye ataweza kunipa taarifa ya mkasa mzima pamoja na tathmini.

Hayo niliyoandika hapo juu ni baadhi ya mambo aliyonifahamisha kuwa yametokea kuanzia siku ile ya Ijumaa yalipovunjwa mabucha hadi siku ya pii yake Jumamosi.

Hili ninalosema sasa ni jambo ambalo kwa miaka yote kila nilipokutana na Hassan moyo uliniuma sana nikiishia kumuombea dua.

Hassan siku ile nilipokwenda kwake ilikuwa Jumapili usiku na hakuwa na taarifa kuwa siku ya Jumatatu, yaani Easter Monday Waislam wameamua kufanya shura ndani ya Msikiti wa Mtoro ambao Imam Mkuu, Sheikh Kassim Juma alikuwa kakamatwa Arusha akielekea Nairobi kwenye matibabu na kurudishwa Dar es Salaam na yuko rumande.

Mimi ndiye nliyemfahamisha kuwa kesho Easter Monday kuna shura ya Waislam wote wa Dar es Salaam kujadili kwa pamoja nini kifanyike kurejesha heshima ya masheikh wetu.

Hassan aliniuliza kama mimi nitakuwepo.
Nikamwambia In Shaa Allah nitakuwapo.

Hassan Chikusa na yeye akaniambia atakuwapo pia.

Kwa ufupi siku ile ndani ya Msikti wa Sheikh Mtoro Mwinyi Mangara iliamriwa baada ya mjadala mkali sana Waislam watoke kwa maandamano hadi Kituo Cha Kati Cha Polisi kwenda kuwatoa masheikh wao korokoroni.

Katika maandamano yale Waislam walipambana na polisi na mabomu ya machozi yalipigwa.

Mapambano haya yalifanyika kati ya kituo cha polisi na Clock Tower.
Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza ya Waislam Tanzania Bara.

Zanzibar maandamano yao yalikuwa mwaka wa 1988.
Maandamano haya yote tatizo ni Uislam.

Hassan Chikusa akakamatwa pamoja na vijana wengi wa Kiislam.
Wakawekwa rumande wakashtakiwa na kuhukumiwa vifungo jela.

Hassan Chikusa akapoteza kazi yake NBC.

Huyu ndiye Hassan Chikusa msomi mkimya ambae baada ya kutoka jela akiwa hana kazi masahibu mengi ya maisha yalimfika.

Lakini siku zote akisema yaliyomfika ni madogo sana na yote ameyakadiria Allah na na yeye bado yu hai.

Kwangu mimi maadamano yale na wale walioshiriki katika yale maandamano kile kilikuwa kipimo.

Tunamuomba Allah amsamehe makosa yake mja wake huyu na amtie Firdaws.
Amin.

View attachment 2305229
Hassan Chikusa​
RiP - Niliwai kuwa nae Karibu Kibiashara wakati Nnaishi na Kusoma South Africa JohanesBurg ! Tulikuwa tunakaa Gorofa moja .Sikuwai jua hii story yake 😭😭😭. Miaka ya Hivi Katibuni alikuwa anaandika Kitabu, sijui kama amekimaliza au la! Mwenyezi Mungu amrehemu.
 
RiP - Niliwai kuwa nae Karibu Kibiashara wakati Nnaishi na Kusoma South Africa JohanesBurg ! Tulikuwa tunakaa Gorofa moja .Sikuwai jua hii story yake 😭😭😭. Miaka ya Hivi Katibuni alikuwa anaandika Kitabu, sijui kama amekimaliza au la! Mwenyezi Mungu amrehemu.
Chipukizi,
Amin.
Kitabu alikimaliza.
 
Machine...
Mbona nipo tunajadili?

Ukiona simjibu mtu ni kuwa hana ustaarabu.

Lakini ikiwa mtu ananiandikia kwa heshima na adabu najibu maswali yake.
Mfano niliuliza katika post number #37 unisamehe pengine nilitumia lugha mbaya pasipo kujua, japokuwa sikuona tatizo lolote katika maswali yale.

Nilicho ona watu wengi wana gadhabika kwa sababu umeandika vitu vigumu na vinavyo weza pelekea kulete utofauti baina ya makundi katika jamii, vitu hivyo vinahitaji maelezo mapana sambamba na maswali yatakayo ibuliwa kuwa yajibiwe.

Sasa watu wanakuona ni mdini au mchonganishi pale ambapo mada yako hii haijibiwi maswali yanayo ulizwa ndio hupelekea watu kufungua hasira yao
 
Loyol...
Maswali kama haya si lazima nijibu mimi unaweza hata wewe mwenyewe kufanya utafiti utapata majibu unayoyatafuta.

Wajomba zangu wawili Sheikh Pazi na Shomari Lupindo wakiishi Manzese kwa miaka mingi toka mimi ni mtoto na sasa nina miaka 70.

Kwa hiyo naijua Manzese vizuri sana.
Nimezaliwa Dar es Salaam.
Sasa wewe mzee ndo umejibu nini hapa? 😁😁
 
Hizo sehemu zote ulizopitia nina wasi wasi nazo. Hizo ndo vichaka vya wafia dini ya kiislam.
1658954919578.png


🤣 🤣 🤣 🤣
Kwa hiyo unaona Mzee Saidi ameandika kwa code..
Yaani aliiingia Karachi , akitokea Kandahar, akaja Kabul kwa siku mbili halafu akaenda Baghdad, kisha akaenda Aleppo, na kurudi Baghdad na kupanda ndege kwenda Tehran... 😂 😂 😂
 
View attachment 2306285

[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Kwa hiyo unaona Mzee Saidi ameandika kwa code..
Yaani aliiingia Karachi , akitokea Kandahar, akaja Kabul kwa siku mbili halafu akaenda Baghdad, kisha akaenda Aleppo, na kurudi Baghdad na kupanda ndege kwenda Tehran... [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hapo alimaa nisha..alitoka magomeni akaenda manzese..kisha mwananyamala..then kigogo..kisha temeke sudani..akarudi kimboka..then yombo..kisha magomeni.

Mzee janja janja nyingi sana anapenda kujipaisha aonekane anahadhi kumbe mhuni tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
View attachment 2306285

🤣 🤣 🤣 🤣
Kwa hiyo unaona Mzee Saidi ameandika kwa code..
Yaani aliiingia Karachi , akitokea Kandahar, akaja Kabul kwa siku mbili halafu akaenda Baghdad, kisha akaenda Aleppo, na kurudi Baghdad na kupanda ndege kwenda Tehran... 😂 😂 😂
Tek...
Naona niweke picha nikiwa Tehran.
1658956208384.png

Nikiwa na watangazaji wa Radio Tehran 2006
 
View attachment 2306285

🤣 🤣 🤣 🤣
Kwa hiyo unaona Mzee Saidi ameandika kwa code..
Yaani aliiingia Karachi , akitokea Kandahar, akaja Kabul kwa siku mbili halafu akaenda Baghdad, kisha akaenda Aleppo, na kurudi Baghdad na kupanda ndege kwenda Tehran... 😂 😂 😂
Tek...
1658956384525.jpeg

Voice of America (VoA), Washington DC 2011
1658956712866.png

University of Khartoum 1998
 
Tekno...
Nasikitika na kuhisi vibaya kuwa mtu atanitukana kwa kuwa tu nimeeleza historia ya jamii yangu.
Mzee Said
JF ya siku hizi imejaa vitukuu na vilembwe vilivyo potezwa na zama za teknohama na hivyo kutokuwa na heshima wala staha.
Taasisi za elimu ziko na kipaumbele cha kutoa Quantity kuliko Quality ili zijipatie fedha za ada zaidi na zaidi... na matokeo yake ni kizazi kinachoona kimeendelea kwa uwepo wa teknolojia mpya ya kuwafanya kuwa tegemezi bila kuwa na uwezo kufikiri kwa kutumia akili binafsi...
 
Askari Waislam wakawaambia wenzao hilo haliwezi kufanyika kuwapiga mabomu Waislam wanaosali kwani ni kufuru kubwa Waislam hawajafanya fujo wamekuja kituoni kufuatilia masheikh wao walioko korokoroni.


Siku hii ya Jumapili yaani Easter Sunday mimi ndiyo niliingia Dar es Salaam nikitokea Le Havre, Ufaransa nikaja Paris kwa muda wa siku mbili kisha nikaenda London kisha Cardiff na kurejea London kupanda ndege kurudi Dar es Salaam.

Kwa ufupi siku ile ndani ya Msikti wa Sheikh Mtoro Mwinyi Mangara iliamriwa baada ya mjadala mkali sana Waislam watoke kwa maandamano hadi Kituo Cha Kati Cha Polisi kwenda kuwatoa masheikh wao korokoroni.

Katika maandamano yale Waislam walipambana na polisi na mabomu ya machozi yalipigwa.

Mapambano haya yalifanyika kati ya kituo cha polisi na Clock Tower.
Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza ya Waislam Tanzania Bara.
 
Huyu mwanahistoria sijawahi kuona akiandika makala inayohusu chochote bila kuingiza uislam.

Imefika hatua unajua yaliyomo yanahusu uislam hata kama kichwa kiko tofauti.

Anyway endelea kupambania uislam wako maana sijawahi ona ukiandika mazuri ya wala kitimoto maana ni kama hawana jema hata moja.
👍🙏
 
Back
Top Bottom